Leteni Maswali ya Kiafya Niwasaidie

Ebwana waungwana na mimi naona ni bora niulize swali langu kabisa.

Waheshimiwa Ma MD, mimi nina tatizo la mba usoni tuu, na utokea only kwenye mikunjo ya pua na kwenye masharafa. Nimekwenda kuonana na madoctor wengi sana wa skin huku ng'ambo lakini wengi wameshindwa kuutambua.

Mba huu ninao tangu nina miaka 12 na sasa ni mtu mzima, lakini huwa natumia cream ambayo huuondoa then nikiacha kutumia tuu unarudi. Wakati nipo Tanzania nilikuwa natumia gentrisone lakini ikawa inanifanya nionekane kama najichuba. So, miaka kama 8 iliyopita niliwa pita UK nikakuta dawa moja inaitwa demovate oitment. Hii ikawa hainichubui lakini mba unapotea na naitumia kama once a week.

Lakini naogopa kuendelea kutumia hizi cream naweza kujipa kansa, baadhi ta ma physician hapa US waliniambia ni bora niendelee kutumia mpaka certain age then utapotea wenyewe, i don't believe that.

Nimewai kunywa dawa za kumeza kama crotimazole lakini still upo pale pale.

swala la muhimu Jee mba wa usoni unaweza kusababishwa na mba wa kichwani? kwani nikiacha nyewele kidogo tuu ndio huu wa usoni uchachamaa. Na mba wangu sio kama ule wa kuonyesha mabaka, wangu hujionyesha kama mabaka meupe nisipopaka mafuata.

Thanks, Nadhani maelezo yatakuwa yamesaidia.
 
mkuu, kuna kinundu kimeota chini juu ya shingo eneo la chini ya medula olongata. Hakiumi wala nini,wengine wananishauri nikitoe lakini naogopa madaktari wetu wa bongo wasije wakakata nerves. je kunatiba yoyote ya kukifanya ki-subsidy? naomba ushauri wako. By the way avatar yako inatia ukakamavu!
 
SPIDER MAN
Swali lako ni gumu sana kulijibu lakini niseme tu kwamba majungu,Umbea na mitizamo hasi vinaathiriwa na mambo mengi sana kama ifuatavyo:
1.Watu wanaokuzunguka-Kama watu wanaokuzunguka kila siku ni watua ambao umbea au majungu kwa ni hali ya kawaida wanaweza kuku infect na wewe kuwa mtu wa majungu au umbea
2.Uelewa duni wa Mambo kwa mfano kama wewe fani yako ni siasa halafu ukaja kuongelea mambo ya afya ambayo huna utaalamu nayo siku zote habari zako zitakuwa ni za kusikia watu wengine walivyosema na wewe ukaja ukaziropoka kwa wengine pasipokujua ni sahihi au la.
3.Masilahi Binafsi- kwa mfano kama wewe ni mla rushwa ni rahisi san kutetea hoja za wala rushwa na kuponda wale wanaopinga rushwa kwa kujaribu kulinda heshima ya territory yenu ya wala rushwa.
4.Hallucinations-ni tatizo la kisaikolojia ambalo wewe unaona mambo vile ambavyo wengi wanaona hayako hivyo na lazima utakuwa na Negative thinking.Hallucination yenyewe haitoshi kumweka mtu katika category yoyote na disease ila ukiwa na hallucinations na tabia nyingine kama woga,wasiwasi,mashaka n.k unaweza ukawekwa kwa watu wenye Depression
5.Stress za kimaisha,kimahusiano n.k
6.Mazingira uliyokulia,Malezi uliyolelewa,Hali yako ya kiuchumi.,Uwezo duni wa kuchambua na kuelewa Mambo n.k vyote vinasababisha mtu awe na tabia hizo za umbea.
CHA KUFANYA
.Ni kumuelimisha zaidi muhusika
.Kumpa Support kifikra
.Kumshauri apunguze Stress n.k
Mchumiajuani nimeridhishwa na majibu ya swali hili je waweza nitumia PM yako tuwasilaiane?
 
Doctor unafanya kazi nzuri, endeleza libeneke. Ushauri wangu.

