Leo katika Historia : Hii ndiyo siri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Nyankore

Senior Member
Jun 24, 2014
131
68
Eid Mubarak!

Baada ya kusherehekea siku kuu ya Eid el Fitri salama kwa waliojaliwa kuwa salama na kutangulia ahera kwa waliojaliwa kutangulia, ikiwa kwa njia yoyote ile ilimradi wametangulia kama wale waliotangulizwa na basi la MOROBEST. Hii imenipelekea kukumbuka watoto waliokufa huko Tabora kwenye ukumbi wa NSSF.

Lakini pia imenikumbusha makala iliyoandikwa na M. M. Mwanakijiji niliyoisoma na kuielewa kisha kuihifadhi kwenye kitunda kumbukumbu changu. Nawaletea kama ilivyo......... karibuni.

KAMA wewe ni mwanachama au umewahi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi, usiendelee kusoma makala hii. Unaweza ukajikuta unashikilia “Roho Mkononi.” Makala hii imewalenga wale wote ambao hawajui siri kubwa ya CCM, siri ambayo leo nitaifunua. Kwa vile wana CCM wenyewe wanaijua siri hii, hivyo kitendo changu cha kuiweka hadharani leo ni kama vile mtu kutoboa siri ya sanaa ya mazingaombwe na kuvunja mwiko wa usiri unaotawala fani hiyo.
Hivyo, kwa wale wana CCM mtajitendea hisani kubwa kama mtaacha kuendelea kusoma makala hii kwa sababu kuendelea kuisoma kunaweza kukusababishia chuki, hasira, kero, n.k. dhidi ya mwandishi. Ni onyo hilo.

Chama Cha Mapinduzi kinataka wananchi wajue mambo mengi sana. Kinataka wajue kuwa ni chama safi, ni chama ambacho kinapigana na ufisadi, na ndicho ambacho kimefungua milango ya “maendeleo” nchini. Kinawapenda wananchi “wafumbue macho” na kuona mafanikio ya aina mbalimbali ambayo yametokea nchini chini ya utawala wa serikali yake.
Mara nyingi viongozi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa asiyeona maendeleo ambayo yametokana na utawala wa CCM, basi huyo si mkweli kwani mtu yeyote anaweza kuona maendeleo hayo na kuyahusisha na utawala wa Chama Cha Mapinduzi. Haya yote serikali ya CCM inataka ujue.

Hata hivyo, kuna mambo ambayo CCM haitaki wananchi wajue kwani ni kama siri ya familia ambayo haitakiwi kutoka “nje” mitaani. Ni kama vitu vinavyofanywa “Nyuma ya Mapazia.” Ni jambo la siri kubwa ambalo endapo Watanzania watalijua, kwa hakika linaweza kusababisha matatizo makubwa kwa Chama Cha Mapinduzi.

Jambo hili CCM inajitahidi kila kukicha kulificha kama mtu afichaye hazina aliyoipata kwa taabu. Hivyo, juhudi zozote za kutoa siri hii ambayo CCM haitaki itoke na kupokelewa, zitakumbana na upinzani mkali, kejeli, vitisho, dharau na hata uadui wa wazi. Hiki wanachokificha ndiyo siri kubwa ya familia ya CCM, siri ambayo leo tutaiweka wazi ili wananchi wajue nini kinaendelea.

Chama Cha Mapinduzi hakitaki wananchi wajue kuwa ni kutokana na uongozi wake, sera, utendaji, na mwelekeo wake ndiyo sababu ya kuwa na migongano tunayoishuhudia leo hii kitaifa.

Ni kutokana na utawala wa CCM, ndiyo maana hadi leo hii Jiji la Dar es Salaam limeshindwa kuweka mfumo mzuri wa maji taka ambao ungeondoa kabisa tatizo la mafuriko katika barabara zetu na kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuendelea kupendeza, siyo kwa kwa kuwa na majengo marefu tu yenye rangi nzuri lakini likiwa na mazingira mazuri na ya kuvutia hata wakati wa mvua! Kukosekana kwa miundombinu mizuri ya maji taka karibu miaka 50 ya utawala wa CCM ni matokeo ya chama hicho na serikali yake. Hili hawataki watu wajue.

Chama Cha Mapinduzi hakitaki wananchi wajue kuwa tatizo la utoaji mikopo na upatikanaji elimu ya juu nchini ni matokeo ya sera, na mwelekeo wa serikali iliyoundwa na chama hicho.

Leo hii tunavyozungumza, yawezekana utakuwa umeshasikia kuwa baadhi ya wanafunzi wamepiga kambi katika ofisi ya bodi ya mikopo wakikata rufaa kupinga walivyoenguliwa kwenye mikopo licha ya kuwa na sifa.

Badala yake watoto wa vigogo ambao hawakupaswa kupata mikopo hiyo, ndiyo waliofanikiwa kupata na kuwaacha watoto wa masikini wakiendelea kutaabika.

Matatizo ya elimu ya juu leo hii nchini hayakuletwa kama zinavyoletwa “Salamu toka Kuzimu.” Matatizo haya hayakutumwa na “Malaika wa Shetani,” bali ni matatizo ambayo yametokana na uongozi wa kisiasa wa Chama tawala Cha Mapinduzi. Kwa muda mrefu sasa sisi wengine tumepigia kelele suala la bodi ya mikopo, na jinsi gani bodi hiyo imeoza na ina kila harufu ya ufisadi. Tulipopiga kelele baadhi ya watu walituona tuna “Roho ya Paka.” Walituona kama watu ambao tunajaribu kutafuta sifa au kujaribu kudhalilisha watu fulanifulani.

Hata hivyo, miaka miwili baadaye ukweli unazidi kudhihirika kuwa serikali ya CCM imetelekeza elimu ya juu na badala yake imeiacha idode kwa kufuata sera ambazo hazifanyi kazi, za kibabe na ambazo msingi wake ni ubaguzi wa hali ya maisha ya watu.

Mara nyingi msemo wa viongozi wa serikali ya CCM ni kuwa leo hii Tanzania hatuwezi kutoa elimu ya juu bure. Kuna baadhi ya watu wanataka watu waamini hivyo. Ukweli ni kwamba, bado Tanzania tungekuwa na viongozi wazuri, wenye maono ya mbali; na wenye ujasiri wa maamuzi, tungeweza kabisa kutoa elimu ya juu kwa kila kijana wa Kitanzania.

Tatizo la elimu ya juu nchini siyo suala la uwezo hata kidogo bali ni suala la uamuzi.
Juni mwaka huu, Chuo Kikuu cha Dodoma kilifungwa, wanafunzi walitimuliwa na serikali ikajisifu kwa kukaza uzi uleule. Hata hivyo walichokifanya kilijulikana, nacho ni kuwa serikali ya Chama cha Mapinduzi haina nia ya kutatua matatizo ya elimu ya juu. Nimebahatika kuona ripoti iliyotathmini matatizo ya taasisi za elimu ya juu ambayo ilikuwa imekusudia kutafuta chanzo cha migomo mbalimbali ambayo imekuwa ikijirudia rudia.

Mara nyingi migomo hii imewafanya wanafunzi wa vyuo vyetu vya elimu ya juu wajisikie kama vile wamo “Mikononi mwa Nunda.”
Ripoti hiyo ambayo unaweza kuisoma kwenye mwanakijiji.com inaeleza kwa undani kabisa hali ilivyo kwenye vyuo vyetu vikuu na kutoa mapendekezo ya hatua gani zichukuliwe kukabiliana na matatizo mbalimbali. Hata hivyo kama ilivyokuwa ripoti nyingine zinazotolewa na serikali ya CCM, ilibakia kuwa ni ripoti tu ambayo haijafanyiwa kazi inavyostahili. Hii iripoti ilikabidhiwa kwa waziri tarehe 1 Juni, 2004. Leo hii miaka minane baadaye imefichwa kabatini na serikali ya CCM inaendelea kutumia mabavu ya kunyamazisha sauti za wanafunzi.
Kitu ambacho serikali hii haitaki watu wajue ni kuwa haina uwezo, nia, au ujasiri wa kukabiliana na matatizo ya elimu ya juu nchini. Ni rahisi zaidi kwa viongozi wa serikali kutumia nguvu ya polisi na kukamata watu usiku na kuwapeleka mahakamani kwa mbwembwe kuliko kutokaa chini na kukabiliana na matatizo ya wanafunzi.

