Lema ashinda rufaa dhidi ya ubunge wake!

Hawa vijana wa BAVICHA walinisababishia msongo mkali sana wa mawazo.
Nilikuwa katika mchakato wa kutafuta ushauri nasaha kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia.
Sasa nimeahirisha zoezi..moyo wangu umerejea katika hali yake ya awali.
Ole wenu vijana wa BAVICHA.Naomba nisiandike sana.
 
Ukweli siku zote hauchangamani na uongo, aibu kwa CCM lakini kwa kuwa mishipa yao ya haya ilikatika siku nyingi hawatalijutia hili.
 
Aaaaah nimeukumbuka,unaimbwa hivi:

moja mbili tatu!!! Lema karuka ruka kaleta vurugu,Lema karuka ruka kapelekwa lupango,Lema karuka ruka hakuna alichokifanya Arusha lakini Lema alipopigwa ban na mahakama barabara,maji,jiji,maendeleo Arusha vilipatikana ....

mingoi kuna mwingine naona utakufaa zaidi.......

karudi baba mmoja (ccm), toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili(ufisadi),
watoto wake wakaja ili kumtaka hali(kina nape, ritz, januar nk),
wakataka na kauli iwafae maishani(wakataka waoneshwe mbinu za wizi).

Akatamka mgonjwa ninaumwa kwelikweli (ccm imezidiwa na ufisid),
hata kama nikichanjwa haitoki homa kali(pamoja na kutajwa hadharani wezi hawaachi wizi kwan wameshakuwa sugu-arosto),
roho naona yachinjwa, kifo kinanikabili (2015 ccm kwishnei),
kama mnataka mali semeni niseme nini


.............alipokwisha kutaja fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili
(ccm imekata roho)......teh teh
 
Masalia & Co plus Washauri wao pamoja na wafadhili wao Wakanywe sumu ya panya sasa au wasage chupa wanywe. Kudos Lema, Bravo CDM.
 
HONGERA LEMA KWA KURUDI BUNGENI Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Godbless Lema amerudishiwa ubunge wake baada ya kushinda katika rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo.

Hukumu imeangalia haswa swala la "Locus Stand" ya kama "waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo". Kadiri ya pingamizi ya mawakili wa Lema Ndg. Kimomogoro na Tundu Lissu, waliofungua shitaka dhidi ya Lema hawakuwa na "Locus Stand" ya kufanya hivyo. Kwa hiyo mengine yote yanakuwa "null and void". Hukumu haikuchukua hata nusu saa aibu iliyoje hii?. Hoja moja tu tena ya kwanza kati ya hoja 18 zilizowasilishwa na upande wa rufaa kupinga hukumu hiyo mbele ya majaji Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao Nathalia Kimaro imeonesha ukomavu wa mawakili Kimomogoro na Tundu Lissu. Nachukua fursa hii kuwapongeza majaji hawa Salum Massati, Bernard Luanda na Nathalia Kimaro na mawakili Kimomogoro na Tundu Lissu kwa kuonesha ukomavu wao na kuthibitisha kuwa taaluma yao haina mashaka hata chembe. Mungu awajaalie wazidi kuwa na mafanikio makubwa na heri katika kazi zao, tunahitaji wazalendo kama hawa ili nchi iwe na ustawi na kudumisha haki.

Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Serikali inatakiwa kumchunguza kwa makini Jaji Gabriel Rwakibalira. Kwa maoni yangu nadhani huyu ni kada wa CCM na kama sivyo basi taaluma yake ni batili na butu sharti achunguzwe pia alisomea wapi kwani hawa ndiyo akina KIHIYO wanaogushi vyeti na kukalia nyadhifa muhimu huku wajuzi walio makini wakikosa nafasi kwa kuwa hawana ndugu wa kuwapachika katika nafasi hizo. Hivi karibuni kulitokea tuhuma zilizoenea kuwa baadhi ya majaji na mahakimu hawajui Kiingereza hali inayosababisha kushindwa kutoa hukumu sahihi kwa misisngi ya haki bali wanahukumu kwa utashi na matakwa yao hii ni hatari kwa taifa letu. Hakika kuna haja ya uteuzi wa Majaji kuchunguzwa upya hii ni aibu kwa Mheshimiwa Rais na washauri wake kwani huu ni mfano mmoja tu wa majaji uozo, Je, wako wangapi wa sampuli yake?

Swali la msingi la kujiuliza ni:
Je, ni raia wema wangapi wameathiriwa na hukumu butu kama hizi hizi za Jaji Gabriel Rwakibalira na wakatumikia adhabu zisizo sahihi kwa kukosa utetezi wa mawakili makini?
 
mwendo mbele; yana mwisho haya; tutafuta jinsi ya kuwafungulia mashtaka sahihi hao waliopoteza muda wa mbunge pamoja na huyo jaji wa sumbawanga kwa kesi ambayo tangu mwanzo ilionekana haina mashiko;
 
Back
Top Bottom