1. Lainisha lugha ili wagonjwa waelewe kwa ufasaha zaidi.

2. Usitoe prescription kama ulivyofanya kwa yule aliyedhani kuwa ana arthritis, prescription bila kumuona mgonjwa haifai. Hivyo basi ni vyema iwapo wagonjwa unaodhani wanahitaji prescriptions ukawashauri wamuone daktari kwa vipmo na ushauri zaidi.
 
Mchumia Juani,

Mimi naomba unitumie taarifa zote ulizonazo (kwa email yangu - nimeituma kwako kutumia PM) kuhusu hili tatizo (ambalo wataalam wanasema si ugonjwa) la diabetes mellitus (Onset Adult Diabetes Type 2).

je, tatizo hili linaanzaje, linadhibitiwa namna gani, na madhara yake ni yapi?

Asante.

./Mwana wa Haki
 
Mchumia Juani, Heshima yako mkuu,

Nashukuru sana kwa moyo wako na elimu yako fasaha unayotupa katika dimba hili, Mungu akuzidishe mwana,

Sasa mimi napenda kujua Meningitis ni nini? Pili dalili zake hasa ni zipi, na mtu anawezaje kujitambua au kuhisi kwamba anakila dalili ya ugonjwa huu na afanye nini kama HATUA ZA AWALI? Na tatu je unatibika? Na ni kwa njia gani (Yaani dawa zake zinakuwaje). Na unaweza kuongezea mengine ambayo sijapata bahati ya kuyauliza kuhusiana na ugonjwa huu.

Natanguliza Shukrani zangu.
 
Mchumia Juani,
tafadhari naomba ushauri wenu.
A.Kuhusu Fungus za sehemu za siri:
Zinatibiwa vipi au na dawa gani? Nimefanya yafuatayo mpaka sasap:
1. Kunyoa muda wote
2. Kukausha vizuri kwa taulo baada ya kuoga
3. nimetumia gentriderm ya kupaka.
Nimeona kuwa nikitumia gentriderm zinapona lakini baada kama ya wiki zinarudi.

B.Mabaka:
Je, kuna dawa ya mabaka ya usoni, mgongoni, kifuani na sehemu nyingine za mwili?

C.Mba:
Dawa ya mba please.

NB: kwa kila moja ya dawa utajazo hapo juu niambie kama mtoto anaweza kutumia, kama hawezi ... ni umri gani unashauriwa?

Je, kwa magonjwa hayo kuna dawa za mitishamba pia, ni zipi, zinatumikaje na dosage yake ikoje.
 
Nina wasiwasi na wewe, kuna mtu hapa amuliza NINI KINASABABISHA KIUNGULIA, mwingine kaulizia link ya ORAL SEX na CANCER, nadhani ungeanzia hapo kutoa majibu, au sio MGANGA WETU?????
 
Mchumia Juani,
Asante SANA kwa msaada wako. Jamani hivi kweli wa TZ tutaendelea kwa mtindo huu na ushabiki wa hivi?Baada ya kuitumia nafasi hii adimu watu mnaanza na kujadili avatar?*?
Mimi naomba kuuliza hivi Asali ina tatizo lolote kwa mtu mwenye kisukari?Sukari nyingi.
Hongera na achana na watu wenye muda wa kupoteza.
Katabazi
 
Napenda kuwa julisha wana JF kuwa nakaribisheni maswali mafupi mafupi yanayohusu tatizo lolote la kiafya.Maswali yote yatajibiwa mara moja kwa wiki iwe ni tatizo ulilonalo wewe binafsi au ndugu,jirani,rafiki au mtu yeyote unayemfahamu,Kumbuka yawe mafupi ili watu wengi zaidi wapate nafasi ya kushauriwa na mimi.Nitakupa ushauri kadri ninavyoweza.Usiwe na wasiwasi niko ktk profession hii

tatizo langu ni hiyo avatar yako. inanipa picha za marehemu na hisia za majinamizi. unaonaje ukiweka nyingine ambayo inaendana na kile unachoongea
 
Hii yawezekana ikawa habari njema.
Tatizo langu: Ni kwa muda mrefu sana sasa (karibu miaka 10 sasa) nimekuwa nikisumbuliwa na kichwa. Kichwa kinagonga (sio muda wote, bali occasionally). Siwezi kumaliza wiki mbili au siku kumi bila kuwangwa na kichwa. Kinauma hadi nakosa raha. Mbaya zaidi mie ni mwanafunzi nipo University of Agriculture-Sokoine. The more I read the more it disturbs me. Ninatumia miwani, lakini naona kama hainisaidii sana.
What should I do...Please help
 
