Laptop Za Bei Nafuu

ManiTek TV

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
410
159

Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia

Makala hii itazungumzia laptop za kisasa ambazo zina uzuri wa kutosha kwa bei nafuu katika aina ya laptop mbali mbali, tutaangalia ya bei rahisi zaidi na pia tutaangalia ya bei ya chini yenye wastani wa vipimo (specs) vizuri kiasi. Bei zote ni kwa mujibu wa soko la UK ikiwa ni pamoja na kodi zote. Katika uchambuzi wetu hatutaingiza MacBook na pia tutaingiza baadhi ya laptop za bei ghali lakini ndio ya chini katika kundi la laptop hizo.



Laptop hii ni kwa ajili ya mtu ambaye anapata intanet wakati wowote anapohitaji kutumia kompyuta yake kwa vile data, programu na karibu kila kitu huhifadhiwa kwenye mawingu (cloud). Bei ya laptop hii ni £200 ambazo ni sawa na 491,359.00 za Tanzania.


OS: Chrome OS ya Google


Prosesa: Intel Celeron 847 yenye kasi ya 1.10 GHz na 2 MB L3 Cache.


Diski: Ina ukubwa wa 320GB aina ya HDD,


RAM: 2 GB na inaweza kuongezwa mpaka 4 GB


Betri: 37 Wh 2500 mAh 14.8 V Li-Ion, haikuelezwa betri hii inadumu muda gani.
Skrini: ukubwa ni inchi 11.6
Uzito: Kilo 1.38


Hii ni kompyuta ya mtu ambaye hahitaji makuu au ndio anaanza kujifunza kutumia kompyuta. Vile vile unaweza kupata Packard Bell N60 kwa bei hiyo hiyo.



Netbook ni laptop kwa ajili ya kazi ndogo ndogo kama vile kutumia intanet, kusoma email na kazi zinazofanywa na MS Office. Pia inaweza kutumika kuhifadhia na kucheza picha, video na muziki Hii si laptop kwa ajili ya shughuli zanazohitaji nguvu kubwa ya kompyuta. Bei yake ni £179.00 sawa na Tsh 439,787.15. Skrini ina ukubwa udogo wa inchi 10.1 na diski ya ndani ina nafasi kiasi cha 320 GB. Betri yake inakisiwa kudumu masaa 3 na ina uzito wepesi wa kilo 1.02. Prosesa ni Atom N2600 ikiwa na core mbili na kasi ya 1.6 GHz. kompyuta hii pia ina webcam kwa ajili ya kuchati.




OS: Windows 7 Starter


Prosesa: Ni aina ya Intel Celeron 847 yenye kasi ya 1.1 GHz.


Diski: Ina ukubwa wa 320GB aina ya HDD


RAM: 1GB


Betri: Inakisiwa kudumu masaa 3 hadi 6, ni aina ya Li Ion ikiwa na cell tatu.


Skrini: ukubwa ni 10.1 yenye rezolushani 1024 x 600 WSVGA


Uzito: Kilo 1.02



Kwa laptop aina ya Ultrabook HP Pavilion ndio ya bei karibu na bure, Ultrabook ni laptop nyembamba zenye nguvu kiasi na mara nyingi huwa zinavutia kwa muonekano. Laptop hii ina upana wa sentimeta 2.1 ambapo inaizidi MacBook Air kwa sentimeta 0.4 tu kwa upana. Bei ya Laptop hii ni £420 sawa na TSh 1,031,875.00


OS: Windows 8


Prosesa: Intel Core i3-3217U yenye kasi ya 1.8 GHz na 3 MB L3 cache


Diski: Ina diski mbili, ukubwa ni 750 GB aina ya HDD, na 32 Gb aina ya SSD


RAM: 4 GB DDR3


Betri: 4-cell Li-Ion polymer inayodumu hadi masaa 8


Skrini: ukubwa ni inchi 14


Uzito: Kilo 1.8


Laptop hii haina sifa maalum mbali ya kuwa ni laptop ya wastani, yenye skrini iliyozoeleka zaidi ya ukubwa wa inchi 15.6, na inamudu matumizi ya kati na kati bila ya matatizo yoyote. Bei yake ni £259 sawa na TSh. 635,246.56


