SoC02 Linda sana hisia zako

Stories of Change - 2022 Competition

Africanicity

New Member
Oct 16, 2020
2
2
Linda Sana hisia zako zisije kukupa au kukupatia madhara baadae kwenye Maisha yako, hata kama zitakuwa au kuonekana chanya kiasi gani kwa Wakati huo, usiwe mwepesi wa kuzionesha kwa Kila mtu na kwenye Kila kitu. jaribu kutumia Akili kabla ya hisia zaidi,hii yaweza kukusaidia kwa baadae.

Mtu aweza kusema inawezekanaje na itakuwaje endapo nitafanya hivyo? Ngoja nikuambie Maisha yanakuwa ni Mazuri unavyoweza kuelezea hisia zako kwa watu wengine na wakati wengine wanapata Tiba kupitia hizo.

Kwanini? Kwasababu hisia uweza kutoa Tiba au manufaa kwa watu wengine, lakini ugonjwa unapokuwa umeponeka na kutoweka ndipo watu uanza kutumia Akili zao wakati huo.Panapo majaliwa kama kutakuwa na faida baina ya pande mbili,basi inakuwa ni heri zaidi lakini inavyokuwa si ndivyo ndipo shida inapoanza kutokea.

Sijaelewa🤗! Endelea kusoma
Ndio maana tunaona na kushuhudia kwa watu wengi wanavyoanza kutongozana Ili waweze kuwa wapenzi,wengi uendeshwa na hisia zaidi kuliko Akili. Hii utaona upande wa mwanamke au mwanaume.

kwa upande wa mwanamke anakuwa na Mawazo ya vitu vingi ambavyo hata kwenye Maisha yake harisi ya nyumbani kwa baba au mama hajawai hata kuyaona au kwa walezi wake. kwa mfano kupendwa zaidi yeye kuliko mtu Yeyote,kupata Mahaba Moto Moto kuliko mtu Yeyote,Zawadi nyingi,muda mwingi kuwa karibu na ampendae,kusikilizwa bila kukosolewa,kupewa kipaumbele zaidi kushinda mtu Yeyote.

Muda mwengine uenda mbali Mbali kwa kudhani katika utashi wake kwamba asipompa ngono mwenzi wake kipindi cha uchumba ni kuonesha kutokumjali mwenzi wake,na hata wenzi wakati mwengine kudhani hivyo ndivyo sahihi. Hii mara ya nyingi uletwa na hisia kuliko matumizi ya Akili.

Kwasababu ingetumika Akili zaidi ya hisia wangejali afya zao,utu wao,dhamani Yao kabla ya kuingia huko kipindi za uchumba, na ndiyo maana tunaona watu kuachana baada ya kutimiza tamaa zao za mwili,mimba zisizo na baba,ugomvi unaotokana na ujauzito,maradhi na watu kubwagana pia na wakati mwingine Mapenzi kufa.

Kwa mtizamo wangu ni kwamba kumpenda mtu hakutokei Kwa mara moja tu,Bali ni hatua ya kuwa ndani ya husiano au Mahusiano. kwa mfano mama kumpenda mtoto ni hatua kutoka kipindi cha mimba au ujauzito,kujifungua na uhusiano kipindi baada ya kujifungua.Ndio maana utasikia mama anasema huyu mtoto nilimchukia au kumpenda tangu nikiwa na ujauzito. kwahiyo swala ya kupenda siyo ajali ya siku moja.

Watu wengi wanapoakuwa kwenye hatua za kutongozana utasikia "Mimi nimetokea kukupenda kwa Moyo wangu wote" badala ya "Mimi nimepata na mvuto mkubwa(hisia) au Mimi nimevutiwa na wewe" . Hii kwa mara ya Kwanza huwa ni Mvuto au hisia kwa mtu na siyo Upendo au kumpenda MTU.

Kwahiyo kwa ufinyu wa Mawazo au Fikra zao kuwa finyu na kuedeshwa na hisia na Wala si Akili wengi ujikuta kuingia katika shida na Matatizo ya kutokuelewa kama ni mivuto iliyotokea au ni Upendo. Hii huwa ni njia panda ya bila ya kwao kutambua kwamba wapo kwenye mvuto na si upendo

Pia kwa wanawake uenda mbali zaidi na kusema " uhusiano huu ni kwaajili ya kunichezea au kunioa" Hisia zimechukua nafasi kubwa kushinda akili. kama akili zingetumika vijana na mabinti wengi wangejua kuwa kipindi cha uchumba ni kipindi cha matazamiao,ni kipindi ambacho ni cha uangalizio kabla ya Ndoa au kuoana.

Kutoa ngono kipindi cha uchumba kudhani ndiyo kuonesha Upendo,rashaha ni ku expose hisia zako kwa mtu ambaye hujui kwa baadae kama atakuwa pamoja na wewe au sivyo, au ataheshimu hisia zako au sivyo.

