Jifunze haya kabla ya kuolewa

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Kuingia Kwenye ndoa ni ndoto ya matamanio ya mwanamke ambayo huanza kujijenga tangu akiwa msichana mdogo sana.

Na ndoa ndiyo hubadili maisha na mwenendo wa matukio yote yaliyotokea nyuma yawe mabaya au mazuri ndani ya Siku moja.

Hivyo ni wazi kuwa mwanamke anapaswa kujiandaa kikamilifu kabla ya kuingia kwenye ndoa ili kuamua ni maisha gani ataishi na mwenza wake.

"Ndoa hubadili kila kitu" aliwahi kusema mshauri wa maisha ya ndoa kutoka nchini Marekani, Sarah E Stewart.

Anasema unapoolewa unaacha kufikiria kuhusu "mimi" unaenda kufikiria kuhusu "sisi".

Anamaliza kwa kusema lengo sio kujipoteza wewe mwenyewe bali ni kufanya maisha ya ndoa yawe na mantiki ya umoja na kufanya ndoa iwe na muda mrefu zaidi.

Kwa kuzingatia hayo ni vizuri mwanamke kuzingatia na kujifunza baadhi ya mambo akiwa peke yake kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Awali ya yote ni kujifunza kwa waliotangulia, mwanamke achukue muda wake kuangalia ndoa za wanawake wengine waliotangulia kisha agundue uimara na udhaifu wa ndoa hizo hasa kwa kuangalia tabia za mwanamke mwenzake.

Kufanya hivyo kutamsaidia kujifunza yaliyomazuri na kuachana na yasiyofaa, jambo ambalo kutamsaidia yeye pindi atakapoingia kwenye ndoa.

Amuelewe kwa kina mwenza wake, inashauriwa kuwa kabla ya ndoa mwanamke achukue muda kujijua mwenendo wa mwenza wake ili kumuimarisha namna ya kumkabili na Kutatua changamoto zitakazojitokeza.

Anapaswa kujua wazi kuwa hata ndoa zenye furaha ndani yake zina matukio mengi ambayo hayajulikani lakini wahusika hujitahidi kuyamaliza kwa ukimya.

Migogoro, Mabishano, hasira, utofauti wa mawazo na ubabe pia ni matukio yaliyomo kwenye ndoa hivyo mwanamke anapaswa kuwa makini katika hilo.

Kiufupi mwanamke hatakiwi kuolewa na mwanaume ambaye atakuwa mtoa lawama kwa kila tatizo linalotokea.

Endeleza kipaji chako na vitu uvipendavyo kabla ya ndoa, Kama vile kuonyesha wazi kipaji chako kwa mwenza wako Kama ususi, kucheza, Mpira, ufumaji, mapishi, uandishi na kadhalika ili kumfahamisha yeye ajue ataishi na mtu wa aina gani na ajiandae.

Pia endeleza vitu uvipendavyo kwa uwazi kwa mfano kama unapenda kuogogelea, kusafiri na Kadhalika kwani kufanya hivyo kutakupa uhuru wa kuendelea navyo hata ukiwa ndani ya ndoa pasipo kutiliwa wasiwasi.

Jiandae kupata majukumu mapya kama vile kupika mara kwa mara, kufua na kufanya usafi wa vyombo na nyumba.

Anzisha ushirikiano imara wa kumsaidia mwenza wako, mshirikishe mawazo yako mfano mipango ya maisha, ndoto yako pia shiriki kwenye mipango yake na msaidie kadri ya uwezo wako kwani kufanya hivyo kutajenga umoja wenu na ndoa itakayokuwa imara.

Acha kutangaza mambo yanayohusu wewe na mchumba wako kwa watu wengine ikiwemo mipango yenu, kufanya hivyo kutakuepusha na hila za marafiki na watu wengine ambao hawapendi uhusiano wenu udumu.

Anza kupunguza baadhi ya marafiki hususani wa jinsia tofauti ili kuondoa mazoea yanayoweza kuathiri uhusiano wako na ndoa yako.

Mchakato huu wa kupunguza mazoea na marafiki ufanyike taratibu ili usigundulike kirahisi anza kwa kupunguza mawasiliano kidogo kidogo.

Punguza kuutumikia mwili, anza kuifikiria ndoa yako kama vile kupunguza mahaitaji ya kununua nguo, urembo na mapambo badala yake wekeza kwenye mipango ya Kiuchumi wakati wa ndoa.

Anza kusevu pesa kwa ajili ya kukusaidia matumizi mbalimbali kwenye ndoa yako ikiwezekana upate hata mtaji mdogo wa biashara.

Pia jifunze matumizi mazuri ya fedha kwa kuwa na nidhamu ya matumizi ili kuepuka kuwa mfuja mali kwenye ndoa.

Wekeza kwenye Vitendo zaidi kuliko Maneno na punguza kuwa tegemezi kwa kila jambo.

Jifunze lugha ya upendo, jiandae kumheshimu mume wako na uwe mtu wa kusamehe.

Peter Mwaihola
 
Back
Top Bottom