Leo hii tunaishi kama tuko kwenye “Dimbwi la Damu” ya ufisadi. Ukiangalia kwa harakaharaka unaweza kufurahia kusikia watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA, wamefikishwa mahakamani. Kuna watu ambao wanatarajia wananchi watoe pongezi au kuonesha kuridhika na viini macho hivyo. Ukweli ni kuwa serikali ya CCM haijaamua kushughulikia matatizo ya benki kuu na ufisadi uliokithiri pale na matokeo yake wamechagua “ka akaunti” ka EPA kuwa kama geresha ya utawala wa sheria.

Serikali hiyohiyo inajua kabisa ni mambo mangapi ya kifisadi yametokea benki kuu na ambayo hata kuanza kuyachunguza hasa haijaanza. Suala la Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Meremeta, Minara Miwili ya Benki Kuu, ni mfano tu wa matatizo ambayo gharama yake ni mara nyingi ya ‘tujisenti’ tulichotwa benki kuu. Hili serikali ya CCM haitaki wananchi wajue.

Chama Cha Mapinduzi na serikali yake kimeshindwa kuonyesha uongozi wa msingi katika kuleta matumaini kwa wananchi hasa kwa kusimamia utawala wa sheria. Leo hii sheria zetu zinafanywa zionekane kuwa ni za upendeleo kwa watu wachache, huku watu wengine wakijifanya kuwa ni miungu watu.

Mara kadhaa mwaka huu, Jeshi letu la Polisi ambalo liko chini ya serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi, limeendelea na unyanyasaji kwa wananchi kwa kukamata watu kinyume na sheria na kuwaweka kizuizini. Nakumbuka jinsi yule mlemavu alivyoswekwa lupango kwa kosa la kutaka kufuatilia ahadi ya rais wake.

Ina maana kuwa katika utawala wa serikali hii ya CCM bado wananchi wanaishi kwa hisani ya watawala kwani watawala kwa kutumia vyombo vyao vya dola, wamejishawishi kuamini kuwa wanaweza kufanya lolote lile, kwa mtu yeyote yule na jaribio lolote lile la kuwahoji litachukuliwa kama ni “kupanda chuki, kuleta uchochezi na kutishia amani!”

Ndugu zangu, serikali ya CCM, ndiyo chanzo cha migomo hiyo kwani ni wao pekee wenye uwezo wa kutafuta suluhisho la kweli. Hivi ni kwanini hadi watu watishie mgomo ndiyo uhakiki wa madai ya walimu unafanywa tena kwa kasi ya ajabu? Ni kwanini hadi watu watishie migomo ndio serikali inaingilia Shirika la Reli?

Je, wakati umefika sasa kwa watumishi wa ATCL nao kugoma ili serikali iingilie kati? Je, wakati umefika kwa wananchi wa Tabora kuanza kuandamana labda serikali itakumbuka kuna watoto 19 waliokufa kizembe kwenye jengo la NSSF?

Wakati umefika tusizungushane na kuhadaiana; kama mafanikio yaliyopo leo Tanzania ni matokeo ya sera nzuri na uongozi mzuri wa CCM basi matatizo yaliyopo nayo ni lazima wawe tayari kuyakubali kuwa yametokana na sera na uongozi wao mbaya. Haiwezekani kocha apewe sifa wakati timu imeshinda lakini wakati timu ikifungwa tuanze kutafuta wachawi!

