To yeye
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 28,514
- 66,503
Kama umelelewa na ndugu, watu baki, au na mama pekee au baba pekee kutokana na kufiwa na mama, au baba ama wazazi wote. Tuwakumbuke na kuwaombea waendelee kulala mahali pema peponi. Nasi tutafuata japo hatujui kama tutakutana njia moja. Tuendelee kumwomba Mungu atupe mwisho mwema.
Nimejikuta siko sawa kwa muda baada ya kumkumbuka marehemu baba aliyekufa nikiwa na miaka mitatu. Kumbukumbu niliyobaki nayo ni kuambiwa na mama kwamba baba alikuwa ananipenda sana😭😭😭.
Mliojaaliwa kulelewa na wazazi wote wawili hongereni na msiache kuwapenda wazazi wenu, wahudumieni msichoke. Hivyo unavyobania kuwapa wazazi katu hutozikwa navyo, watachezea na kutapanya wengine.
Mungu ambariki mama yangu, aendelee kujaaliwa afya njema, amepambana sana mpaka nimefikia hapa.
Poleni sana wahanga, duniani tunapita wote pambaneni na maisha mpaka tone la mwisho la jasho na damu👊.
Andika R.I.P kwa mzazi aliyekwisha tangulia mbele za haki, kuna member atakupa pole kwa kureply comment yako, utajisikia vyema.🙏🙏🙏
Mungu awabariki sana 🙏