nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
na Grace Macha, Arusha
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ametoa ufafanuzi kuwa Gervas Mgonja si katibu wake kama ilivyodaiwa na vyombo vya habari kwani alishamuachisha kazi tangu Juni 16, mwaka huu.
Mbunge huyo alisema taarifa hiyo imetokana na mkakati wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutaka kumchafua kwa kumhusisha na ujambazi.
Mgonja anashikiliwa na polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuhusika na ujambazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Lema alisema katibu wake hivi sasa anaitwa Lucia Fransisco na alishaandika barua kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali ikiwemo jeshi la polisi kuwajulisha mabadiliko hayo.
Lema alisema kuwa taarifa za kumuachisha kazi Mgonja alizitoa miezi mitatu lakini ameshtushwa na baadhi ya vyombo vya habari kuandika kwamba huyo bado ni katibu wake.
Tanzania Daima, lilipata nakala ya barua ya Lema kwenda kwa mkuu wa polisi mkoa wa Arusha (RPC) na mkuu wa polisi wilaya ya Arusha (OCD), akiwajulisha juu ya kumsimamisha kazi Mgonja na uteuzi wa Lucia.
Sehemu ya barua ya Lema iliandikwa hivi: Kuanzia Juni 16, mwaka huu, Lucia ndiye katibu wangu na kama kutatokea mabadiliko yoyote nitawaarifu, kwa msingi huo Gervas Mgonja siyo katibu wangu tena kuanzia sasa.
Kwa mujibu wa Lema, katika siku za hivi karibuni ameanza kupata hisia kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia mbinu chafu kumhusisha na makosa ya kihalifu ili kumdhoofisha kisiasa.
Alisema baada ya kusikia taarifa za gazeti hilo alimtumia ujumbe mfupi wa simu Mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha (RPC) kusikitikia kitendo hicho.
Kamanda RPC, nakusalimia nimefuatilia magazeti asubuhi ya leo nimeona moja linasema katibu wa mbunge ahojiwa kwa ujambazi, ninatambua unayo barua kwa OCD na ngazi zote husika.
Mgonja siyo katibu wangu kwa muda mrefu sasa, kama taarifa hiyo ni ya polisi, basi nitakuwa mwenye huzuni kuwa sasa hata jeshi la polisi linafanya kazi kisiasa, hata hivyo haki na utu havijawahi kushindwa. Asante na siku njema.
Jana, gazeti moja, liliripoti kuwa katibu wa mbunge wa Arusha mjini, Gervas Mgonja, anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.
Kwa mujibu wa gazeti hilo Mgonja anatuhumiwa kuhusika na matukio kadhaa ya ujambazi mkoani Arusha na gari lake binafsi linahusishwa kuwabeba watuhumiwa wa ujambazi.
Wakati huohuo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Arusha Mjini kimesema kuwa Gervas Mgonja anayeshikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ujambazi si katibu wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Ephata Nanyaro, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa Mgonja aliachishwa kazi kwenye ofisi ya mbunge toka Juni 16, mwaka huu, hivyo taarifa zilizotolewa zikimuelezea kuwa ni katibu wa Lema zilikuwa na lengo la kukichafua chama.
Alisema ofisi zote za umma kwenye wilaya ya Arusha zimeshaandikiwa barua kujulishwa mabadiliko hayo ya uongozi katika ofisi ya Mbunge.
Tunalitaka jeshi la polisi kusimamia ukweli na haki, kamwe lisihusishe tukio la Mgonja na CHADEMA wala lisijihusishe na siasa; na tunaomba sheria ichukue mkondo wake na sisi tutatoa ushirikiano pale tutakapohitajika kufanya hivyo, alisema Nanyaro.