Lema: Posho si dhambi, dhambi ni posho inapokosa utu

Inawezekana tunajadili vitu viwili tofauti. Mimi ninachojadili ni yaliyosemwa na Lema kwenye kikao cha wabunge (Kama Zitto alivyoainisha, unless you say Zitto is a liar) kumlaani Zitto kwa kuonekana kikwazo cha wao kujiongezea posho, si hizi blabla alizoandika humu unazoita falsafa.

Yapi? hayo yaliyoko juu ndiyo ya kwake hayounayomrisha wewe hatuyatambui....
 
Ndugu yangu we mgumu kuelewa: Wabunge wachape kazi kila kitu kipatikane kama huduma za afya bora, mikopo ya elimu hata bure kusoma, barabara nk ndo wabunge wadai posho. Ndiyo hoja ya Lema na kama kila kitu kiko sawa wananchi wameshughulikiwa posho zao basi hata wakipewa bentley sawa si wamewajibika. Nimetolea mfano mishahara ya watumishi singapore na ilikuwa maskini kama sisi tu

Bora niwe mgumu kuelewa kuliko kukubali kuwa uwajibikaji wa wabunge uwe ni kwa motive ya kuongezewa posho!!!!!
 
Mkuu, Msimamo wa lema uko wazi juu ya Posho, rudi kasome hapo juu hizo zingine ni porojo tu.
Ame-spin baada ya watu kumshtukia na kuanza kuhoji ukamanda wake. Muulize Mnyika kama unataka kujua msimamo wa Lema kwenye issue ya kuongezewa posho.
 
Kwa hili habebeki asilani mkuu kama hoja ni uwajibikaji basi ingeweza kusimama hata bila ya mbeleko hiyo ya posho!!!!!!!

Hivi mkuu uwajibikaji unapimwa kwa kuongezewa posho au welfare improvement??!!!!!!

Hivi alikiwa na sababu ya kiweka nemo posho kama hoja ya msingi ilikuwa na uwajibikaji???!!!!

Hivi wewe ungepewa hii thread kabla haijatundikwa hapa ili utoe ushauri una uhakika tungeisoma kama ilivyo hapa????!!!!

Ningeisoma kama ilivyo. Tatizo watanzania hatufatilii pande zingine mambo yanakwendaje. Lakini kama umefuatilia nchi nyingi zilizoendelea na maskini hoja ya posho sio ishu kubwa kama tunavyofikiri.

Mfano uganda wagombea wa urais walilalamika incumbent president kutumia usafiri wa umma M7 aliwapa shangingi kila mtu na ulinzi kampeni nzima na ndo utaratibu mpaka leo.

Marekani shughuli za kichama, chama anachotoka rais wanachangia gharama.

Lakini kwa mfano wa Singapore ilitosha kuweka mjadala huu wa posho chini. Nchi kama inakuwa tajiri kwa maana ikiendelea tukafika hatua ambayo haachwi mtu nyuma hakuna shida ya mishahara mikubwa na posho kama kweli walitufikisha nchi ya ahadi
 
Mantiki iko wapi hapo. Hana hoja ya msingi hapa zaidi ya mwendelezo wa ulaghai kisiasa.

He can't even talk the talk let alone walk the walk.

Kama anaona ongezeko la mishahara na posho za wabunge ni immoral akilinganisha na hali ya kimaisha kwa Watanzania wengi, basi alitakiwa kuacha kwanza kuzipokea ili afanane na hao walalahoi na kuanza kuisukuma serikali ili iweze kuongeza kipato kwa watumishi wote ili baadaye na yeye kama mbunge kipato chao kiongezwe.

Unachofanya kwa sasa ni utapeli wa kisiasa ambapo anataka kuilaumu serikali wakati akiendelea kupokea ongezeko la mishahara na posho wakati ana nafasi ya kuikataa.

Ningemwelewa kama angezikataa kwanza hizi posho na marupurupu na kuanza kuwapigania wananchi anaodai kila siku anawapigania.

