Labda sioni au nimekosea, Ng'ombe anaweza kuwa hivi?

Kama hujawahi kumuona live haimaanishi kuwa hayupo! Mie nimebahatika kuwaona hao ng'ombe live ndio nikawashirikisha.

Ushauri wa bure: wakati mwingine usimwambie mtu ni muongo ilhali wewe haujui ukweli ni upi. Pendelea kujifunza zaidi badala ya kutegemea vya kutafuniwa tu!!
Tuna shida ya kudhani mazingira tuliyomo ndo yalivyo kwa ulimwengu mzima! Na hii hutufunga fikra za kujifunza na kupata mawazo mapya!

Utagundua comments nyingi ni za kudhani hakuna ng'ombe wa aina hii duniani, huyu atakuwa ametengenezwa na wengine hadi washasema atakuwa hatari kwa afya! Wengine hadi aina ya cancer washaijua!!!!

Huku kujua kwingi huku ni shida!

Kama hapa bongo tu tuna breed zina uzito wa tani 1, utashangaaje tani 2! Nimetembelea banda la NARCO pale nane nane morogoro kwa miaka 3 mfululizo, nakutana na ng'ombe wa kg 900, hadi 1,100, nitashangaaje kwa wenzetu kuna wa kg 2,000?

Kwa mnaokumbuka, wakati JK ameenda Zambia akiwa rais akaenda kushangaa ng' ombe wa kilo 800, MTU mmoja Iringa akasema Mimi ninao wa hadi 1,300Kg, na kama mnakumbuka Jk aliporudi alienda kumtembelea, tukaonyeshwa na wa maziwa waliokuwa wanatoa Lita 37 kwa siku, na hakuwa Asas!

Niliwahi ongea na mzee wangu mmoja wakati ninashangaa ng'ombe wenye uzito wa 1000kg, akaniambia wakati wa mwalimu tuliwahi pewa mbegu toka Russia na wakapelekwa pale mwanza chuo cha kilimo, anasema walikuwa na uzito wa 1,500 kg hadi 1,700 kg, hawakuwa wanafungwa kamba, ilikuwa ni minyororo tena kupitia puani!

Akasema uzalishaji wake haukuendelea maana walikuwa wakorofi sana na waliua wafanyakazi wengi sana na ilifikia hatua wanauawa kwa risasi!

Kanda ya Geita, ngala na bihalamulo kuna breed jamii ya ankole wana jina la kuenyeji wanaitwa "nyabugesela" ukikutana na dune lake la miaka 5, linalotunzwa vizuri, kwa uliyezoea aina za Zebu na Tarime, sijui utasemaje!!!

Ni kweli kwa tusivyojua tusikimbilie ujuaji na kuita watu waongo na kurukia utafiti hadi wa madhara kwa kuongozwa na uelewa wetu finyu!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom