Elvis Legacy
JF-Expert Member
- Aug 10, 2017
- 3,396
- 4,740
Asalaam
Watanzania wenzangu. Pasipo na shaka yoyote nimejiridhisha kuwa tupo katika kifungo cha ufukara kutokana na laana za kuwasaliti mababu zetu na mila zetu nzuri.
Naomba tuungane kwa kuombea laana hizi zitutoke tuwe huru na hatimaye tupige hatua kimaendeleo.
1.Tukemee laana ya vijana na wazee kutumia muda mwingi kujadili Simba na Yanga kuliko mstakabali na maslahi ya nchi kama kupatikana kwa katiba mpya itakayowawajibisha watawala na kuwapa wananchi nguvu ya maamuzi kwenye nchi yao.
2. Tukemee laana ya kuchagua viongozi wajinga kuanzia mtaa,kata,jimbo hadi taifa. Tuombe mababu zetu watuoneshe viongozi wanaofaa sio kuchagua kwa itikadi zao za vyama.
3. Tukemee laana ya uoga wa kutetea haki zetu, uvivu wa kifikiri, na kutokuwa na maono ya mbali ili kulikomboa taifa letu kwa hawa wakoloni weusi.
4. Tukemee laana ya kufanywa vikaragosi wa kukimbiza moto mchana.
Mengine mtaongezea. Mwaka 2024/2025 tukapate viongozi sio watawala.
Watakatifu mababu na mabibi zetu tunaomba mtusamehe kwa kuwasaliti na tutaenzi mila zote nzuri mlizotuachia. Zile mbaya mtatusamehe.