Lema: Dhambi kubwa kuliko zote duniani ni dhambi ya woga

ukishakuwa muoga ni rahisi kufanya shiriki maana hilo ndilo utakaloamini kuwa suluhisho la matatizo yako kwakuwa tu umeogopa kujaribu

Kuogopa nini kuiba au kufanya uhalifu? hayo yote ni haramu na ni dhambi kwa dini zote.
 
Kuoga kuchukua haki yako uliyoitambua baada ya kuikosa kwa zaidi ya miaka 50

Haki ipi uliyoikosa? na wewe unadanganywa na wanasiasa uchwara unakubali, wao wanatafuta mchange vijisenti vyenu wao wakachote wajengee majumba mahawara zao, hukijui kisa cha Josephine? au uoga ule ndio mnaodanganywa muondoke nao?

Hakuna haki uliyonyimwa, haya tueleze ulichokikosa mpaka leo ni nini?
 
Tobaa! Kamanda kajizila, kaenda mstari wa mbele kabisa vitani. Anachana fisadi mbili live!! mwili unasisimka. No tafsida no bla bla!! Hatarii
 
Hana ilmu huyo, dhambi kubwa na isiyosameheka ni kumshirikisha Mwenyeezi Mungu.

Elimu ni zaidi ya vyeti mkuu,ila kwa mtu mjinga uamini kua makaratasi na kukariri vitu vichache kichwani ndio elimu!huu ni ugonjwa ambao Watanzania kadhaha tunao,wengi wetu hatujatambui,wala hatujui maana halisi ya elimu!baadh yetu nadhani tumefuta ujinga tu hata kama ni kwa level ya bachelor,ila kuelimika bado hatujaelimika!sasa kwa mtazamo wako wewe na Lema ni nani anaeonekana ame elimika mbele ya jamihi?Mtu mjinga ni muoaga na mwenye kutojiamini siku zote!
 
ama kweli nimeamini makahaba na watoza ushuru watawatangulia watu kuingia ktk ufalme wa mungu
 
Pitapita zangu nikaiona hii video Mh Lema akiongea na Mh Mulongo. Ndio maana Lema alimwambia umekuja hapa kama unaenda kwenye sendoff. Maana eti hajashuka hata kwenye gari kafika kaanza kubishana na lema. Huyu jamaa sijui alipewa uku wa mkoa kwa vigezo gani!!


 
Last edited by a moderator:
Vijana hawadanganyiki tena. Wewe kama hauna mke/mume, watoto, wazazi, ndugu na jamaa wanaokutegemea endelea kumsikiliza huyo Mh. Lema halafu uone hao wanaokutegemea (kama ni kweli unao) watasaidiwa na nani pindi utakapolipuliwa na bomu na hao CHADEMA.
 
Mtu mwenyewe unaitwa Sumu !! Maneno yako, na nafsi yako yamekaa kama jina lako lilivyo!!!

Endelea kumwaga sumu unasikilizwa..
 
Dhambi kubwa kuliko zote ni ushirikina na sio uwoga usipotoshe jamiii

Hiyo imeandikwa wapi?? Biblia inaeleza kuwa waoga ndio watakaoanza kuingia katika lile shimo la moto! Mwenzetu hiyo umeitoa wapi?? Au nia yako uonekane umepost kuingiza siku??
 
Hiyo imeandikwa wapi?? Biblia inaeleza kuwa waoga ndio watakaoanza kuingia katika lile shimo la moto! Mwenzetu hiyo umeitoa wapi?? Au nia yako uonekane umepost kuingiza siku??

kumbe bibilia iyo isharekebishwa mara kibao me nafata Quraan ambayo haijafutwa hata herufi tokea ishushwe feel sorry for you broo
 
mbunghe wa arusha mjini kupitia chadema godbless lema akiwahutubia wananchi wa arusha kwenye mkutano wa hadhara aliwatangazia kuwa WOGA NI DHAMBI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI...KUPIGANA VITA SIO DHAMBI...NI HERI VITA INAYOTAFUTA USAWA KULIKO AMANI...HIVYO VIJANA, WAZEE NA AKINA MAMA watumie kila walichonacho kupigana, kutokubali kuonewa, kutokuogopa kufa, wajitokeze kupigana VITA.

Je, kwa kauli hizi, lema sio mhaini? lema hajatangaza vita? lema hajahamasisha vurugu na kauli hii sio hatari sana kwa umoja wa kitaifa wa nchi yetu???
Watanzania tusikubali hadaa hizi za wanasiasa, tusikubali laghai hizi za wanasiasa, tutafakari na kutumia akili zetu ipasavyo.

Lema: Hakuna dhambi mbaya duniani kama dhambi ya Woga - YouTube
 
Back
Top Bottom