Napenda kuwa julisha wana JF kuwa nakaribisheni maswali mafupi mafupi yanayohusu tatizo lolote la kiafya.Maswali yote yatajibiwa mara moja kwa wiki iwe ni tatizo ulilonalo wewe binafsi au ndugu,jirani,rafiki au mtu yeyote unayemfahamu,Kumbuka yawe mafupi ili watu wengi zaidi wapate nafasi ya kushauriwa na mimi.Nitakupa ushauri kadri ninavyoweza.Usiwe na wasiwasi niko ktk profession hii

Nimekutana na mshikajaji kimwili condom ikapasuka, ila katika tendo lenyewe mimi nilimkalia kwa juu nikajisugua kwenye uume wake kama mara tano akanikojolea. Tatizo sio mimba ni ukimwi maana imepita kama miezi mi nne toka tujuane. Je ukimwi upo kwenye shahawa au michubuano!
 
Dear Doctor,
Je tatizo la kutojisikia hamu ya kufanya mapenzi mara kwa mara kwa wanawake husababishwa na nn? Je kuna dawa yoyote ambayo itamsaidia mwanamke kuwa na hamu ya sex?
 
Dear Doctor,
Je tatizo la kutojisikia hamu ya kufanya mapenzi mara kwa mara kwa wanawake husababishwa na nn? Je kuna dawa yoyote ambayo itamsaidia mwanamke kuwa na hamu ya sex?

Usipojisikia hamu si ndio powa... sex sio muhimu...




jus kiddin. lol
 
Nimekutana na mshikajaji kimwili condom ikapasuka, ila katika tendo lenyewe mimi nilimkalia kwa juu nikajisugua kwenye uume wake kama mara tano akanikojolea. Tatizo sio mimba ni ukimwi maana imepita kama miezi mi nne toka tujuane. Je ukimwi upo kwenye shahawa au michubuano!

pole dada angu,kwani ndio hivyo tena ajari kazi,alafu sio ukimwi,ungeuuliza "je HIV virus wapo kwenye mbegu za kiume au kwenye damu?kama michubuko ilikuwepo na jamaa alikuwa na hao virus basi kunauwezekano mkubwa ukawa umewapata pia.Waweza fanya ngono na mtu aliye na ngoma nawe ukawa salama tu iwapo kama akutakuwepo na michubuko,ila mara nyingi michubuko uwepo wakati wa hilo tendo ingawa si rahisi kuona na ata kuhisi hiyo michubuko.

ushahuri;
ni vizuri uwende pima ngoma ili uwe huru zaidi maana hivi sasa ni lazima utakuwa umetingwa na mawazo mengi saana
 
Dear Doctor,
Je tatizo la kutojisikia hamu ya kufanya mapenzi mara kwa mara kwa wanawake husababishwa na nn? Je kuna dawa yoyote ambayo itamsaidia mwanamke kuwa na hamu ya sex?

unamaana ipi kati ya hizi mbili
(1)wanafanya mapenzi ila hawana hamu ya kurudia tendo baada ya first half
(2)wanafanya kwa nadra sana

jibu lako lipo baada ya kunipa ufafanuzi hapo juu
 
Dear Doctor,
Je tatizo la kutojisikia hamu ya kufanya mapenzi mara kwa mara kwa wanawake husababishwa na nn? Je kuna dawa yoyote ambayo itamsaidia mwanamke kuwa na hamu ya sex?

utakuwa 'hujafanywa' vizuri mpaka ukapata ule utamu wenyewe ule. ile raha yenyewe ukiipata utakuwa unajisikia hamu kila ukikumbukia na utakuwa na hamu kubwa. dawa yake ndiyo inabidi uonane na ma-technician, ni-PM for appropriate referral if interested.
 
unamaana ipi kati ya hizi mbili
(1)wanafanya mapenzi ila hawana hamu ya kurudia tendo baada ya first half
(2)wanafanya kwa nadra sana

jibu lako lipo baada ya kunipa ufafanuzi hapo juu
wanafanya kwa nadra sana, kama kwa mwaka mara 3, hamu inakuwa haipo hadi uguswe guswe hivi ndio inakuja.
 
Back
Top Bottom