OS: Windows 8


Prosesa: AMD C60 yenye kasi ya 1 GHz, 1.33 GHz TurboBoost na 1 MB cache


Diski: ukubwa ni 320 GB aina ya HDD,


RAM: 2 GB DDR3 na unaweza kuongeza hadi 4GB


Betri: 4-cell Li-Ion polymer inayodumu hadi masaa 8


Skrini: ukubwa ni inchi 15.6 Sata 3 ikiwa na rmp 5400


Uzito: Kilo 1.978


Laptop hii inavutia mno kwa vile ni laptop ya rahisi mno ukilinganisha na nyingine zenye skrini mguso ukizingatia kwamba Windows 8 imetangenezwa hasa kwa matumizi ya aina ya mguso (touch). Bei yake ni £350.00 sawa na Tsh 858,459.89, laptop yenye skrini mguso inayoifuatia hii kwa urahisi inauzwa 1,052,254.18 ambayo pia ni Asus.


OS: Windows 8


Prosesa: Intel Pentium B987 yenye kasi ya 1.5 GHz na 3 MB cache


Diski: ukubwa ni 500 GB aina ya HDD Sata 3 na kasi ya 5400 rpm


RAM: 4 GB


Betri: Li-polymer 38WH yenye cells 3 inayodumu hadi masaa 5


Skrini: ukubwa ni inchi 11.6 yenye kukubali hadi miguso 10 kwa wakati mmoja.


Uzito: Kilo 1.3


Sifa ya laptop hizi ni kuwa na nguvu, nafasi kubwa ya diski na uimara wa kufanya kazi muda mrefu bila ya kutetereka. Pia huwa na skrini kubwa mno na hugharimu pesa nyingi kuliko zote. Pia laptop hii inawafaa watu wenye kufanya shughuli zinazohitaji graphics kama vile utengenezaji wa video (video editing), au watu wanaotumia kompyuta kupita kiasi (heavy users)


OS: Windows 8


Prosesa: Intel Core i7-3630QM yenye kasi ya 2.4 GHz, 3.4 GHz ikiwa na TurboBoost, DMI 5 GT/s na 6 MB Cache.


Diski: 1.5TB (2 x 750GB) SATA II (7200 rpm) na 8 GB Express Cache SSD


RAM: 16 GB DDR3 (1600 MHz)


Betri: 8-cell Li-ion (89Wh) pamoja na betri hii kuwa na nguvu kubwa hudumu masaa 3 tu kutokana na nguvu kubwa ya laptop hii katika prosesa, graphics na RAM.


Skrini: ukubwa ni inchi 11.6 yenye kukubali hadi miguso 10 kwa wakati mmoja.


Uzito: Kilo 3.81 ndio laptop nzito kuliko zote tulizozizungumzia


Kadi ya Graphics: Imesimama peke yake (dedicated) NVIDIA GeForce GTX 675M Graphics yenye 2 GB GDDR5.


Laptop hizi ni washindi katika makundi yao kwa kuwa na bei nafuu lakini haina maana ni nafuu kwa ujumla, pia ni nafuu katika soko la UK na sio masoko yote Duniani, ambapo ukweli ni kwamba UK si mahala sahihi pa kutafuta vya rahisi bali ni mahala sahihi pa kutafuta ubora (quality). Usikose makala zijazo tutakapozungumzia Laptop za Convertible (zenye kibodi za kutoka au laptop/tablet)

Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia

 
Kazi nzuri Mkuu lakini Hapo kwenye kipengele cha mwisho umeweka laptop moja tu, Itakua vizuri ukiongeza baadhi maana watu wengi wamekua wakihitaji kununua gaming laptop lakini hushindwa kufahamu aina na mahali pakununulia.
 
Kazi nzuri Mkuu lakini Hapo kwenye kipengele cha mwisho umeweka laptop moja tu, Itakua vizuri ukiongeza baadhi maana watu wengi wamekua wakihitaji kununua gaming laptop lakini hushindwa kufahamu aina na mahali pakununulia.

Sawa kaka nimekupata, muda ukiruhusu tutajaribu kuandika mada inayozungumzia Gamers Laptops peke yake
 
Vipi kuhusu Laptop kutoka brand ya Lonovo?
Ubora na gharama zake ikoje ikilinganisha na brand zingine za Laptop tulizozizoea?
 
Kazi nzuri Mkuu lakini Hapo kwenye kipengele cha mwisho umeweka laptop moja tu, Itakua vizuri ukiongeza baadhi maana watu wengi wamekua wakihitaji kununua gaming laptop lakini hushindwa kufahamu aina na mahali pakununulia.


gaming laptops mwanangu ni story nyingine. unless una upwards ya 1.5m za kuchoma on a new laptop
 
Back
Top Bottom