Lakini hii TRUVADA sasa yamtia kiwewe na kumletea kifaduro……….

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,174

Kweli aliniapia ya kuwa yeye sasa basi imetosha kabisa!
Kweli aliniapia ya kuwa yeye sasa hataki tena hata iweje!
Kweli aliniapia ya kuwa yeye sasa siyo teja wa asali tena!
Kweli aliniapia ya kuwa yeye sasa siyo mshupaliaji wake!
Lakini hii TRUVADA sasa yamtia kiwewe na kumletea kifaduro.

Yawaje kweli yote aliyoniapia kuyaona kazi bure?
Yawaje kweli yote aliyoniapia aone ulikuwa ni utani tu?
Yawaje kweli hata soo asinionee pale anafarijiwa na TRUVADA?
Yawaje kweli muarobaini huo sasa aone ndiyo jibu la tamaa zake?

Ngonjera anazonipa kweli kichwani haziingii hata chembe.
Ngonjera anazotamba nazo bado kwangu ni upuuzi mtupu.
Ngonjera anazojivunia bado hazina uthibitisho hata chembe.
Ngonjera zake zadai eti amechoka kuwakiana nao tamaa kila kuchako.

TRUVADA kwani ni kitu gani kama siyo kinga ya nusunusu?
TRUVADA ni nini kama bado haiko majaribioni tu nawe ni jaribio tu?
TRUVADA ni nini kama siyo chambo ya kukutia majaribuni nawe unaswe?
TRUVADA ni nini kama haiwezi kukulinda kwa asilimia zote kabisa?

Hii mistari ngoja nimtafute P Fanki Majani nitoke na Singo yake naona inaweza kunitoa!
 
TRUVADA..............imezua jambo

lemonade halahala hii TRUVADA isije kutufanya mbaya...............maana hii kuwakiana tamaa sasa yaweza kuchukua sura mpya ya matumaini.............
 
Last edited by a moderator:
"TRUVADA kwani ni kitu gani kama siyo kinga ya nusunusu?"
Hapa mkuu sijaelewa vizuri inakinga, inapunguza makali au inatibu?
 
Mkuu kuipata hiyo TRUVADA kwetu sisi wa dunia ya tatu itakuwa bado ni ndoto! Dozi moja ni zaidi ya Tshs.Milioni, nami naishi chini ya dola moja kwa siku!
 
Truvada zimejaa tele mjini kaka.. sema ndio hivyo wanapewa wale walioathirika tu tena bure kwa msaada wa watu wa marekani
 
Back
Top Bottom