Laana kubwa imeikumba CCM nzima kwa dhuluma kubwa kwa watu masikini -Umemuona Bi.Mwajuma Ramadhani?

Hamna dhulma hapo, haman anaemiliki kilicho chini ya Ardhi wala huwezi kukirithi. Yeye chake ni cha juu ya ardhi. Huyo bibi akajipumzikie hao wanaomtumia kisiasa ndio wanaomdhulumu na ndio wenye laana.

FF land includes mines and minerals, whether or not held apart from the surface. And ‘mines and minerals' include any strata or seam of minerals or substances in or under any land, and powers of working and getting the same. So, land ownership include the right to minerals underneath and the airspace over it.

Ila aliyeleta hii issue kama vile ameileta kisiasa. Bongo kila kitu ni siasa.
 
katumika kisiasa... mwenye 106 years anamjuaje ngeleja??

i dont like ufedhuli lakini siasa ikizidi balaa

Inashangza Yaani kuna wtu kwa life expecatancy yetu Tanzania bado wanaweza kumeza maelezo haya bila kujiliza mambo kadhaa. Sasa Ngeleja na kafumu si majina ya kanda ya ziwa huko. Kuyataja hayo majina inaashiria nini kwani?
 
FF land includes mines and minerals, whether or not held apart from the surface. And ‘mines and minerals' include any strata or seam of minerals or substances in or under any land, and powers of working and getting the same. So, land ownership include the right to minerals underneath and the airspace over it.

Ila aliyeleta hii issue kama vile ameileta kisiasa. Bongo kila kitu ni siasa.

Mkuu hapa siasa ni ipi ? Mie nimeona news kwenye TV basi nikaona wacha tuje kujadili hapa kosa la presentation ni lipi ? Nimeileta kavu kavu bila ya kuchambua chochote .
 
Mkuu hapa siasa ni ipi ? Mie nimeona news kwenye TV basi nikaona wacha tuje kujadili hapa kosa la presentation ni lipi ? Nimeileta kavu kavu bila ya kuchambua chochote .

Kichwa cha habari: "Laana kubwa imeikumba CCM nzima kwa dhuluma kubwa kwa watu masikini -Umemuona Bi.Mwajuma" Au ndio ilivyotoka kavu kavu ITV? Pia rudia kusoma post yako. Kuna issue nyeti kwenye huu uzi but your presentation inafanya watu wengine waone kama imekaa kichama zaidi which of course is not wrong. Pia mimi kusema uzi umekaa kisiasa sio sehemu ya majadiliano?
 
Kichwa cha habari: "Laana kubwa imeikumba CCM nzima kwa dhuluma kubwa kwa watu masikini -Umemuona Bi.Mwajuma" Au ndio ilivyotoka kavu kavu ITV? Pia rudia kusoma post yako. Kuna issue nyeti kwenye huu uzi but your presentation inafanya watu wengine waone kama imekaa kichama zaidi which of course is not wrong. Pia mimi kusema uzi umekaa kisiasa sio sehemu ya majadiliano?

Sawa mkuu nimekusoma lakini hii laana kwa CCM hujaiona ? Maana haiwezi kuwa ya Tanzania kwa kuwa madini yetu ndiyo ynayo umiza watanzania masikini na wana siasa wana kula na wageni .Huyu mama kalia kataja wote zaidi ya 4 wote ni ni wana siasa na wana CCM wote .Sasa hapa inakaaje hii mkuu ? Tuendelee kupeana elimu .
 
Ndugu wana JF nilikuwa naangalia news hapa kweli nime shake .Yule mama wa miaka 106 kutoka Geita hadi Dar kutafuta haki tena hana nauli kwa kuomba lift .Kamtaja Ngeleja, Kamtaja Kafumu, na wengine .Katishiwa maisha , kaporwa eneo lake la madini na nij urithi.Kweli laana iko CCM na serikali yetu .Yule mama akahamie wapi afanye nini ? Jamaniu nyie mnasemaje ? Mmemuona mama analia hadharani ITV ?

Mimi sisemi chochote kuhusu huyo bibi, ila naomba tu kukumbushwa kuhusu wale mababu wa East Africa ambao walidai kwamba mwenzao mmoja alipigwa risasi na kuuawa na polisi wakati wakiandamana pale mahakama kuu! Hivi arobaini ya yule babu aliyepigwa risasi ishapita?! nimeu-miss sana mpunga wa kwenye hitima; manake ni mtamu balaa!

Pole sana bibi, mungu akuzidishie nguvu!
 
:shock:Ushindwe na ulegee! unadhani kuwa na umri mkubwa ni chanzo cha utahira? ndio tuseme wewe ukizeeka utakuwa bongo sinzia na udenda ukikutoka? Naona ungekuwa Shinyanga ungewa mwuaji mkubwa wa vinkongwe. Baba yangu ana 92 lakini ana sound mind, anaweza kujenga hoja na anajua news za yanayoendelea duniani!!

kuna mzee mmoja yupo 96 yupo vizuri sana upstairs. anajua alipostaafu alipata kiasi gani.. na anatakiwa apate nini kama pensheni. pia anajua kuweka rekodi za vipimo anavyofanyiwa si mchezo.... akipimwa pressure au sukari anaweka rekodi yake vizuri i.e. tarehe, nani kapima, majibu n.k.
 