Ni kuwa makini kwa dada zangu au watoto wa kike. kwahiyo kama hisia zako zitachezewa,na dhamani yako itashuka na muda mwingine kukupelekea kuaibika katika jamii. Jinsi utavyokuwa mwepesi ku Expose hisia zako kwa watu tofauti tofauti bila kutumia Akili,siku zote utaumizwa na kudhalilika au hata muda mwingine kushusha dhamani yako.

Dunia tulinayo ni dunia ambayo chako ni chetu lakini chetu ni chetu hakiwezi kuwa chako. Pia kitu cha kujua ni kwamba Upendo wawezwa kutengeneza na pia wawezwa kuharibiwa. kwahiyo Upendo hauwezi kuwa ni tukio la ghafla (accidentally),lazima liweze kuwa ni la muda mrefu.

Kwa upande wa wanaume wao udhani kwamba wanavyokuwa kwenye hatua ya awali ya Mahusiano ni kwamba mara zote ni lazima kumfanyia Mpenzi wake au mwenzi wake kuwa na Furaha wakati wote,ni kumuonesha kumjali mwenzi wake kwa Mali na Hali. Sasa ndiyo utakuta Wanaume wengi uingia katika maisha ambayo hawana uwezo nao kama kumfanyia manunuzi(shopping),kumtoa nje (outing),kumfanyia shererehe ya kuzaliwa mwenzi wake (birthday party) kwa kutumia hisia zaidi ya Akili.

kama wengi wangetumia akili kushinda hisia zao wangeweze kutafakali Hali zao za uchumi na Maisha yao kiujumla kama wangeweza kumuda au si ndivyo. Lakini zaidi ya asilimia kubwa uendeshwa na hisia zaidi na kujikuta wameingia gharama ya muda na Mali Kwa kiasi kikubwa na baadae baada ya hisia kufikia kikomo hujikuta na masononeko,Udhuni,mfadhaiko na hasira muda mwingine.

Na ndiyo maana wengi ubaki na malalamiko kwa wenzi wao au wapenzi wao kwamba hukujali hata muda,Mali na hisia zangu zote kwako. Hii mara nyingine ikienda zaidi ya utu hujikuta hutenda unyama na unyanyasaji kwa wenzi wao kama wa Ngono na mengineo kadha wa kadha.

Mwisho wa hisia kama hizi huwa ni hatari Kwa mabinti wengine au wanawake wengine kama wataweza kukutana na watu kama hawa waliodhulika au kupata madhara ya mara ya Kwanza kwa watu mabinti au wanawake wengine.

Hii upeleke wanaume wengine kuingia kwenye Mahusiano na wanawake au mabinti wengine kwa lengo la kufidia hasara au hasira walioipata kwa wenzi au wapenzi wa mwanzo. Hii huwa ni hatari kwa watu wote na si kwa wanawake tu. Kwasababu hata wahenga husema “hasira ni hasara”

Wanaume hudhuni suluhisho la hayo yote ni kuwaingulia wanawake na kuwaacha na kuendelea na Maisha Mengi na wengine kuwapatia madhara au magonjwa kama UKIMWI/VVU kwa lengo la kuponesha majeraha au hasira kwa hawa wanawake au mabinti wengine.

Pia kuna misemo mingi inayotunika mtaani kwamba “wewe piga alafu pita hivi” au “uoe wa Nini wakati kijana meno ipo” Hii si hasara kwa upande wa wanawake na mabinti tu Bali na kwa wanaume na jamii mzima

kwa mfano mimba zisizo na baba,ndoto nyingi kufia njiani,kukatisha masomo,umaskini,ongezeko la watoto wa mtaani,kukataliwa kwa watoto wakike katika familia zao au jamii zao,kufungwa au vyombo vya dola kuhusika,ugomvi baina ya familia moja na nyingine,chuki,hasira,visasi baina ya wapenzi, na Ndoa za Utotoni.

Hii pia yaweza kutokea Kwa upande wa wanawake lakini kwao huwa si asilimia kubwa kama kwa wanaume. kwa mfano kutoa mimba kwa lengo la kukwepa majukumu ambayo hayawezi lakini wengi huweza kulea ujauzito kama jamii inayomzunguka kumkubali na Hali yake na kuwa karibu Naye.

Mara nyingi pia tuliona au kuambiwa au kusikia kwamba wakati wa zamani wanaume waliweza kuchaguliwa wanawake na wazazi wao katika jamii Yao au jamii iliyo karibu nao. Sisemi kwamba ni lazima iwe hivi,lakini najaribu kutoa tadhimini yangu fupi kwa mawazo yangu.
Kwa watu wa kale

Hii iliweza kutengeza ulinzi kwa wapenzi au wezi, kwasababu kama kukitokea tatizo ni lazima familia za hawa wapenzi waweze kujua ni Nini tatizo lilipo baina ya hawa watu wawili, kwasababu wapenzi hawa kutokea eneo moja ambapo ni rahisi kutambua tatizo na kuweza kujua pale endapo mmoja atakuwa kaweza kurudi Nyumbani na kukaa au kuonekana mara kwa mara katika maeneo Yao au katika Kijiji Chao.

