LATRA mnamuangusha Rais Samia

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
757
842
Nitoe masikitiko yangu kwenu LATRA, mmekasimiwa majukumu na Mhe Rais wetu ya kuratibu na kusimamia usafiri wa Nchi kavu lakini hamumtendei haki kabisa Rais wetu, maana mkishatoa hivyo vibali hamna muda wa kufuatilia kama mliowapa vibali hivyo kama wanazingatia masharti ya vibali hivyo!.

Hivi mnataka Mhe Rais ndie awe anafuatilia kila kibali mlichokitoa nchi nzima wakati mpo hapo maofisini?.

Majuzi nilitembelea njia ya Gongolamboto - Chanika - Zingiziwa(Ngobedi) niliyoyaona hayavumiliki lakini pia hamuwqtendei haki wananchi na wapiga kura wa mama Samia.

Hivi inaingia akilini gari yenye kibali cha Gongolamboto - Zingiziwa (Ngobedi), itoke Gongolamboto ifike Chanika ishushe abiria na gari hiyo hiyo ipakie watu hao hao kwa nauli nyingine kwenda Zingiziwa (Ngobedi) tukasema ni haki hiyo!.

Inakuwaje hayo yanatokea LATRA, Polisi Usalama barabarani, n.k, mkiona?, hivi kweli mnania ya kumsaidia Rais wetu au mnampango wa kumhujumu achukiwe na wapiga kura wake?.

Tafadhali mamlaka husika chukueni hatua mmusaidie Rais wetu na sio kumhujumu!.
 
Back
Top Bottom