Whatever you look at it, this guy is political con and profiteer.

Huna hoja unabwabwaja tu kama malaya, Ukigomea inaend wapi unajua mashariti ya bungeni kuwa ukisha saini tu kuwa umehudhulia posho inaingizwa kwenye akaunti yako, hoja ya chadema ilikuwa ni posho zote za kipuuzi zifutwe na siyo kwenye bunge peke yake lakini kwa wapuuzi kama wewe mkakomalia kuwa ni bungeni tu...
 
Kwa hili habebeki asilani mkuu kama hoja ni uwajibikaji basi ingeweza kusimama hata bila ya mbeleko hiyo ya posho!!!!!!!

Hivi mkuu uwajibikaji unapimwa kwa kuongezewa posho au welfare improvement??!!!!!!

Hivi alikiwa na sababu ya kiweka nemo posho kama hoja ya msingi ilikuwa na uwajibikaji???!!!!

Hivi wewe ungepewa hii thread kabla haijatundikwa hapa ili utoe ushauri una uhakika tungeisoma kama ilivyo hapa????!!!!
We bado hujajua chanzo cha mgogoro huu, alikua anachangia mjadala wa ndani(breafing) kabla ya bunge, kuna watu waliozua hoja ya posho, anatoa maoni yake ndio mbeleko ilipoanzia. Sasa hoja ya msingi ni posho ziende na usawa ndio hoja ya Rais wa AR.

Nadhani maumivu ya wengi ni kuona mwenzio aningiza mfukoni wakati wewe huna. hoja syo posho ni tatizo maana sawa zikafutwa posho zote alafu msiongezewe mishahara hayo mapambano faida yake iko wapi? TUACHE kupayuka tu posho mbaya mbaya mbaya! hiv posho ni nini? siyo rushwa hii!! maana tumekomalia wabunge na posho zifutwe, lakini mwalimu akisimamia mtihani wa mock shuleni si analipwa posho pia na siku hiyo hatafanya kazi yeyote nyingine. tufute zote eeh?. hoja siyo posho hoja ni tofauti za kipato tuu. Tatizo watanzania mmeaminishwa posho dhambi na siasa za upepo. ukweli ni masilahi yetu watumishi yawe mazuri na masoko ya kilimo yawe bora vipato vipande. Ila sasa kama serikali imeshidwa isichaguwe wakulipwa zaidi na wengine kidogo ndio hoja ya lema hii.
 
Nitapiga kura pale tu ambapo nitakuwa nagombea uongozi,vinginevyo viongozi wetu wengi ni wachumia tumbo.
 
Mantiki iko wapi hapo. Hana hoja ya msingi hapa zaidi ya mwendelezo wa ulaghai kisiasa.

He can't even talk the talk let alone walk the walk.

Kama anaona ongezeko la mishahara na posho za wabunge ni immoral akilinganisha na hali ya kimaisha kwa Watanzania wengi, basi alitakiwa kuacha kwanza kuzipokea ili afanane na hao walalahoi na kuanza kuisukuma serikali ili iweze kuongeza kipato kwa watumishi wote ili baadaye na yeye kama mbunge kipato chao kiongezwe.

Unachofanya kwa sasa ni utapeli wa kisiasa ambapo anataka kuilaumu serikali wakati akiendelea kupokea ongezeko la mishahara na posho wakati ana nafasi ya kuikataa.

Ningemwelewa kama angezikataa kwanza hizi posho na marupurupu na kuanza kuwapigania wananchi anaodai kila siku anawapigania.

Whatever you look at it, this guy is political con and profiteer.

Maelezo yake sijaona sehemu akilaumu serikali zaidi ya kuwapa changamoto wabunge wenzake. Ni kweli uwajibikaji wao unaendana na malipo wanayopokea? Bila shaka hapana lakini wapo wanaowajibika na wanastahili posho ya sasa.