Chama Cha Mapinduzi ndicho kinahusiana moja kwa moja na utendaji kazi wa taasisi za serikali. Taasisi hizi ni zile ambazo unaweza kuziona hata “Dar es Salaam usiku,” zote zinahusiana moja kwa moja na chama tawala.

Hata hivyo, swali kubwa ambalo sisi sote tunakabiliwa nalo ni kuwa, kama kweli tunataka kuikabili CCM kama ilivyo na kuweza kuisababisha ibadilike, yawezekana tukarudi na akili zetu, lakini je, “Tutarudi na roho zetu”?

Kama itakuwa hivyo, nina uhakika Watanzania wote siku moja watatambua ni kwa kiasi gani Chama Cha Mapinduzi kimekwaza kasi ya mafanikio na maendeleo ya taifa letu. Na siku hiyo ambapo Watanzania watakaoweza kuibadili CCM kwa chama kingine kuweza kushika hatamu za uongozi wa taifa, hapo ndipo kwa hakika sisi sote tutafurahia “Zawadi ya Ushindi.” Ushindi ambao wengi wetu tunauongojea na kuufanyia kazi; ushindi ambao kwa hakika utakuwa ni ushindi mnono tena mtamu.
Hii ndiyo siri; siri ambayo Chama Cha Mapinduzi hakitaki wananchi wajue kuwa matatizo yanayotokea sasa ambayo tukiyaorodhesha yatajaza juzuu, ni matokeo ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi. Wananchi watambue kuwa wakati wowote viongozi wa CCM wanajaribu kukana kuwa CCM haijamtuma mtu kufanya ufisadi; wanajaribu kuruka kitu ambacho hakiwezekaniki.

Ni rahisi kwa mama kumkana mtoto wake kuliko kwa CCM kukana ufisadi nchini. Ni mpaka watakapokubali kuwa wao ni sehemu ya tatizo, hapo ndipo chama cha Mwalimu kitakapoanza kweli kujisafisha kutoka ndani. Kwa sasa hivi, hawataki kujiangalia kuwa yawezekana tunachokiona huku nje ni dalili tu ya kile kilichomo ndani.
 
Tanzania itapata maendeleo makubwa mno endepo watanzania watabadilisha serikali ili sera za uendeshaji nchi ibadilike.So solution simple ni kubadili serikali."Maendeleo ni kubadilisha."
 
huwezi kumkana mama yako mzazi ambaye amekuzaa na kukuleeni.ccm ndio nguzo mama ya watanzania wote.acha irrelevance fallacy zako mleta mada.umekaa nyuma ya keyboard kutukana ccm ambayo ndio tunu ya taifa
 
Nimesoma hapa nimekasirika kupita kiasi!! sitaki kutukana lakini itoshe tu kukuambia kuwa: CCM haijawahi kunizaa wala kuwa NGUZO mama yangu wala sina tunu za CCM ambazo ni Ufisadi, Ujangili na wizi!! samahani sana!!
 
KIJANA HUJITAMBUI TU,ccm ndio msingi wa tunu ya amani yetu mpaka sasa,utawala bora wa kidemokrasia wa uhuru wa maoni,ccm imekuwa nguzo mama kwako toka umezaliwa imekupa elimu toka chini mpaka chuo kama umesoma.leo vijana sampuli yako chadema na vyama vya upinzani vimewarubuni na kuwaharibu kwa elimu ya sumu dhidi ya ccm mama yenu.
 
Tanzania itapata maendeleo makubwa mno endepo watanzania watabadilisha serikali ili sera za uendeshaji nchi ibadilike.So solution simple ni kubadili serikali."Maendeleo ni kubadilisha."

Rais anaweza kutoka chama chochote kile ila Rais bora atatoka chama cha mapinduzi.
 
