LATRA kuruhusu daladala zenye namba E na D pekee kuingia kituo cha mabasi Mwenge wanafikira nini?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Haya ni maajabu,

Wanazuia mabasi yasiyo na namba D au E kuingia lakini wameruhusu Bajaji na bodaboda kuingia..

Tena wanasema madereva na wasaidizi wao wavae sare kama za shule, suruali dark blue na shati jeupe kisa kituo kipya.

Latra sio akili zao zinawaza nini?

Kama hawana mambo ya kufanya watusaidie kuondoa bajaji ambazo sasa zimejimilikishia njia kama daladala.

Njia ya Mbezi to Makumbusho wamesimamisha kutoa leseni kwa daladala lakini wameachia bajaji zifanye hiyi route.

Ushauri wangu LATRA ifutwe, maana hakuna kazi inafanya.
 
Kuna njia nyingi sana hapa dar sasa hivi hawatoi leseni na wanakuka na kigezo cha gari liwe na namba fulani wakati kuna vibajaji vimechoka ukiviona vitatembea utadhani mlevi wa mbege.

Wananchi tunahitaji kusafiri na sio namba za magari, kjna magari yana namba E lakini ni mabovu kuliko hayo namba A.

Latra ingesema mabasi yanayo takiwa ni yale yenye seat kuanzia 40 na kuendelea tungewaelewa, tungejua wanalengo la kuounguza foleni

Tunaomba wizara husika ilitazame hili, jiji linapitia wakati mgumu sana kwenye usafiri kwa sababu ya taasisi isiyo na maoni kama latra.
 
Haya ni maajabu,

Wanazuia mabasi yasiyo na namba D au E kuingia lakini wameruhusu Bajaji na bodaboda kuingia..

Tena wanasema madereva na wasaidizi wao wavae sare kama za shule, sufuali dark blue na shati jeupe kisa kituo kipya..

Latra sio akili zao zinawaza nini?

Kama hawana mambo ya kufanya watusaidie kuongoa bajaji ambazo sasa zimejimilikishia njia kama daladala.

Njia ya mbezi to makumbusho wamesimamisha kutoa leseni kwa daladala lakini wameachia bajaji zifanye hiyi route.

Ushauri wangu latra ifutwe, maana hakuna kazi inafanya..

Mihemko kama ya watoto wa shule walionunuliwa uniform mpya za Shule baada ya viraka vya mda mrefe.
 
Wabongo huwa hawapendi vitu vizuri na huwa wanapenda shida wakati wote.

Ukitaka kujua kuwa wabongo wanapenda matatizo angalia tu vyombo vya usafiri vya uma wanajazana humo mpaka wanakanyagana na hakuna anayelalamika.

Hii nchi ngumu sana.

Ndio maana viongozi wetu wanatuchukulia poa sana, wameshatujua tulivyo.
 
Simply LATRA wanataka gari mpya ndio ziingie kituo kipya.

Same mentality waliyoitumia kwenye uniform za madereva na makondakta wao.

Kituo kipya, mabus mapya, uniform mpya.
Hicho kituo kitachakaaa na kitakua kiwa kichafu kama vingine hapa mjini.. cha ajabu bajaji chakavu zinaingia..

Pia namba za magari hazimaanishi upya wa gari.. kuna magari namba E lakini ni ya mwaka 1983
 
Wabongo huwa hawapendi vitu vizuri na huwa wanapenda shida wakati wote.

Ukitaka kujua kuwa wabongo wanapenda matatizo angalia tu vyombo vya usafiri vya uma wanajazana humo mpaka wanakanyagana na hakuna anayelalamika.

Hii nchi ngumu sana.

Ndio maana viongozi wetu wanatuchukulia poa sana, wameshatujua tulivyo.
Mkuu kuna sera ilikuwepo enzi za JK wakati wanazitoa hiace.. kwamba mabasi ya mjini yawe makubwa na ilikuwa ni kuanzia sest 40.. ili kupunguza msongamano.

Haya mambo ya latra ni utoto , hayana msaada wowote ..
 
Haya ni maajabu,

Wanazuia mabasi yasiyo na namba D au E kuingia lakini wameruhusu Bajaji na bodaboda kuingia..

Tena wanasema madereva na wasaidizi wao wavae sare kama za shule, sufuali dark blue na shati jeupe kisa kituo kipya..

Latra sio akili zao zinawaza nini?

Kama hawana mambo ya kufanya watusaidie kuongoa bajaji ambazo sasa zimejimilikishia njia kama daladala.

Njia ya mbezi to makumbusho wamesimamisha kutoa leseni kwa daladala lakini wameachia bajaji zifanye hiyi route.

Ushauri wangu latra ifutwe, maana hakuna kazi inafanya..
Kwanini una chuki na bajaji?
 
Back
Top Bottom