Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Lema kaongea kitu cha kweli.

Invasione ya Bodaboda Africa imeua sanaaa.
Imejeruhi mnoo.
Na mpaka sasa nafikiri ndo inaongoza kwa vifo na ulemavu Barani Africa.

Ispokuwa ni jinsi anavyo pitisha hoja yake.
 
Kwa nini viwe tofauti? Kwa nini wao wafanye kazi BOT, kazi za Umoja wa Mataifa na kwingineko? kama ni shida ya kazi hata watoto wa Waziri wawe na shida na kazi.

Watoto wao wanafanya kazi New York theb wanakuja kuwahadaaa wajinga nyie kwamba kaendesheni toyo na kasomeni Ualimu
Ndo maana nikakwambia ni utofauti hata wewe unaweza kuingia kweny system au kuwa na kipato kikubwa na wanao wakafika mbali...Hata marekani sio wote wanaokula keki ya taifa kuwa na akili.

Hao chadema na CCM ndo walewale hawana jipya pambania familia yako
 
Mkuu nchi ina wajinga sana, wao watotobwao wako hadi Umoja wa Matifa huko New York, tena wameajiriwa kwa Vimemo, huku watoto wa Choka mbaya wakiambiwa waende Ualimu na TOYO
Zile scholarship za kwenda kusoma like USA ,Canada France,Sweden , Amsterdam yaani zile nchi nzurinzuri Ni watt wao ndio wanaoenda
 
Ni mfano usio sahihi wala hauna mantiki hii ni duni vipato ni tofauti kila mtu na riziki yake na utaftaji wake ...Atambue kwamba hata ambao Wana vipato vya juu ni wachache sana mno .

Yeye ni mwanasiasa na wenzio wanasiasa wanajua kuanzia kupiga dili na kuiba , sio lazima kwani hapo unagusia wananchi wa hali ya chini kabisa.. wanasiasa wote sijui lema na wenzio CCM wote akili sawa wao ndo wanufaika na pesa za wananchi ...je hao bodaboda waache kazi then waende wapi?

Kuna watu wamekaa nje miaka mpaka 20 ila wanaporudi bongo wanajua Kuna tofauti ya kule na huku ...wale wenzetu wameendelea sana unaweza kutoka kule baada ya kukaa sana ukaja bongo ukapaona kama pananuka ila ukiwa na akili unalow matarajio ukirudi bongo kwamba hapawezi kuwa kama ughaibuni

.Wenzetu miaka miwili basi kila kitu anaona kinyaa ni ushamba mtupu ..
Kama nchi unadhani kuwaingiza vijana hawa wa miaka 15 hadi 30 kwenye kazi ya uboda boda itaisaidia nchi kupiga hatua
 
Sorry bro mimi nimeajiriwa nafanya kampuni ya kilimo, ni vile tu tumezoea shida na kuona ni kawaida. Ila hiyo kazi ya boda boda hapana kwakweli watu tubadili mitazamo pengine.
Kuna kuna ku adapt habits and neuropathway za umasikini unaona uko sahihi. Jamani boda risk Ni kubwa kwa maisha yake yaani Sana mno. Safety Ni ndogo.


Kuna kuzoea kupanda daladala unaona uko sahihi ama kula ugali wali viazi mahindi choma chemshwa makande uji wa mahindi ugali wa mahindi wewe unajipa comfortableness kuwa uko sawa. Ila siku ukionja utamu wa dunia utaona Kama ulikuwa gerezani.


Hivi hamjui Kuna watu wanazoea gerezani hata wakitoka wanaomba Tena kurudi.


Yaani Kuna kitu kinaitwa subconscious mind is very powerful than you combined millions times.
 
Sasa wewe unataka wafanye kazi gani?
Hapo sasa ndio tunaletwa pamoja dhidi ya ujumbe anao tupa Lema, kwamba serikali imeshindwa kurahisisha fursa zilizopo ili watu wake wafanye kazi zenye kuwahakikishia usalama wao na zenye tija.. Badala yake wao wanajinufaisha na vizazi vyao halafu nyinyi wanawaaambia eti boda boda ni maisha.
 
Lema yuko sahihi by the way, vijana wetu tunaumizwa sana na bodaboda lakini kwa nchi kama hizo za africa hasa huko Tanzania ni shida vile vile vijana wetu kutafuta kazi mbadala ambayo haijuulikani iko wapi wala utaipatje
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi.

Lema amesisitiza Kuwa Bodaboda ni Kazi isiyofaa inayouwa na kuwapa ulemavu Vijana Wengi.

Lema amenena haya kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mlale Unono!

======

"Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha bodaboda na kudai ni kazi ya heri nitaomba radhi. Bodaboda ni kazi ya mateso,imeumiza watu na kujeruhi watu wengi.Acheni kudanganywa na Serikali iliyo kosa mbinu za kuokoa maisha yenu. Umasikini sio sifa."

View attachment 2539929
Haya alitakiwa sasa akawaeleze Mh Majaliwa na Mh Mwinyi. Kuwaeleza bodaboda wenyewe ni kuwakashifu.
 
Ndo maana nikakwambia ni utofauti hata wewe unaweza kuingia kweny system au kuwa na kipato kikubwa na wanao wakafika mbali...Hata marekani sio wote wanaokula keki ya taifa kuwa na akili.

Hao chadema na CCM ndo walewale hawana jipya pambania familia yako
Unamwambia yeye apambanie maisha ila wakati anapambania anatozwa kodi halafu hiyo kodi inawanemeesha watoto wa wengine aisee hii haiko Sawa unaonaje
 
Hapo sasa ndio tunaletwa pamoja dhidi ya ujumbe anao tupa Lema, kwamba serikali imeshindwa kurahisisha fursa zilizopo ili watu wake wafanye kazi zenye kuwahakikishia usalama wao na zenye tija.. Badala yake wao wanajinufaisha na vizazi vyao halafu nyinyi wanawaaambia eti boda boda ni maisha.
Wapo bodaboda wametoboa na wengine wanalisha familia zao hivi nikuulize Kati ya bodaboda na yule cashier wa Mlimani city s yupi anaingiza hela zaidi?
 
Back
Top Bottom