Nimesoma hapa nimekasirika kupita kiasi!! sitaki kutukana lakini itoshe tu kukuambia kuwa: CCM haijawahi kunizaa wala kuwa NGUZO mama yangu wala sina tunu za CCM ambazo ni Ufisadi, Ujangili na wizi!! samahani sana!!
mkuu pole kwa mawazo makali ya kuchoma moyo wako lakini haya ndiyo maisha ccm ni jana leo na hata kesho.
 
huwezi kumkana mama yako mzazi ambaye amekuzaa na kukuleeni.ccm ndio nguzo mama ya watanzania wote.acha irrelevance fallacy zako mleta mada.umekaa nyuma ya keyboard kutukana ccm ambayo ndio tunu ya taifa

Hukuona vigezo na masharti pale mwanzo ktk kusoma hii mada??
Haya, pokea buku 7 yako kajipumzishe na ile nusu pale kwenye corner
 
KIJANA HUJITAMBUI TU,ccm ndio msingi wa tunu ya amani yetu mpaka sasa,utawala bora wa kidemokrasia wa uhuru wa maoni,ccm imekuwa nguzo mama kwako toka umezaliwa imekupa elimu toka chini mpaka chuo kama umesoma.leo vijana sampuli yako chadema na vyama vya upinzani vimewarubuni na kuwaharibu kwa elimu ya sumu dhidi ya ccm mama yenu.

Vipi kuhusu tunu ya uadilifu na uwazi.
 
huwezi kumkana mama yako mzazi ambaye amekuzaa na kukuleeni.ccm ndio nguzo mama ya watanzania wote.acha irrelevance fallacy zako mleta mada.umekaa nyuma ya keyboard kutukana ccm ambayo ndio tunu ya taifa

Labda kwenu peke yenu sii kwa watanzania wanaojielewa
 
huwezi kumkana mama yako mzazi ambaye amekuzaa na kukuleeni.ccm ndio nguzo mama ya watanzania wote.acha irrelevance fallacy zako mleta mada.umekaa nyuma ya keyboard kutukana ccm ambayo ndio tunu ya taifa
Kuna mambo mengine unayopaswa kukaa na familia yako na kuwakaririsha kama hili kuwa CCM ni mama yao!! na sio kuja kutukaririsha wengine. samahani sana.
 
Kuna mambo mengine unayopaswa kukaa na familia yako na kuwakaririsha kama hili kuwa CCM ni mama yao!! na sio kuja kutukaririsha wengine. samahani sana.

kijana jenga hoja hakuna mahali nimesema uongo hapo.ccm imekuwa kimbilio la wanyonge na maskini kwa sasa,ccm imekuma mama kwa watoto wetu walio vyuo vikuu kwa kuwapatia mikopo ya kusoma,ccm imejenga shule za wazazi kupeleka vijana wao mashuleni kupata elimu.ccm mama ambaye huwezi kumkana utakuwa labda na laana ya ukoo wako
 
KIJANA HUJITAMBUI TU,ccm ndio msingi wa tunu ya amani yetu mpaka sasa,utawala bora wa kidemokrasia wa uhuru wa maoni,ccm imekuwa nguzo mama kwako toka umezaliwa imekupa elimu toka chini mpaka chuo kama umesoma.leo vijana sampuli yako chadema na vyama vya upinzani vimewarubuni na kuwaharibu kwa elimu ya sumu dhidi ya ccm mama yenu.

Kwa mtu mwenye akili timamu anaweza akajilazimisha ili akuelewe ingawala kidogo kama utatofautisha kati ya CCM chini ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete na ile CCM ya Mwl J.K. Nyerere. Tatizo lako wewe Mkuu mmaranguoriginal ni kuwa umetangaliza ubnafisi, ndiyo maana inabidi ukitukuze hicho chama tawala chini ya hao waheshimiwa. Ni kwa sababu wewe ni kati ya wachache ambao mmepata vitu bure chini ya chama tawala hasa mianya ya wizi nk. Ni nyie mnamiliki mali za watanzania as if wewe ndiye muumba wa mali hizo, ni nyie ambao hamtumii hata akiri ya darasani kama hamna ya kuzaliwa nayo mnagawa mali za watanzania bure kwa wachina, ni nyie ambao kwenu mawazo ya kujenga misingi ya innovation ktk jamii ni kama ndoto, ni nyie ambao mnaendeleza utamaduni wa kupewa bure bila kuangalia athari zake, ni nyie ambao mnawafanya watanzania waonekane watu wasio wa maana kwa jamii zingine ulimenguni, ni nyie ambao mnatuma viongozi nchi za nje wanajibehave kama viongozi kutoka banana republic nk. Chama tawala chini ya mwl Nyerere ilikuwa ni nguzo na zawadi toka kwa Mungu, lakini chama tawala chini ya hao viongozi wako waheshimiwa (Mwinyi, Mkapa, Kikwete) ni msamiati wa USANII na si zaidi ya hapo. Jitambue.
 
