Lazima tuwatathmini mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na wabunge

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
NINASIKIA eti serikali ndio kwanza imeanza kuwatathmini viongozi wake. Au kwa maneno mengine watu wa serikalini watakuwa wanatathminiana. Sasa mimi kichwa kichaka lakini mwenye akili nadhani kama sio kushinda Wazungu wote basi kushinda Wachina wote ninatoa mapendekezo haya ambayo nyie Watanzania msionambelewalanyuma mkikubali kuyazingatia mtabadili kabisa mustakabali wa linchi lenu lisilo na mbele wala nyuma.

Kwanza, lazima viongozi nilionesha hapo juu na wengine wapewe visheni, misheni, malengo na kisha wao waweke mikakati ya kufikia yaliyopangwa.

Pili, pawe na uwazi na uwajibikaji katika utendaji wao na mtu hata mmoja asithubutu kubaki ili asukumwe kuondoka. Ukiboronga au ukiwa mbabaishaji aga mapema tu na utapewa haki zako zote.

Tatu, pamoja na serikali kuachiwa kufanya tathmini yake mimi ninadhani ni muhimu kwa sisi members wa JamiiForums kuwatathmini jamaa hawa sisi wenyewe tukishirikiana na Watanzania wengine kupitia magazeti, televisheni, redio na ofkozi tovuti.

Tathmini hiyo iwe kwa kutoa alama zifuatazo:

AAA- Kiongozi ni safi na bora kabisa na anastahili kupewa dhamana kubwa zaidi, motisha na nishani ya utendaji. Ana visheni, misheni, malengo na anajua anachokifanya kwa eneo lake au nchi na watu wake. KUBWA zaidi haogopi mtu au chama anachoogopa ni wananchi kwa m maneno mengine anatumikia wananchi na sio wakubwa fulani au chama fulani.

AA- Kiongozi ni bora na anastahili kuchaguliwa tena ili mradi ajitahidi kuwa safi zaidi. Anakwaza na siasa ya chama chake. Hana fursa ya kufanya makubwa zaidi.

A- Kiongozi ni bora na anajitahidi lakini sio safi na aendelee kuchunguzwa na kutathminiwa. Katawaliwa kabisa na siasa na wanasiasa lakini akiachana navyo ni kiongozi mzuri sana.

B- Kiongozi ni mtu mwenye uwezo wa kawaida wa kawaida na mtu yeyote mwingine anaweza kushika nafasi hiyo na akafanya sawa na yeye. Yupo katika nafasi yake kwa sababu ya nguvu za chama au kisiasa.

C- Kiongozi ana uwezo chini ya kawaida. Asome, aelekezwe, ashauriwe, aadabiwe na kadhalika ili kumpa fursa ya kujaribu angalau kwa mwaka mmoja tena. Analindwa na wanasiasa na serikali kwa sababu zisizojulikana.

D- Kiongozi ni bomu, mbabaishaji, mtegaji, hana malengo na anachongojea ni mshahara tu mwisho wa mwezi. Akaripiwe, aonywe na achukuliwe hatua nyingine zinazofaa. Hata wenhyewe wanasiasa hawamtaki lakini wana lao wanalojua.

E- Kiongozi ni uozo mtupu. Hafai na hatufai. Aondolewe mara moja na awezeshwe kujiajiri mwenyewe maana nchi haina shida ya watu wa kuajiri. Kisiasa, kijamii na kiuchumi ni liability au mzigo usiobebeka.

NInaomba wakuu wa JamiiForums kutengeneza jedwali lenye majina ya Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wabunge na Wakuu wote wa vyama vya siasa ambao watafanyiwa tathmini hii kupitia mtandao huu. Tathmini hii itakuwa 'updated kila siku' huku taratibu tukishirikiana na watu kama kina Mo Ibrahim ili baadaye na sisi tuingie kwenye mchakato unaochangia kuwashawishi, kuwahamasisha na kuwasukuma wanasiasa na viongozi wetu kuacha ubabaishaji na uzembe na badala yake wawe makini na wachapa kazi ili tuondokane na umasikini tusiostahili kuwa nao katika karne hii.

Mfano:

Wabunge:
Na. Jina Jimbo Tathmini Maelezo
222. Iga Upinde Ilala C Anayo mwenyewe

Iga
 
Wazo zuri sana, lakini will never materialise in Tanzania. Nani atamchunguza mwenzake ? Kulikuwa na tume ya maadili ya viongozi wa umma, haijafanya chochote.
 
Kama tathmini ikifanyika ya mawaziri, halafu mawaziri fulani wakapata low rating, I am afraid experience has shown that the thread will be removed a' la thread ambayo ilikuwa inasuggrest majina ya viongozi mbadala ambao wanaweza kuchukua nafasi ya muungwana!! Tatizo la kuwa na mods who are partisan!!
 
Back
Top Bottom