Ligi Kuu ya Vodacom 2013/2014

Niweke mambo sawa tu kwamba mimi ni shabiki wa Azam FC.
Ni shabiki wa Man City vile vile. mwisho wa msimu mkiwa mnatoa pongezi msinisahau.
 
Kikosi cha Simba ni hiki: Dhaira chollo babaubaya kaze owino mkude redondo homoud mombeki tambwe chanongo.
Pembeni atakuwa Abuu, Miraji Adam, adeyun, Zahoro Pazi, Sino, Marcel, messi, neymar, n dogo m1 katoka abajalo, ndemla, edo, shevishenko, kipalamoto, Mkoko, gallas, Hassan Khatib, wengine mtanikumbusha
 
Niweke mambo sawa tu kwamba mimi ni shabiki wa Azam FC.
Ni shabiki wa Man City vile vile. mwisho wa msimu mkiwa mnatoa pongezi msinisahau.

Kwanza, karibu sana Mkuu na asante kwa kujitambulisha mapeema. Pili, sisi tuko fair ikitokea unastahili pongezi , tutakupatia, zipokee lakini pia unapostahili 'madongo' yapokee pia tena kwa shukrani. Asante sana.
 
Kamanda kwa jinsi Simba mlivyokuwa na njaa mwaka huu nategemea kuwaona mkishuka daraja. Siunajua kuwa Kabouru ndiye amekuwa akiwasaidia angalau kwa kununua mechi ndipo mnashinda sasa ameshaachia ngazi na anaisupport Ashanti Utd kwahiyo mwaka huu ni mwaka wa mateso kwenu.

Kwa kikosi tulichosajili Yanga sioni timu hata moja ya kutusimamisha. Ninatarajia ushindani kutoka kwa Azam(wateja wetu hawa), Coastal Union na Ruvu Shooting lakini timu nyengine zilizobaki tutazishikisha adabu tu kiroho safi.

Tumefukuza vibaraka wake wote na tukasajiri wachezaji wa timu siyo wa kiongozi ndiyo maana hakuna mchezaji hata mmoja aliesajiriwa na mtu safari hii...Majembe yameingia jana unatarifa hizo halafu natamani nikuone umevaa uzi wa CCM...
 
Mashabiki wote mliohamia AZAM kutokea SIMBA mwaka huu kwenu ni MAJANGA tu.
huku mitaa ya twiga na jangwani ikiwa raha.
 
Mkuu Mphamvu nimechukizwa sana na Simba kutumika kisiasa.

Kwa hiyo, nitakuwa kwenye mgomo wa mwaka mmoja kutoiunga mkono Simba kwa njia yoyote ile ikiwa ni pamoja na kutoichangia hata senti moja yangu kwa kununua tiketi za mechi, jezi zao na kutopoteza muda wangu kuitetea kwenye hili jukwaa.

Hii pia itakuwa ni mwendelezo wa https://www.jamiiforums.com/sports/403020-kwa-nini-mimi-ni-mshabiki-wa-manchester-united.html

Nakuunga mkono kwa kuisusia Simba, hizi ndizo harakati zenyewe. Lakini kushabikia Manchester no, hawa watu wanaendelea kututumia kwa kila namna, kuna maana gani kutochangia timu zetu halafu unachangia biashara za wazungu. Ndio, Manchester ni kampuni na inaingiza siku wewe unapokaa bandani na kupaza sauti kuishabikia...
 
mkuu kwa kikosi chako cha madogo, msimu huu hauhitaji kombe nini? naona unataka kugombea nafas ya 4 na kina kagera/mtibwa

Wale madogo ni wazuri sana, tatizo hawapewi nafasi, kuna washambuliaji nao ni Marcel Kaheza, Zahoro Pazi, Rashid Ismail, Ramadhani Kipalamoto na Edward Christopher hawa wakiingia kwenye sebule hawakukosi; Kuna mawinga nao Frank Sekule, Ramadhani Singano, Ibrahim Twaha na Haruna Chanongo, hawa wanakimbia na chaki na wanapiga cross za kufa mtu; kuna viungo wa dimba la juu nao ni Abdalah Seseme, William Lucian ni wataalamu wa penetration pass, kuna viungo wa dimba la chini nao ni Jonas Mkude na Said Ndemla, hawa ni hatari kwa kupandisha timu na kuwalinda mabeki na kuna huyu Said Ndemla ni mtaalamu wa mipira iliyokufa, tukipata mpira wa adhabu karibu na eneo la 18 hilo ni goli kwa asilimia 90 akipewa huyu dogo kupiga.
 
mwaka huu yanga ambaye amezoea kununua itakuwa ngumu sana..

Wengine nani kawakataza kununua? Siku hizi nyie hamnunui kwa sababu Friends of Nyau hawapo? Yanga inanunua wachezaji si zaidi ya hapo. Nyie mnauza wachezaji na kununua marefa. ndio tofauti ya timu hizi kwa sasa.
 
Nakuunga mkono kwa kuisusia Simba, hizi ndizo harakati zenyewe. Lakini kushabikia Manchester no, hawa watu wanaendelea kututumia kwa kila namna, kuna maana gani kutochangia timu zetu halafu unachangia biashara za wazungu. Ndio, Manchester ni kampuni na inaingiza siku wewe unapokaa bandani na kupaza sauti kuishabikia...

Value for money. Ninapotumia my hard fought money nataka maximum benefit from the product and services I buy.

Heri nitumiwe na Man Utd kuliko kutumika na Simba inayotumika kisiasa. Siku hizi people pay to watch the best.
 
Ligi ya mwaka huu naisubiri kwa hamu sana...

Sababu kubwa ni imani niliyonayo juu ya timu nyinginezo ukiacha wababe Yanga na Simba...

Timu kama Coastal Union "Wagosi wa Kaya" wamefanya usajili mzuri mno, na historia inaonesha hawa jamaa wakiwa wazuri basi ligi huwa ya ushindani sana...
Mkuu sii vibaya niki kurekebisha hapo WABABE, m-babe pekee ni Azam, hao wengine ni wakongwe.
 
Msimu huu Azam asipochukua ubingwa napumzika kushabikia soka la bongo.
 
Mashabiki wote mliohamia AZAM kutokea SIMBA mwaka huu kwenu ni MAJANGA tu.
huku mitaa ya twiga na jangwani ikiwa raha.

Je, namimi nilie hama yanga na kuamia Azam hayata nikuta hayo majanga? "Yanga ni kama sinema ya kihindi"
 
Back
Top Bottom