Vijana mnaotumika kuikashifu CCM mnakosea sana. Ni sawa na mtu kumkana mzazi wake. CCM ndio dira ya Mtanzania.
 
nimependa neno lako la mwisho JITAMBUE.mmaranguoriginal najitambua sana ndio maana nipo ccm,haya madai unayotoa dhidi yangu ni uongo uliopitiliza mimi ni mwanifu kwa mali za watanzania na ccm imekuwa mwaminifu pia,suala la kada mmoja kuwa fisadi lisijumlishwe ni la chama kizima,wewe ndio unakuwa bias na kukimbia kivuli chako ccm
 
kijana jenga hoja hakuna mahali nimesema uongo hapo.ccm imekuwa kimbilio la wanyonge na maskini kwa sasa,ccm imekuma mama kwa watoto wetu walio vyuo vikuu kwa kuwapatia mikopo ya kusoma,ccm imejenga shule za wazazi kupeleka vijana wao mashuleni kupata elimu.ccm mama ambaye huwezi kumkana utakuwa labda na laana ya ukoo wako
Sasa unataka hoja gani! ccm kuwa kimbilio la maskini wakati ukiangalia kuna bonde kubwa kati ya maskini na matajiri wakati huu hapa nchini. Mijini badala ya kuwawezesha wakina mama na wamachinga, serekali ya ccm ndiyo inayowakodolea macho Mgambo wa majiji kama Dar,Arusha,Mbeya ,Mwanza na kungineko wakiwanyang'anya mali zao bila kuwasaidia chechote!! CCM inasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu kupata mikopo!Looo!! Tuhuma kuwa mikopo inatolewa kwa upendeleo wewe hujazipata?Rejea alichokiandika mtoa mada kuhusu Bodi ya mikopo kuwa na harufu ya kifisadi, hili mbona ccm inashindwa kulishungulikia? au wanaopata mkopo ni watoto wa vigogo wa chama?CCM imejenga shule!! Shule bila walimu, maabara na hata hao walimu wachache, bado maslahi yao ni duni!! ni mtoto yupi wa kigogo wa chama hicho anayesoma huko? Au nyie mnataka kujenga shule na kisha muagizie watoto wa wengine wakasome huko ili hali wa kwenu muwapeleke kwingine? Sasa kama ccm ni mama wa aina hii!!!! Naweza kumfananisha na mama anayezaa mtoto na kumtelekeza sokoni.Kumbe mwenye laana ya ukoo ni asiyeona kasoro hizi zote na nyingine nyingi za chama hicho.
 
lete ushahidi hapa kwamba kuna ufa mkubwa kati ya maskini na tajiri ndani ya ccm.jifunze kuwa objective,leo wewe na mtoa mada mnatoa tuhumu kuhusu bodi ya mikopo ya vyuo vikuu,NIKUULIZE SWALI KATIKA MIAKA HII MIWILI UMESHUHUDIA MIGOMO YA WANACHUO KWAMBA WAMEKOSA MIKOPO YA KUSOMA.TAJA CHUO CHOCHOTE KILICHOFANYA MGOMO. CCM IMEFANYA MAAJABU MAKUBWA SANA NDIO NGUZO MAMA
 
Back
Top Bottom