Wanasiasa wote uonekana walaghai mpaka pale wanapopewa nafasi za kimamlaka. Bahati mbaya wabunge hawana mamlaka yote yote kulingana na katiba ya nchi. Isome katiba wao wapiga porojo tu
 
Bora niwe mgumu kuelewa kuliko kukubali kuwa uwajibikaji wa wabunge uwe ni kwa motive ya kuongezewa posho!!!!!
Mkuu Olesaidimu, mimi nashindwa kutambua. Nilifikiri uwajibikaji wa wabunge ungepimwa kutokana na ustawi wa wananchi wanaowakilishwa. Mkuu ninayemheshimu sana kama Aweda anahoji kuwa hata wakipunguziwa posho mfugaji wa Mbulu atafaidikaje? Hivi hela itakayookolewa ikinunua dawa ya kuoshea mifugo kwenye josho Mbulu huyo mfugaji wa Mbulu takuwa hajanufaika?

Hivi kweli hawa wanaotaka kuongezewa mishahara na posho watakuwa na moral authority ya kuhoji kwa nini Kikwete au Pinda wanajilipa mishahara mikubwa wakati tunawagharamia mahitaji yao yote? CDM tusipojifunza na kujenga tabia ya kukosoana pale tunapokosea, tunaelekea pabaya.
 
Ningeisoma kama ilivyo. Tatizo watanzania hatufatilii pande zingine mambo yanakwendaje. Lakini kama umefuatilia nchi nyingi zilizoendelea na maskini hoja ya posho sio ishu kubwa kama tunavyofikiri.

Mfano uganda wagombea wa urais walilalamika incumbent president kutumia usafiri wa umma M7 aliwapa shangingi kila mtu na ulinzi kampeni nzima na ndo utaratibu mpaka leo.

Marekani shughuli za kichama, chama anachotoka rais wanachangia gharama.

Lakini kwa mfano wa Singapore ilitosha kuweka mjadala huu wa posho chini. Nchi kama inakuwa tajiri kwa maana ikiendelea tukafika hatua ambayo haachwi mtu nyuma hakuna shida ya mishahara mikubwa na posho kama kweli walitufikisha nchi ya ahadi

Kwanza fact halafu ndio mifano,kujaza mifano ya nchi nyingine ambazo mode of production, GDP, Income per Capita, IMR, MMR na life expectancy wametuacha mbali kabisa ,achilia mbali technological advancement!!!!!!!

Sasa angeweka hoja hizi kwanza mpaka matunda yaonekane kwa wananchi at large then ongezeko la kipato ni spontaneous,lakini unapoyaweka haya kama matawi na shina likiwa ni posho hapo mimi sikuelewi na tukubaliane kutofautiana katika hili!!!!!!

Umeongelea investing on human resource kama njia moja wapo ya kutokea kwenye malipo mazuri. Yeye katika hoja yake hilo limekaa vipi in relation to allowances!!!!!

Ndio maana nasema clarification na derivation zenu zinawafanya baadhi ya viongozi kutokuwa makini na hoja zao!!!!!!

Iacheni hoja ijisimamie na kama kuna nyongeza aweke yeye mwenyewe huo ndio uwajibikaji sio kusema halafu atuachie sisi kama hivi tukipasuana vichwa!!!!!!
 
Ame-spin baada ya watu kumshtukia na kuanza kuhoji ukamanda wake. Muulize Mnyika kama unataka kujua msimamo wa Lema kwenye issue ya kuongezewa posho.
Unajua huu waraka ni wa lini au umekurupuka tu mkuu....
 
