Le Tshentemba Pub Arusha

Njopa

Senior Member
Nov 18, 2010
192
30
Washikaji, Mie na jamaangu tumeanzisha Pub hapa Arusha Tumeiita Le Tshentemba Pub sasa tuna siku 10 toka tuanze. Hii ipo Nairobi Rd karibu na Police post na ofisi ya mtendaji kata mkabala na Manyara guest house, inatazamana na Nat Oil Petrol station. Biashara ni ya wastani tu. Tatizo langu bado tu wapya kwa hii biashara, inaonekana pia kwa vile pale awali palikuwa na Night clubs hata sasa wateja wake wanakuja zaidi usiku na leseni yetu ni mpaka saa 6 usiku na kama tukiawazuia mauzo yatashuka saana. Tunafikiria kubadilisha leseni iwe tena night club, ukizingatia uzoefu wetu ni mdogo inatupa tatizo. Wasichana wanachelewa kulala inakua ngumu hata kuchukua stock maana tunafanya kazi pia kumbe ni budi kuwahi kazini. Lakini pia hatuna chumba cha staff! Tunatafuta chumba maeneo ya karibu na pale bado hatujapata.

Kwa wazoefu naomba ushauri wenu kwa mambo yafuatayo;
1. Nifanyeje kuongeza mauzo katika mazingira haya
2. Tupafanye kuwa night club na utaratibu ukoje?
3. Tunawezaje kufunga stock kirahisi asubuhi, na ni lazaima stock ifungwe mida hiyo tu
4. Kama kuna mtu anaweza tusaidia kupata chumba cha staff maeneo hayo kwa bajeti isiyozidi Tzs 50,000.00

Shukrani 0786262635
 
nitafute nikutengenezee receipt book, invoice, kutengeneza sare za wafanyakazi wako pamoja na tshirt pia
karibu kwa huduma
 
1.angalia makosa ya mtu wa kwanza nawe jilekebishe,kuwe na show/ band za kufanya watu waje kuona tofauti na uboa ,usisahau kufanya matangazo ya kutosha,
2.usikae na wahudumu zaidi ya miezi sita (sababu ya kuwazoea wateja inafanya wateja wakose hudumu kwa wakati au ubaguzi)
3.kuwa na wahudumu amba wanapokezana kazi hii inasaidia kwenye umakini kiutendaji
4.wajali wafanya kazi wako ili kupunguza wizi nakufanya kazi kwa ufanisi
5.wape nafsi km wamepata show time ww waweke mikakati km kulipia kiasi fulani cha pesa (inavutia mabwana kuja kwenye pub yako yy anapata nawe unapata)
6.kuwa na maneja ambaye anakagua stock kila siku ww uwe unamkagua meneja kwa wiki au mwezi
7.usafi mhm sana hasa wa choon na chakula (glass ziwe na chemsiwa maji ya moto)
8.kuwa night club nifaida kwako
 
Ngoja nipitie kwanza hapo jioni leo kisha ntakuwa na la kukushauri,ila si vyema sana ukajipa umeneja wewe mwenyewe,utakuwa unawkosesha amani wafanyakazi wako hasa wahudumu na kupelekea biashara kupoa sana.
 
Usifanye mahesabu usiku ila hakikisha unalala na hela itakayokuwepo na hata kama wewe unaenda kulala hela inayokuwepo had sa sita chukua mahesabu asubuh..... Hakuna haja sana ya kubadili leseni mjini mambo ni magumashi tu sisi tunakesha na leseni hatuna na maisha yanakwenda maana zipo grocery zinakesha pia. Maisha ya mjin ni magumashi ukitaka biashara ife jidai unafata sheria

Mpare wa milimani
 
Washikaji, Mie na jamaangu tumeanzisha Pub hapa Arusha Tumeiita Le Tshentemba Pub sasa tuna siku 10 toka tuanze. Hii ipo Nairobi Rd karibu na Police post na ofisi ya mtendaji kata mkabala na Manyara guest house, inatazamana na Nat Oil Petrol station. Biashara ni ya wastani tu. Tatizo langu bado tu wapya kwa hii biashara, inaonekana pia kwa vile pale awali palikuwa na Night clubs hata sasa wateja wake wanakuja zaidi usiku na leseni yetu ni mpaka saa 6 usiku na kama tukiawazuia mauzo yatashuka saana. Tunafikiria kubadilisha leseni iwe tena night club, ukizingatia uzoefu wetu ni mdogo inatupa tatizo. Wasichana wanachelewa kulala inakua ngumu hata kuchukua stock maana tunafanya kazi pia kumbe ni budi kuwahi kazini. Lakini pia hatuna chumba cha staff! Tunatafuta chumba maeneo ya karibu na pale bado hatujapata.

Kwa wazoefu naomba ushauri wenu kwa mambo yafuatayo;
1. Nifanyeje kuongeza mauzo katika mazingira haya
2. Tupafanye kuwa night club na utaratibu ukoje?
3. Tunawezaje kufunga stock kirahisi asubuhi, na ni lazaima stock ifungwe mida hiyo tu
4. Kama kuna mtu anaweza tusaidia kupata chumba cha staff maeneo hayo kwa bajeti isiyozidi Tzs 50,000.00

Shukrani 0786262635

Kwa nini usiite Chez Njopa? Mengine washasema wenzangu.
 
Guys Nawashukuru nyote kwa Ushauri! Hakika awamu kwa awamu nitatekeleza mengi ya ushauri wenu. Ningependa kunetwork na wengine wenye biashara kama yangu niweze kujifunza zaidi! Capt Tamar ulipita? mbona hukunitafuta? ulizia Mapunda. Ladyfurahia ningependa kukutembelea nione uniform, n.k. Duly Zura pole, siwezi kuacha biashara hiyo, natafuta maisha na kupambana na umaskini, najua inakukwaza lakini tuvumiliane. J33, Wanan nawashukuru na nitafuatilia. Kwa sasa kweli bado sijaajili meneja, hii ni kutokana na ukweli kwamba jamaa yangu alishakuwa na mameneja walimuibia sana! Nilifikiri nifanye kwa muda nione trend kisha pengine nitaajiri kama nitampata mwaminifu. Kuhusu bendi za muziki ni ngumu maana eneo sio kubwa kivile. Natamani ningejenga banda zuri kubwa pale nje at least lakini nimeonywa sana watu wa Tanroad wanavunja hata kama sio jengo la kudumu. Asanteni
 
Mkuu,heshima kwako,samahani jana sikuweza kupita kutokana na sababu 2/3 rest assured nitapita japo ninywe soda,na kaushauri kidogo,kazi njema mkuu.
 
kaka Njopa tupia na tupicha tuone ulivyopendezesha mkubwa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom