NJAKIHUTIKO
Member
- Oct 10, 2023
- 49
- 43
Ameoa huko huyu DC....?Mkwe wa Ndugai yupo!
Namanyele 😂😂😂
Ameoa huko huyu DC....?Mkwe wa Ndugai yupo!
Namanyele 😂😂😂
Nabii Lema alitabiri kuwa Mfadhili wao atakata roho wakafikiria ni utani.Hatimay Mwenyezi Mungu akamwondoa aliyewapa hii Kiburi mpaka leo wamepoteana.
Nilijuwa wana ubavu huo kumbe walikuwa wanategemea Mwanadamu
Hahaha dc wa mchongoDC kabla ya suspect kuwa arrested ni LAZIMA awe na docket police, DC nenda kwanza kafungue kesi police ili uchunguzi ufanyike, kama kuna kesi ya kujibu then ukamataji ndio utafanyika,upumbavu wa DC
Kwa kweli inashangaza sana.Sifa kuu ya kwanza ya utanzania ni unafiki.
Suti ya Jualikali ni Moto sana iwekwe Makumbusho ya TaifaView attachment 2807083
Basi sawa Mwishimiwa
Anakamatwa kwanzaHahaha kwanini asimfungulie mashitaka kwanza kama kuna kosa akalitenda? kisha mahakama itampa taarifa ikiona anakosa la kujibu.
Kila mtu ana mamlaka ya kutuma polisi kukamata watu nchi hii.
View attachment 2807083
Basi sawa Mwishimiwa
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, ili ahojiwe kwa alichoeleza "kutoa kauli za uchochezi" kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 24, 2023.
Katika video ambayo inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, Lema anahamasisha wanaume wa Kijiji cha Korongwe Asilia, wamuue Mtendaji wa kijiji chao kwa madai ya kuwasumbua wananchi.
Hata hivyo Lema amezungumzia video hiyo kuwa, hakuhamasisha kitu kama hicho na asingeweza kutoa kauli kama hiyo badala yale aliwaambia wanaume wamuoe mtendaji huyo ili asiwasumbue jambo ambalo amejitetea kwa kusema "lugha za kisiasa."
Kwenye video hiyo, Lema akiwa na baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema katika Vitongoji vya Forodhani na Fipa, Kata ya Korongwe, anaonekana kutamka neno
ambalo limetafsiriwa na Mkuu wa
Wilaya kuwa ni kutaka wanaume wamuue mtendaji anayewasumbua.
Lijualikali amesema haiwezekani kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa watu aachiewe kutamba kwa kauli hiyo ambayo imesababisha taharuki kwa wananchi na Mtendaji huo ambaye kwa sasa maisha yake yako shakani, huku kiwango cha utendaji kikishuka.
"Namuagiza OCD wa Nkasi, kuchukua hatua za kisheria mara moja kumuita kokote aliko Godbles Lema ili afike Nkasi akafanyiwe mahojiano kuhusu kauli yake ya kichochezi ya kuhatarisha hali ya usalama wa mtendaji huyo katika eneo letu na kukwaza juhudi za wananchi kufanya shughuli za maendeleo," amesema Lijualikali.
Akijibu swali ni kwa nini jambo hilo lilitokea muda mrefu lakini wamechelewa kutoa taarifa, Mkuu wa Wilaya amesema walianza kwa uchunguzi kuhusu kauli hiyo ilikuwa na maana gani na ililenga nini kitokee na kwamba wamejiridhisha haikuwa kauli nzuri.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali ameagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo na kumkamata Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema ili ahojiwe kwa kauli za uchochezi alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara Oktoba 24,2023.
Kwenye Mkutano huo ambao ulifanyika katika kata ya Korongwe jimbo la Nkasi Kaskazini ambako anaelezwa kuwa alitamka kuwa wanaume wa Kijiji Korongwe asilia wamuue Mtendaji wa Kijiji hicho Daud Ismail.
Hata hivyo Lema amekanusha madai ya uchochezi huo akisema alitamka kuwa wanaume ‘wamuoe’ mtendaji huyo akidai ni lugha za kisiasa na wala hakuna madhara yoyote kuhusiana na utendaji wake.
Imedaiwa Lema akiwa na baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema kwenye mkutano huo katika Vitongoji vya Forodhani na Fipa, Kata ya Korongwe, kwa makusudi alitoa kauli ya vitisho kwa mtumishi huo baada ya wananchi kulalamika kwenye mkutano huo kuwa wanasumbuliwa na Mtendaji huyo.
DC Lijualikali alisema haiwezekani kiongozi mwenye ushawishi kuachiwa atambe kwenye kauli hiyo ambayo imepeleka taharuki kubwa kwa wananchi na Mtendaji huo ambaye kwa sasa maisha yake yako hatarini.
Aman na utulivu ni jambo la msingi sana kuamua vitu kwa njia ya ubabe ni sawa na kuvuta fegi sheliNa ashughulikiwe barabara akitibitika na uovu huo....