Pia iliweza kutengeza uhalisia halisi wa Maisha na kujuana kiundani zaidi baina ya hawa watu wawili kiuchumi,Mahusiano,tabia,magonjwa,vyakula,Imani au kuamini na kadhalika. Kwahiyo hakuwa na jambo gumu kuelewana au kutambuana kwa Wakati huo. Pia ilikuwa ni ngumu kudai au kufanya kitu ambao kipo juu ya Uwezo wao, kwasababu ya utambuzi wa Hali zao zilivyokuwa kwa Wakati huo.

Lakini leo katika Karne yetu ya 21 imekuwa tofauti kulingana na nyakati na muda pia. Mambo mengi yamebadilika na yamekuwa tofauti na wakati huo. Hii haimaanishi maisha hayawezi kuendelea ya kuoa na kuolewa au uchumba. Mambo ni lazima yaendelee.

Leo watu wanaongia katika uchumi si wajamii mmoja au Taifa moja,watu wamekuwa na mwingiliano mkubwa na pia hata changamoto zimekuwa tofauti na zile za kale.

Kwa mfano, mwanafunzi wa chuo anaweza kukutana na mwanafunzi mwengine chuoni na kuhahidiana kwamba watukuja kuona watakapo kuja kumaliza chuo. Hii yaweza kuwa ni kitu kizuri lakini kama kitaongozwa na hisia za mwili na Wala si za Akili ndipo hatari inapokuja kwao.

Wengi ndoto zao huwa ni kwenye picha na siyo uhalisia kwao. Uishia kwenye ngono tu na tamaa ya Mwili. Hii utokana na kutokujua kwamba wao ni watu walio tofauti katika nyanja mbali Mbali kama vile Malezi,familia zao,jamii zao,mtazamo,kimawazo,kiuchumi,kiimani au katika kuamini,katika kutafakali,kufikili na kutenda,kuchukulia ,magonjwa au maradhi au magonjwa mbali Mbali ya kuridhi au kutoridhi na vitu vingi kama hivyo.

Kwahiyo kama kudhaminiana na kuvumiliana au kuchukuliana pia inahitaji muda kufamiana kiundani zaidi katika utofauti wa mambo hayo kama uchumi wao,tabia zao,magonjwa na vitu vingine. Bila kuwepo kwa uvumilivu baina Yao na kupeana muda na nafasi Ili kila mmoja aweze kumjua au kumfahamu mwenzi wake kwa kupata taarifa kutoka kwa mwezi wake au jamii yake katika mambo mbali Mbali,hii itapelekea mmoja kudhani kwamba mwenzi wake hampendi au hamjali na kutaka yeye kuwa chini yake na kutawaliwa kwenye Kila jambo

Hii ni kwasababu mmoja au wote kutaka kuwa mkubwa au mtawala(dominant) dhidi ya mwengine. Hii utokana na kuto tafakari au kuto tumia akili kwamba wote ni watu tofauti na wametokana na jamii tofauti. Hii upelekea leo hii kuona Mahusiano mengi kufa au Ndoa nyingi kufika hatima au mwisho kwa haraka zaidi na kila mmoja wao kubaki na bumbuwazi. Hii utokea kama sintofahamu Fulani hivi baina yao

Hali ya kufahamiana au kujuana katika utofauti huo walionao inawawezesha wapenzi wote kutochukulia kitu kibinafsi( don't take it personally) na kuwa na wigo mpana wa kujua utofauti huo na kuchukulia tu katika utofauti huo na si sababu ya mtu mwenyewe kutenda kwa kujifurahisha mwenyewe au kutaka mmoja apate shida au mateso

Hali hii ikifuatwa kwa hisia zetu bila tafakari zetu zinaweza kuwa ni shida kila siku kwa watu au wapenzi,hii itaweza kusaidia jamii yetu kiujumla na TAIFA.

wapenzi ni lazima waweze kujuana kiundani zaidi katika tofauti zao bila kificho, kwasababu kweli siku zote huwafanya watu kuwa huru bila kubaki na makando Kando kadha wa kadha. Lakini katika jamii zetu wanadhani kufanya tofauti zetu kutojulikana kwa watu ni udhaifu na ndiyo maana mambo mengi huwa na madhara makubwa kwa baadae ukweli unapojulikana .

kitu ambacho hawajua ni kwamba udhaifu haupo katika kuweka utofauti wetu wa kimaisha yetu kwa watu wengine, Bali ni kuweka hisia zetu kwa Kila mtu. kwa mfano kumwambia mwezi wako ugonjwa au magonjwa yanakusumbua wewe au jamii yako ni faidi kwenu na kwa jamii zetu zote na kwa jamii au vizazi vijavyo baadae.

Hitimisho
Hisia zetu za mwili zishindwe na hisia zetu za ndani (Akili) siku zote Ili iwe faida kwA Kila mmoja wetu. Hisia za nje ya Mwili ni hatari kama zitawala mambo ya ndani kushinda hisia zetu za ndani zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom