Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,932
- 31,178
Heshima sana wanajamvi,
Leo muda wa saa saba na nusu mchana nimekutana na waziri wa fedha Bi Saada Mkuya Salum hapa mjini Arusha.Najua wengi mtakata kwakuwa mnamwona kwenye luninga zetu akibwabwaja huko Idodomya katika lile jumba lililoja kila aina ya vituko.
Ni hivi wakati najiandaa kupata chakula cha mchana ghafla wanaingia vijana wanne wa TRA wakiongozana na askari polisi mwenye v mbili nje ya ofisi yangu kuna CCCTV nawaona askari wengine wawili wenye silaha wakijiweka tayari kwa lolote.Nawapokea bila ajizi nawauliza kulikoni kijana mmoja ananiwahi kwa kuniomba Z report nampatia anaikagua kama dakika 5 ananirejeshea baada ya kuirekodi katika daftari lake na kuondoka ?.
Nabaki nikijiuliza maswali mawili matatu hivi Z report siku hizi inakaguliwa na bunduki ?.Kuna mfanyabiashara aliyesajili VRN atakayekaidi kutoa Z report ili iweje ?.Nadhani matumizi ya askari wetu yafaa yaangaliwe upya.Wakati bado najiuliza maswali mengi naikumbuka hotuba ya waziri wa fedha wakati akiijibu michango ya waheshimiwa wabunge.
Nawasilisha.