Usisome nusu ya article na kutaka kuelewa yale unayotaka kuyaelewa wewe na mengine ambayo yatasababisha mshindwe kumlaumu Lema myatie kapuni. Hebu soma hapa chini ili uelewe article yote na siyo uelewa wa robo robo au nusu nusu tu. Dhahabu ya Watanzania tangu 1999 mpaka 2011 imeingiza $12 billion na nchi imeambulia $496 million tu, kama kungekuwa na kodi ya 30% basi nchi ingeambulia $4 billion zaidi na hivyo kuwezesha kupandisha mishahara ya wafantakazi Serikalini kwa kiwango cha juu kabisa na kuongeza ubora wa huduma mbali mbali nchini ikiwemo maji, usafiri, elimu, afya n.k. lakini MACCM yameshatiwa mfukoni kwa wachukuaji wenyewe mnawaita wawekezaji. Mkishawekewa mabilioni kwenye bank accounts zenu kule uswiss hamjali kabisa maisha ya Watanzania walio wengi. Muhongo alitaka kuwatoza hao wachukuaji 30% wakatishia kuondoka ikafutwa kimya kimya.

"Ni kweli gharama za Maisha zimepanda lakini hazikupanda kwa Wabunge tu pia kwa Wananchi wote wanaoishi Tanzania , Hivyo tukiacha ubinafsi tukawajibika vizuri Bungeni kulinda masilahi ya Taifa na kutetea maisha ya Wananchi wetu, bila shaka hata tukionekana tunaendesha magari ya kifahari kama Rolls Royce, Bentley, Benz , hakuna mwananchi hatakeyesema kwa nini Mbunge anaendesha gari zuri kwani kila mtu atakuwa na afadhali ya maisha ktk Nchi yetu."

BAK..umekuwaje tena ndugu?Lema ndiye anayedai WABUNGE WAONGEZEWE POSHO SASA,KWA SABABU MAISHA YAO NI MAGUMU NA MASLAHI YAO NI MADOGO.

Hayo ya kada zingine sio hoja ya dharura kwa Lema kwa sasa, hayo ni ya mwaka jaaana wakati na yeye akiiga hizo porojo za kukataa ongezeko la posho kabla jana hajafanya u-turn hadharani na kuungana na akina Shibuda kudai ongezeko hilo lipitishwe bila kuwajali hao wabunge wanaopinga(Zitto).
 
Bora niwe mgumu kuelewa kuliko kukubali kuwa uwajibikaji wa wabunge uwe ni kwa motive ya kuongezewa posho!!!!!

Hapa hakusema kwamba waongezewe posho ndo wawajibike. Anaongelea kama wanaweza kudeliver yani wakiwajibika na maendeleo yakawepo kwa kila mtu basi hata wakidai posho wataeleweka.

Vilevile nakubaliana na hoja yako kwamba posho si kigezo cha watumishi hao kuwajibika.

Nchi zilizoendelea zinazotaka kuhamasisha sekta binafsi wafanyakazi wa umma hawazidi mishahara ya sekta binafsi ( Marekani hata rais anazidiwa na mkurugenzi wa kampuni) na nyingine Mwanasiasa hawezi kumzidi mtendaji wa kitaaluma, mfano ufaransa meneja wa kampuni ya umeme ya umma mshahara wake ni mara 4 ya mshahara wa rais
 
“POSHO SI DHAMBI , DHAMBI NI POSHO INAPOKOSA UTU” – LEMA

Nimetafakari sana niliposoma kwenye magazeti kuwa sisi wabunge tumeongezewa posho bila hata sisi kufahamu jambo hilo .
Na kila mtu ametoa maoni mbali mbali juu ya jambo hili , ni kweli ni msimamo wa chama chetu (Chadema) kupinga posho mbali mbali zisizokuwa na tija na tulikubaliana hivyo kwenye vikao vya Chama Chetu vya Wabunge na kupinga mfumo wa posho uliopo kwa sasa ni msingi sahihi wa Chama kuonyesha hisia na ubadhilifu mkubwa unaotokana na ulipwaji mbaya wa posho kama ambavyo imejitokeza mara nyingi na hata hivi karibuni tumeshuhudia madudu mengi kwenye ripoti ya kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Jairo. Lakini suala hili haliwezi kuepukwa kabisa na Chama kinajua ila utaritibu wa ulipwaji posho kwa watumishi mbali mbali wa umma ni tatizo kubwa na kuna mapungufu mengi sana ndio maana kupinga posho haina maana tu ya kupinga kiwango cha pesa anachopokea Mbunge au mtumishi yeyote wa UMMA bali mfumo mzima wa sera ya posho ili uweze kuwa na tija na kupunguza mianya ya wizi katika mfumo huu ambao umekuwa ukitumika vibaya kuliibia Taifa.

