Ladha za Kwenye Juice za Box/Paketi

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,153
13,223
Badonnasugua kichwa inawezekanaje box/packet likawa na ujazo wa mapera/maembe/mchanganyiko na ladha ile ile halafu liuzwe kwa shilingi mia tano au elfu mbili ili hali kukamua juice yenyewe unahitaji matunda kibao

au tunaongopeana?
 
Badonnasugua kichwa inawezekanaje box/packet likawa na ujazo wa mapera/maembe/mchanganyiko na ladha ile ile halafu liuzwe kwa shilingi mia tano au elfu mbili ili hali kukamua juice yenyewe unahitaji matunda kibao

au tunaongopeana?

Juice inachukuliwa ni fresh kutoka tbs ikiwa matunda yaliyowekwa ni 20%.
 
kinachoongeza ni sukari, rangi(sio zote), maji na preservatives nyingine ili idumu.
 
We kunywa tu but chemicals ni >70%

Hapo upo correct maana bro wangu anafanya kwenye hivo viwanda vya juice vya a..... Matunda wanaweka ila ni kidogo sana.hayazidi 20% . Na tbs wanatambua kuwa ni fresh juice ikiwa matunda ni kuanzia 20% .
 
Hakuna Cha Matunda Hawa 0.1% Hapo Ni Mwendo Wa Radha Na Sukari + Rangi Labda Baadhi Na Gesi Kwa Mbaali Usidanganyike Ni Madawa 100%
 
Badonnasugua kichwa inawezekanaje box/packet likawa na ujazo wa mapera/maembe/mchanganyiko na ladha ile ile halafu liuzwe kwa shilingi mia tano au elfu mbili ili hali kukamua juice yenyewe unahitaji matunda kibao

au tunaongopeana?
Juisi ya aina yoyote iwe Juisi ya Maembe/Mapera/Machungwa/Apple/Mananasi/ukiona imetengenezwa na kuwekwa kwenye Box Au Packet ujuwe hiyo juisi ni Feki. Usinywe ina Madhara ya Sumu ndani yake.

Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi'





BILA shaka unapoingia dukani au supermarket kununua juisi ya box, huwa unaamini kuwa iliyoandikwa ‘100% Pure Juice' huwa ni halisi na ndiyo bora. Kwa kukuongezea imani zaidi, watengenezaji wameweka na neno ‘No Sugar Added' au ‘No preservatives' (haikuongezwa sukari wala dawa)!

Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!


Lakini kwa juisi za maboksi imewezekana kuwa na ladha moja kwa sababu za kikemia zinazofanywa kiwandani wakati wa kuhifadhi juisi hiyo ambayo huweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo siyo kweli kwamba unachokunywa ni asilimia 100 ‘pure'.

NINI KINACHOTOKEA?
Ni kweli kwamba ‘100% pure juice' hutokana na matunda halisi kama vile machungwa, mananasi, embe, n.k, lakini mchakato wake wa kukamua, kuhifadhi na hatimaye kumfikishia mlaji ndiyo wenye dosari za kiafya.

Kinachofanyika baada ya tunda kukamuliwa ni kuhifadhi juisi yake kwenye matanki maalumu makubwa ya viwandani. Ili juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika, wanalazimika kuondoa hewa yake asilia ya oksijeni (mchakato unajulikana kitaalamu kama ‘deaeration'), kitendo ambacho huifanya juisi hiyo kupoteza ladha yake ya asili.

NINI HUFANYIKA KUREJESHA LADHA YA MATUNDA?
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Food Renegade' wa nchini Marekani unaojishughulisha na masuala ya lishe na kuhimiza ulaji wa vyakula asilia, makampuni yanayozalisha juisi hukodisha makampuni yenye ujuzi wa kutengeneza ladha mbalimbali za matunda na manukato.

Makampuni hayo husimamia utengenezaji wa maboksi ya kuhifadhia juisi ambayo huwekwa ladha na harufu ya matunda husika. Inaelezwa zaidi kuwa makampuni hayo ndiyo yanayotengeneza pia manukato (perfumes) maarufu duniani, kama vile Dior na Calvin Klein.

Lakini cha kushangaza, virutubisho vinavyotumika kutengenezea ladha hiyo bandia haviorodheshwi kwenye boksi na wenyewe wanajitetea kwa kusema kuwa ladha hiyo haiwezi kuorodheshwa kama sehemu ya ‘ingredients' kwa sababu hutengenezwa kutokana na tunda lenyewe, ingawa wataalamu wengine wanadai utengenezaji wake huhusisha kemikali zingine ambazo siyo za asili.

Mtaalamu mwingine kutoka Taasisi ya Sera ya Kilimo na Biashara nchini Marekani, Bi. Alissa Hamilton J. D (PhD), ameelezea kwa undani jinsi juisi ya machungwa inavyotengenezwa kiwandani. Undani huo umo kwenye kitabu chake cha; ‘Squeezed: What You Don't Know About Orange Juice'. (Kitu usichokijua kuhusu juisi ya machungwa).

Katika kitabu hicho, mwanadada huyo anasema kuwa ni muhimu kila binadamu kujua kwa undani jinsi chakula chake kinavyoandaliwa, kwa sababu maelezo au lebo inayowekwa kwenye boksi, siyo tu haisemi ukweli, bali pia hailezi ukweli wote.

