Watu wanapenda kweli deadline
Na sisi tusio watumishi wa Serikali,hatustahili kupata hivyo vitambulisho?Wana JF, leo ni siku ya mwisho kwa watumishi wa serikali na taasisi zake kurudisha fomu za kuomba vitambulisho vya uraia, leo maofisa wengi wa serikali wako katika misururu mirefu ya kurudisha fomu hizo.
Si ndo hapo,nashangaa au watumishi wa serikali wapo dar tu,maana kila dar dar,utafikiri dar ndo tanzania pekee,nchi kubwaa hii jamaani,na idadi ya watu waliopo ni hata theluthi haifikiMbona mikoani hatujapewa hizo fomu, au ni kwa ajili ya watumishi wanaoishi DAR tu!?
Watu wanapenda kweli deadline
Da ebwana ni kweli kabisa watu hupenda deadline,mwenye ninafanya mambo mengi nje ya deadline.Niko mbioni kubadili tabia.
Nyie subirini kwanza, mpaka wapate wenye nchi na nyie ndo mtapataNa sisi tusio watumishi wa Serikali,hatustahili kupata hivyo vitambulisho?
wewe unajisemea tuu ungejua watumishi wenyewe tunavyotaabika kupata cheti cha kuzaliwa ungetulia tu. Mtumishi amezaliwa miaka ya 50 na ushee kabla ya uhuru na alizaliwa kwa mkunga wa jadi kusikokuwa na hati ya kizazi.
Hata hviyo mtumishi huyu ana PASI YA KUSAFIRIA KAMA RAIA WA TANZANIA lakini anaambiwa atoe elfu 20 apewe cheti cha kuzaliwa ili apate National ID.
Yaani hata sielewi hii PASI iliyotolewa na JAMHURI YA MUUNGANO WA TZ inasaidia nini ikiwa haitambuliki kama utambulisho wa MTZ.haitoshi kumpa mtu national ID? Hizi elfu 20 za cheti cha kuzaliwa ni za nini?
Ahaa anyway WATZ tumezoea kuburuzwa na huwa tunakubali tuu bila kuhoji.
Dar ndo Tanzania, sehemu zingine ziko masaburini mwa TZ.