Lindi na Mtwara yaingiza Sh 162.9 bilioni za mauzo ya ufuta

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1564907743312.png


Mikoa ya Lindi na Mtwara imeingiza Sh162.9 bilioni zitokanazo na mauzo ya zao la ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Kilo moja ya ufuta imeuzwa kati ya Sh2,650 hadi Sh3,100 kwa msimu wa mwaka 2018/2019 .

Hadi kufikia jana Jumamosi, Agosti 3, 2019, mikoa hiyo imeshauza ufuta tani 59,208, Mkoa wa Lindi ukiwa kinara kwa kuuza tani 52,232 na kuingiza Sh144.6 bilioni na Mtwara ukiuza tani 6,975 na kuingiza Sh18.2 bilioni. Akisoma taarifa ya mikoa ya kusini katika ufunguzi wa maonyesho ya Nanenane kanda ya kusini, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amesema kutokana na mauzo hayo, halmashauri 15 za mikoa hiyo zimeingiza zaidi ya Sh4.9 bilioni.

“Lindi tumeingiza Sh4.3 bilioni na Mtwara Sh377.7 milioni , niwapongeze wakulima kwa kuendelea kuiamini Serikali na kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani, ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kusimamia kazi ya ukusanyaji wa ufuta mpaka kuuzwa,” amesema Shaibu.

Mkuu wa wilaya ya Masasi, Selemani Mzee akifungua maonyesho hayo kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), amesema Bajeti ya 2019/20 iliyopitishwa na Bunge, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetengewa Sh318.4 bilioni. “Kilimo pekee kimetengewa Sh253.8 bilioni, Mifugo na Uvivu Sh64.9 bilioni ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2018/19 zilitengewa 26.7 bilioni.

Kwa hiyo hapa kuna ongezeko kubwa la bajeti,” amesema Mzee. Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga amesema zao la ufuta linaweza kulimwa zaidi ya mara moja kwa mwaka kama kutakuwa na uwezekano wa kumwagilia.

“Katika kituo chetu tuna shamba la kuzalisha mbegu lakini tunazalisha kwa njia ya umwagiliaji na unaweza kuvuna mbegu kwa mwaka mzima, sasa kwa wakulima kinachohitajika ni kuwa na uwezekano wa kuwa na umwagiliaji,” amesema Dk Kapinga.
 
Tukiwekeza kwenye kilimo na viwanda(processing industiries) tutafika mbali sana ila tumekazana kujenga miundombinu ya matrilioni huku kilimo tunakisau(tunatoa ajira kwa wageni kupitia hii miradi na hivyo hela nyingi zinatoka humu nchini na kuenda kwa mabeberu) huku sisi tukibaki masikini na watu wetu hawana ajira!

Kingine,tuna mifugo mingi ambayo inazalisha ngozi kwa wingi na tungekuwa tunafikiri sawasawa,ngozi hizi ni raw material kwa uzalishaji wa bidhaa kama viatu ila hatuna mkakati wowote wa kutumia mazao yatokanayo na mifugo kujenga nchi yetu kupitia mapato ya mauzo ya nje kwa bidhaa tutakazozalish na kuziuza nje ya nchi bali tunaona ufahari kugharamia miradi ya matrilioni(mingine isiyo na ulazima kwa sasa) na kuwapa wenzetu wa nje ajira mbali na kuondoka na fedha tunazowalipa na kuzipeleka kwao.
 
Tukiwekeza kwenye kilimo na viwanda(processing industiries) tungefika mbali sana ila tumekazana kujenga miundombinu ya matrilioni kilimo tunakisau(tunatoa ajira kwa wageni na zaidi hela nyingi zinatoka humu nchini na kuenda kwa mabeberu) huku sisi tukibaki masikini na watu wetu hawana ajira!

Thanks for that, kaa tunataka kuendelea lazima katika budget yetu kiwango cha juu kabisa kiwe katika kilimo, ndio tupate enough raw materials, ambazo inturn zitawezesha ziwada vya agri proccessing kufanya kazi,, na kutengeneza ajira tosha kwetu sis, sasa mkuu niambie hii sgr je italeta ajira ngapi?

Steiglers george itakamilika lini? italeta ajira ngapi? lakini tukiwekeza kwa kilimo in less than 5 years, tz will be way way ahead, lets focus on agri-manufacturing, agri-proccessing, lakini shida huyu mkubwa hataki kuambiwa yeye ni mtaalamu wa kila kitu mkuu
 
Thanks for that, kaa tunataka kuendelea lazima katika budget yetu kiwango cha juu kabisa kiwe katika kilimo, ndio tupate enough raw materials, ambazo inturn zitawezesha ziwada vya agri proccessing kufanya kazi,, na kutengeneza ajira tosha kwetu sis, sasa mkuu niambie hii sgr je italeta ajira ngapi? steiglers george itakamilika lini? italeta ajira ngapi? lakini tukiwekeza kwa kilimo in less than 5 years, tz will be way way ahead, lets focus on agri-manufacturing, agri-proccessing, lakini shida huyu mkubwa hataki kuambiwa yeye ni mtaalamu wa kila kitu mkuu
Viongozi wetu hawawazi sawa sawa na hili ndio tatizo!!
 
Aaah sky eclat lazma ununue ila nasikia wanalipa ila asilimia 30.Korodhw cjui imeingza shngap
 
Back
Top Bottom