Likizo gani hizi;mnasumbua watoto wetu

MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,013
1,443
hivi ndo likizo gani mnazowapa wanafunzi wetu, yaani watoto wanakaa wiki mbili halafu wanarudi kusoma wiki 2,then wanfunga tena, This is totally insane!Kwa taarifa yenu watoto hawasomi na waalimu hawafundishi,watoto wanacheza mpira tu na waalimu wanapiga soga!It does not make sense at all:watoto wamefanya mitihani na matokeo wamepewa from what miracles waalimu wao watahangaika kumfudisha mtoto kwa wiki mbili then wafunge shule! You good people could help in this, huku ni kusumbua watoto!Sie wote tumetoka huko na sasa tuna fanya vitu ambavyo tusingependa kufanyiwa!Ndio kwani nani angetaka apewe likizo za mikatomikato kama hii, eti kwa sababu ya sensa,ipi hiyo kwa minajili ipi,kwani huko likizo kunazuiaje sensa,watoto wanaweza kuhesabiwa nyumbani au shule!Mtoto anayesoma boarding na wazazi wako mbali ataweza kweli hii nenda rudi yenu!KAMA WIZARA ICHOKA KUFIKIRI NAMNA BORA YA KUUNGANISHA MATUKIO WANGEOMBA USHAURI HATA KWA WATOTO WENYEWE,NINA HAKIKA WANGEPATA USHAURI MZURI KULIKO HAYA WANAYOFANYA!HII SIO HAKI KWA WATOTO NA WAZAZI!
 
unalalamikia shule gani fafanua mkuu,kajamba nane,kidumu na ufagio,kayumba au jamii ya st marysna kenton ukinipa majibu ntachangia
 
Tatizo kubwa ndani ya nchi mambo hayaendi kitaalam mambo yanaendeshwa kisiasa zaidi kwani kungekuwa na info kuhusu sensa kuanzia mwaka jana ina maana wataalam wizarani wangepanga taratibu za likizo, kwa kuwa walishtukizwa na walikwisha tuma taratibu zao kwa wakuu wa shule ndivyo wamegeuza ili mradi kifanyike tu .
 
unalalamikia shule gani fafanua mkuu,kajamba nane,kidumu na ufagio,kayumba au jamii ya st marysna kenton ukinipa majibu ntachangia

Nivea karibu shule zote hapa nchi hali ni hari jojo walikuwa likizo tare23/06 wamerudi 30/06 na watafunga 04/08 to 08/09 je huoni ni usumbufu?
 
nivea hapa zinazungumziwa shule za msingi za serikali
 
Last edited by a moderator:
Nivea karibu shule zote hapa nchi hali ni hari jojo walikuwa likizo tare23/06 wamerudi 30/06 na watafunga 04/08 to 08/09 je huoni ni usumbufu?

Wanadai eti walifunga ili kutoa nafasi kwa wanafunzi waliokuwa wanashiriki UMITASHUMTA kule Tanga, na hiyo tar 4 Aug ndpo walimu wataochaguliwa watakapoanza semina za sensa baadae kufuatiwa na sensa yenyewe. Well, tuseme nini sasa? Mipango hovyohovyo inayosimamiwa na serikali dhaifu!
 
unalalamikia shule gani fafanua mkuu,kajamba nane,kidumu na ufagio,kayumba au jamii ya st marysna kenton ukinipa majibu ntachangia

Zote mchanyange!!! Maana yake zote zote kasoro International Schools (ambazo nchini hazizidi tano hivi)!!!
 
Ni shuel zote tu hata private. kwa mfanao Marian Girls wamefungua June 23 wanafunga tena August 18 et sababu ya sensa. Mtoto ametoka tabora au bukoba anasafirui kila mwezi. Uozo huu
 
unalalamikia shule gani fafanua mkuu,kajamba nane,kidumu na ufagio,kayumba au jamii ya st marysna kenton ukinipa majibu ntachangia

shule zote wakati wa sensa wanafunz watarudi makwao pambaf we acha kubisha kila unachoambiwa kwan uko st wanasoma manyani wasihesabiwe
 
Back
Top Bottom