Pengine sisi wabunge ni vyema tukatambua kwanini wananchi wanapiga kelele kuhusu posho nilishawahi kusema Bungeni wakati nachangia kwenye Wizara ya Ustawi wa Jamii kuwa mshahara wa Wabunge , posho mbali mbali za Wabunge pamoja na marupurupu mengine yanaonekana kuwa anasa pale watumishi wengine wa serikali kama Manesi ,Asikari Magereza,Polisi ,Makarani Mahakamani wanapolipwa chini ya shilingi laki mbili na nusu kwa mwezi na wakati huo huo wanasikia mwakilishi wao akipiga kelele Bungeni kuwa posho ya laki mbili kwa siku ni ndogo. Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU , Na hapa lazima kutokee ugomvi wa kimasilahi na mgogoro mkubwa kati ya mwakilishi na anaye wakilishwa.

Pengine masilahi anayopata Mbunge ni ya kawaida sana tena sana ila yanaonekana kuwa anasa pale ambapo yeye kama mwakilishi anapolipwa kiwango cha posho cha siku moja ambacho ni sawa na mshahara wa mpiga kura wake kwa siku thelasini. Mimi nafikiri namna peke ya wabunge kutetea masilahi yao bora kwanza ni kupigania masilahi ya wapiga kura wote Tanzania na tukifanya hivi kama Wabunge hakuna Mwananchi hatakayeshangaa kwanini Mbunge awe na masilahi bora kwani ubunge ni nafasi kubwa pia inayositahili heshima kubwa kwani ni uwakilishi katika jamii.

Ebu jiulize wananchi wanaposikia Wabunge wamepewa milioni tisini kununua magari na wakati huo huo serikali imenunua bajaji kuwa ndio magari ya kubeba wakinamama wajawazito yaani (Ambulance) ni wazi kabisa wabunge wataonekani ni watu katili na walioenda bungeni kwa masilahi binafsi japo kuwa ukweli unabaki kuwa Wabunge wanahitaji magari imara na mazuri. Lakini Wabunge kama watafikiri Bajaj ni sawa kuwa gari la wakinamama wajawazito na wao kuchukua milioni tisini kwa magari ya binafsi bila kupiga kelele na kukataa unyanyasaji huu kwa wakina mama na Wagojwa ,hivyo ni dhahiri kuwa ugomvi hapa katika posho na masilahi ya Wabunge utasababishwa na tofauti ya masilahi dhidi ya wale waliowachagua kuwatetea ,Hivyo namna pekee Mbunge anaweza kutetea masilahi yake bora bila kuingiliwa na na kubugudhiwa ni Mbunge kuanza kufikiria masilahi ya watu wengine ambao pia ni watumishi wa UMMA ambapo yeye ni mwakilishi wake .

Nafahamu kuwa pamoja na kupinga mfumo mzima wa utaritibu wa posho ulivyo sasa tafakari ya kweli ni kwamba masilahi ya watumishi wa UMMA bado ni madogo sana kwa hiyo Uzalendo wa kweli sio tu kupinga masilahi bora bali serikali iwajibike kikamilifu kudhibiti wizi na ufisadi unaotokana na utaritibu mbaya wa ulipwaji posho , kuongeza makusanyo katika kodi mbali mbali ,kutumia rasilimali za Nchi vizuri ili masilahi ya watu wote Nchi hii yaweze kuwa na tija kwa maisha ya Watanzania na watu wengi waweze kuishi maisha ya faraja na kutimiza malengo yao muhimu ya maisha

Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

Nitakuwa ni mtu mwenye mashaka sana kama nikiwaza kuwa masilahi duni na maisha ya kuishi chini ya kiwango ni Uzalendo , Sasa Wabunge mkitaka msipigwe mawe barabarani ,msitukanwe , msionekane ni wasaliti wa jamii aliyowachagua , Sasa huu ni wakati wakusema , Mshahara wa Polisi ,Magereza,JWTZ, Walimu, Makarani Mahakamani na hata sekta zote za Serikali na Binafsi masilahi ya mishahara yao yaongezwe kwa asilimia kama ambavyo mmjiongozea nyie kwenye posho zenu tena zinazohusu siku moja tu lakini wao wanaomba kwa mwezi lakini hawapati. Sasa pamoja na kupinga mfumo mzima wa sera ya posho kama ambavyo Mwenyekiti wetu wa Taifa alisisitiza na kuomba sera hii iangaliwe upya ili kupunguzia Taifa mzigo mkubwa na kuboresha viwango vya mishahara vya watumishi wa UMMA , ni vyema nikarudia kusema kuwa ““POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.
Ni kweli gharama za Maisha zimepanda lakini hazikupanda kwa Wabunge tu pia kwa Wananchi wote wanaoishi Tanzania , Hivyo tukiacha ubinafsi tukawajibika vizuri Bungeni kulinda masilahi ya Taifa na kutetea maisha ya Wananchi wetu, bila shaka hata tukionekana tunaendesha magari ya kifahari kama Rolls Royce, Bentley, Benz , hakuna mwananchi hatakeyesema kwa nini Mbunge anaendesha gari zuri kwani kila mtu atakuwa na afadhali ya maisha ktk Nchi yetu.
“ Baba yangu aliniambia “ Watu wengi wanaokwenda Kanisani na Misikitini huwa wanatoa sadaka ndogo kuliko pesa wanayotumia sehemu mbali mbali za anasa ndio maana Taifa lina Bar nyingi kuliko nyumba za Ibada” TAFAKARI

LEMA- MB
mimi kila siku nagombana na watu ninapowaambia kwamba Lema hoja zake zote ni za msingi na ndio ukibishana nazo utahabika. nakushukuru sana Mbunge wangu naomba namba yako ya simu ili niwasiliane na wewe nina mambo ya msingi na ninaamini wewe una carage ya kuyasema mbele ya spika
 
Katika hili siungani kabisa na lema. Lema anatakiwa kuonesha mfano kwa kuungana na wenzie wakina myika,zitto natundulissu kupinga wabunge kujiongezea posho.

Lema anatakiwa kujua wabunge kujiongezea posho ni dhambi huku wananchi hasa wafanyakazi wa umma wakiendelea kuteseka.
Hujui unapinga nini na unataka nini au unasema nini...
 
Kwanza fact halafu ndio mifano,kujaza mifano ya nchi nyingine ambazo mode of production, GDP, Income per Capita, IMR, MMR na life expectancy wametuacha mbali kabisa ,achilia mbali technological advancement!!!!!!!

Sasa angeweka hoja hizi kwanza mpaka matunda yaonekane kwa wananchi at large then ongezeko la kipato ni spontaneous,lakini unapoyaweka haya kama matawi na shina likiwa ni posho hapo mimi sikuelewi na tukubaliane kutofautiana katika hili!!!!!!

Umeongelea investing on human resource kama njia moja wapo ya kutokea kwenye malipo mazuri. Yeye katika hoja yake hilo limekaa vipi in relation to allowances!!!!!

Ndio maana nasema clarification na derivation zenu zinawafanya baadhi ya viongozi kutokuwa makini na hoja zao!!!!!!

Iacheni hoja ijisimamie na kama kuna nyongeza aweke yeye mwenyewe huo ndio uwajibikaji sio kusema halafu atuachie sisi kama hivi tukipasuana vichwa!!!!!!

Hoja zako hizi ziandike sehemu alafu soma statement yake nukta kwa nukta utaziona kwamba ameziongelea.
 
Back
Top Bottom