Anasema kwamba, kama kweli ‘pure orange juice' tunayokunywa ilipatikana baada ya kukamuliwa chungwa peke yake na kuwekwa kwenye boksi, basi bila shaka ladha ingekuwa tofauti kati ya boksi moja na lingine, kwa sababu chungwa moja linatofautiana ladha na chungwa lingine. – mengine matamu, mengine makali.

Mbali na hilo, kila kampuni inayotengeneza juisi ya machungwa ina ladha yake. Juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Tropicana ina ladha tofauti na juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Ceres, sababu ya tofauti hiyo inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.

Chanzo.
Topic: Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi'
 
Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’ PART2

Aidha, Hamilton anaendelea kueleza mchezo mchafu unaochezwa na watengeneza juisi viwandani kwamba ladha ya juisi hiyo ya machungwa hutofautiana pia kati ya nchi na nchi, kwani viwanda huweka aina ya ladha kwenye chungwa kulingana na vile ambavyo wanapenda watu wa eneo inakokwenda.

Juisi inayotengenezwa kwa ajili ya nchi za Amerika Kaskazini huwa na kiwango kikibuwa cha kirutubisho aina ya ‘ethyl butyrate’, ambacho ni moja ya kemikali inayotumika sana kwenye utengenezaji wa manukato na ladha. Mbali ya kirutubisho hicho kuwa na uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za ladha za matunda, lakini pia hakina gharama (cheap).

HATUA GANI ZA KUCHUKUA SASA?
Kama makala haya yatakuwa yamekushitua na kukushangaza, jua hauko peke yako. Hata hivyo, lengo kubwa la makala haya ni kukufumbua macho ujue juisi unayokunywa siyo salama kiasi gani na uwe na uamuzi wa kuicha au kuendelea kuitumia kwa hiyari yako mwenyewe, lakini siyo kwa kudanganywa na maelezo ya uongo ya kibiashara yanayowekwa juu yake.

Kama ambavyo mwandishi wa kitabu hicho Bi. Hamilton anavyosema: “Lengo la kitabu changu siyo kukataza watu kunywa juisi, isipokuwa kuwafanya wakijue vizuri wanachokinywa. Watu wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani utengenezaji wa juisi hivi sasa umekuwa wa kibiashara zaidi, hii itawafanya wawe na maamuzi sahihi kuhusu afya zao.”

Ingawa ni vigumu sana kuepuka ‘kuingizwa mkenge’, lakini unaweza kujiepusha na madhara ya kiafya yatokanayo na unywaji wa juisi hizi ‘feki’ kwa kupendelea kunywa juisi uliyoitayarisha mwenywe nyumbani na kuacha kununua vyakula au vinywaji ‘ready made’, hasa kwa vile ambavyo vinapatikana kwa wingi sokoni.

TAHADHARI
Kwa ujumla matunda na juisi zake zina virutubisho vingi muhimu kwa ustawi wa afya ya binadamu, lakini tahadhari inatolewa kwa wanaopenda kunywa kiasi kingi cha juisi za matunda, hasa juisi ya machungwa ambayo inaelezwa kuwa na sukari nyingi.

Kiasi cha glasi moja ya juisi ya machungwa ina wastani wa gramu 25 za ‘fructose’, (sukari), kiwango ambacho ni cha mwisho kabisa anachotakiwa mtu kutumia kwa siku moja. Hii ina maana kama utakunywa zaidi ya glasi moja pamoja na vinywaji vingine vinavyotumia sukari, kama vile chai, tayari utakuwa umezidisha kiwango kinachopendekezwa kwa siku.

Iwapo utakuwa na tatizo la unene na unahitaji kupunguza uzito, ni vyema ukapunguza sana au ukajiepusha kabisa na uywaji wa juisi za matunda, kwa sababu kiwango cha sukari kilichomo ni zaidi ya wastani unaotakiwa.

Ili upate faida za virutubisho vinavyopatikana kwenye matunda, yakiwemo machungwa, unashauriwa kula matunda hayo kama yalivyo kuliko kukamua juisi na kutupa makapi yake. Inaelezwa kwamba sukari iliyomo kwenye chungwa inapoliwa pamoja na nyama zake (fibre), sukari hiyo huwa haina madhara kwani huweza kujichanganya kwenye mfumo wa damu bila kuleta athari zozote kwa mlaji.

Hivyo ushauri wa ujumla unatolewa kwamba pendelea zaidi kula matunda na mboga za majani kama zilivyo kuliko kunywa juisi zake. Kwa kufanya hivyo utajiepusha na uwezekano wa kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Iwapo utakunywa, basi kunywa nusu glasi au isizidi glasi moja kwa siku. Asanteni.

 
Saf sana umeeleza vizuri.... Nlikimbia soda... Sasa juice hawanipati... Ila beer sijafaanya utafiti kama ile ni pure Ngano...... Anyway ngoja niangalie upande wa tbl....
 
kwa hiyo ni matunda kweli?

kwa baadhi ya juice hutumia matunda kweli,, lakini kuna nyingine sio matunda kuna product maarufu kwa jina la LADHA, hii inaharufu na ladha kama matunda japo ni chemicals tu, na huchanganya vyote juice kidogo na LADHA nyingi ili kupinguza gharama za matunda.
 
Nakubaliana na wewe MziziMkavu. Panapowezekana tule/tunywe juisi kutoka matunda asilia na sio yaliyotengenezwa na kuhifadhiwa kwenya maboksi/chupa.
 
Back
Top Bottom