LADY JAY DEE vitani na CLOUDS FM

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,916
Vita ya wasanii na mafisadi inazidi kushamiri kila kukicha, mwaka 2011 tuliona jinsi Anti-Virus Movement ilivyokuja kudai haki za wasanii kwa nguvu ya umma. Hata hivyo, mwenye pesa sio mwenzio na mafisadi walifanikiwa kuzima harakati hizo tena kwa kutumia mkono wa serikali. Hata hivyo, wanamuziki kadhaa wameendeleza harakati zao pamoja na harakati za Anti-virus kuzimwa. Tunaona msanii PeenLawyer alivyofanikiwa kwa kiasi kikubwa alipoamua kuleta mixed tape yake aliyoipa jina la Uswazi Mix tape inayokemea ufisadi katika muziki wetu.

Lakini nani hasa anayelaumiwa kuendekeza rushwa na ufisadi? wasanii amekuwa wakidai kuwa Clouds imekithiri kwa rushwa. Lady Jay Dee hivi punde tu amefunguka kupitia mtandao wa Twitter akidai kudaiwa rushwa ili ngoma yake ya JotoHasiraiweze kupata airtime. Lawama zote zinaonekana wazi kuelekezwa kulekule. Zoma tweets mwanadada Komando Lady Jay Dee aka Wallet hapa chini:

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira"

"Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"

"Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive".

"Hee! Kuna wajinga wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"

" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"

LADY JAY DEE AWASHUKIA CLOUDS MAFISADI WA MUZIKI WA BONGO - Truth Well Told
 
It takes so long time to be trusted but few sec not to be trusted! I think clouds nid to rebrand themselves on how they operate!
 
sa hizi ndo ameona hilo wako wengi lakini wanaogopa kusema labda kwa kua ameanza sasa watajitokeza na wengine.
 
cloud wamejaa wahuni,matapeli,wazinzi,waongo,mafisadi na wezi.Namkumbuka sana Kipanya wakati yuko Cloud,enzi zake cloud haikuwa kijiwe cha wahuni.
 
Wanasema ukipandishwa na wanadamu watakushusha Jide alishawishiwa na Clouda kuacha dini yake ili awe mwanamuziki na kweli umempaisha, anatakiwa alione hili amrudie Mungu ili ibilisi asiendelee kumtesa. Namuombe Mungu amfungue alipofungwa ili asidondoke na shetani ashindwe, maana kuwa na vita si jambo zuri sababu hata ukishinda una uhakika gani adui yako ataendelea kukuangalia ukineemeka?
 
Cloudz!! kinachonishangaza ni style yao ya kutangaza yaani utagundua kwamba huyu ni mwanaume ukisikia 'sauti ya bezi' tu lakini mambo mengine yooote ni kikekike kwa kwenda mbele!!
 
Binti Machozi akumbuke kwamba Gadber Habash alikuwa mtangazaji wa redio ya wafu pia alikuwa manager wa baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva kama Dudu Baya n.k na yeye alikuwa anawachakachua kwa maana halisi.
 
Huyu Dada naye alishawahi kuwa mdau mkubwa wa katika hiyo media, na ndio iliyompa huo umaarufu alionao. Sasa kama kweli alikua anajua kua ubaguzi wa kupendelea nyimbo za wasanii waliopo ktk label ya Clouds kuwa inaua muziki wetu kwanini hakusema kipindi kile ambacho yeye alikua akipendelewa zaidi? Tofauti na hapo bado hajiamini kua anaweza kusimama bila hii media.
 
ukiiinuliiiwaaa na wanaadaamuuuuuuuuu...................!ni laaziiimaaaaaa utashuushwaaa tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu...............
 
Huyu Dada naye alishawahi kuwa mdau mkubwa wa katika hiyo media, na ndio iliyompa huo umaarufu alionao. Sasa kama kweli alikua anajua kua ubaguzi wa kupendelea nyimbo za wasanii waliopo ktk label ya Clouds kuwa inaua muziki wetu kwanini hakusema kipindi kile ambacho yeye alikua akipendelewa zaidi? Tofauti na hapo bado hajiamini kua anaweza kusimama bila hii media.

Kosa ni kuendelea kufanya makosa, yeye ameshtuka kwahiyo na wengine washtuke pia
 
mbunge wangu alipotoka hadharani na kuwakemea clouds fm bungeni, wakamwita mhuni! leo tunazidi kushuhudia uhuni ule ule!
 
Bob Marley aliwahi kusema "You can fool some people for some times but you can't fool all people all the time".. Jay Dee alikuwa fooled for sometimes na sasa amezinduka. naamini wengi watazinduka kama yeye
 
Wanasema ukipandishwa na wanadamu watakushusha Jide alishawishiwa na Clouda kuacha dini yake ili awe mwanamuziki na kweli umempaisha, anatakiwa alione hili amrudie Mungu ili ibilisi asiendelee kumtesa. Namuombe Mungu amfungue alipofungwa ili asidondoke na shetani ashindwe, maana kuwa na vita si jambo zuri sababu hata ukishinda una uhakika gani adui yako ataendelea kukuangalia ukineemeka?

Dini ipi tena hiyo aliyojiunga...please come again..!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom