Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,029
- 1,646
Tamko la LHRC kuhusu hali ya Mgomo wa Umeme nchini la February 19, 2024 limeainisha hoja zifuatazo
Hoja 5 za LHRC kuhusu Mgawo wa Umeme Nchini
1. Serikali imekuwa inatoa ahadi hewa kuwa tatizo la Umeme litaisha toka kipindi cha Mradi wa gesi 2012 hadi leo 2024
2. Kukatika kwa Umeme kunaathiri Haki za Kikatiba ikiwemo
-Ibara ya 22 na 23 (Haki ya Kufanya kazi na kujipatia Ujira)
-Ibara ya 14 (Haki ya Uhai kwa Kupata Huduma Bora za Afya)
-Ibara ya 18 (Haki ya Kupokea na kutoa taarifa)
3. Tatizo linajirudia licha ya Vyanzo mbalimbali vya Uzalishaji ikiwemo Gesi asilia inayozalishwa Mtwara na Lindi (Songo songo, Mnazibay, Msimbati na Madima)
4. Mbali na Changamoto Watanzania wanazopitia kutokana na Mgawo wa Umeme hakuna anayewajibishwa
5. Bunge limeshindwa kusimamia kuhakikisha Serikali inatimiza ahadi ya kupatikana kwa Umeme Machi 2024, badala yake limeongeza muda hadi Juni 2024
Pamoja na hoja hizo wametoa mapendekezo yafuatayo ikiwemo Serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana ndani ya muda mfupi
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetakiwa kupanga ratiba ya matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kuzingatia sayansi ya mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kutoa taarifa zisizo na Mkanganyiko wa Wananchi kuhusu Mgawo wa Umeme
Pia Serikali imetakiwa kuongeza uwekezaji katika vyanzo vya uzalishaji wa nishati ya umeme isiathirika kirahisi na mabadiliko ya hali ya hewa ili kuongeza upatikanaji endelevu wa umeme