Miaka 106 alionyesha cheti cha kuzaliwa? Anatembea huyo? Geita unaijua au unaisikia. Huyo ni mkuu wa idara ya gamboshi. Jihadharini na siku za mwisho
 
Ndugu wana JF nilikuwa naangalia news hapa kweli nime shake .Yule mama wa miaka 106 kutoka Geita hadi Dar kutafuta haki tena hana nauli kwa kuomba lift .Kamtaja Ngeleja, Kamtaja Kafumu, na wengine .Katishiwa maisha , kaporwa eneo lake la madini na nij urithi.Kweli laana iko CCM na serikali yetu .Yule mama akahamie wapi afanye nini ? Jamaniu nyie mnasemaje ? Mmemuona mama analia hadharani ITV ?
asa kila kitu kina mwisho walishazoea kuibia maskini ila mungu atawapiga kofi tu...
 
katumika kisiasa... mwenye 106 years anamjuaje ngeleja??

i dont like ufedhuli lakini siasa ikizidi balaa

we akili zako zimeganda yaelekea.. siasa ndio inayoongoz anchi nawewe upo jamii hapa kwa kuwa unafuata siasa za nchi yako.kwan kuwa 106yrs hana akili ama?ni sawa na mtu kuvunjika mguu akahuliza akaambiwa madokta wa mifupa wapo moi muhimbili na akifika hapo lazima atamjua mkuu wa kitengo mabye ndio ngeleja kwa upande wa madini
 
Hamna dhulma hapo, haman anaemiliki kilicho chini ya Ardhi wala huwezi kukirithi. Yeye chake ni cha juu ya ardhi. Huyo bibi akajipumzikie hao wanaomtumia kisiasa ndio wanaomdhulumu na ndio wenye laana.
USIONGEE KM UNAHARISHA NA MDOMO.hv yule mzazi wako kule sigimbi anayeish kwenye nyumba yk ya msonge serikali wakija wakimfukuza na kuchukua ardhi yk, mkidai haki yenu mtakua mnatumika kisiasa?
 
USIONGEE KM UNAHARISHA NA MDOMO.hv yule mzazi wako kule sigimbi anayeish kwenye nyumba yk ya msonge serikali wakija wakimfukuza na kuchukua ardhi yk, mkidai haki yenu mtakua mnatumika kisiasa?

Kwa nini mjadala wa huyu Bibi maskini unachukuliwa kirahisi sana ? Hii ni dhuluma kuna makosa anaweza kusema yule bibi wa umri wake anaweza asiwe sahihi na umri wake lakinisi kubezwa .Katoka Geita si kwa miguuu ameomba lift na kawashukuru maaskari wa Usalama barabarani wamekuwa wanamuombea lift kwenye magari hadi kafika Dar .

Kaja na karatasi zake kumbuka wabibi wengi ni CCM hawawezi kuibuka kirahisi tu na madai mazito kama haya .Thinkers let's come back to our sense tuachane na mijadala ya kitoto kila mara .Jikite kwenye hili kwanza .
 
.hawa wazee wanatakaga wenyewe angesema kipindi cha kampeni kamfumu angempa haki yake na angesaidia wana igunga kumfahamu huyu mtu sasa mwache akome na liwe funzo kwa wengine na wazee wenzake wanayo ipa kura ccm
Naungana na wewe, hapa hakuna hoja. Huyo bibi nahisi karukwa akili tu. Haiwezekani jambo hili liwe real. Mbona wastaaf wa iliyokuwa east african community huwa wanachapwa mboko hadharani wakijidai kutafuta haki yao, sembuse kikongwe huyu, mwambieni akajinyonge pale kwenye miti ya magogoni akiwa na makabrasha yake, hapo ndio tutaamini, ni utomaso tu sasa hapa potelea mbali kudadadeki, mshatufanya mazuzu kiasi cha kutosha sasa ni vurugu tu ustaarabu sitaki tena, potelea mbali....
 
hakuna sheria tanzania kwa wenye madaraka sasa nani atamsikiliza zaidi ya sisi kumuonea huruma?tujipange jamani hii nchi iendako siyo kabisa
 
AZIMIO LA ARUSHA NA SIASA YA TANU JUU YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA
Imetolewa na Idara ya Habari,
TANU, Dar es Salaam, 1967

SEHEMU YA KWANZA
Imani ya Tanu

SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA
IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII
Kwa kuwa TANU inaamini:-

(a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
(b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;
(c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya
kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya
Mikoa hadi Serikali Kuu;
(d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo
yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na
wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;
(e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii
hifadhi ya maisha yake na ya mali yake aliyonayo kwa
mujibu wa Sheria;

(f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki
kutokana na kazi yake
(g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili
wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana
kwa vizazi vyao;
(h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda
sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia
muhimu za kuukuza uchumi; na
(i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,
kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili
kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya
mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine
na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani
na siasa ya watu wote kuwa sawa.

MADHUMUNI YA TANU

Kwa hiyo basi, makusudi na madhumuni ya TANU yatakuwa kama
hivi yafuatavyo:-
(a) Kuudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake;

(b) Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara
kanuni za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu.
(c) Kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na Serikali ya
watu ya kidemokrasia na ya kisoshalist;
(d) Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika
vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika;
(e) Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa
kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi;
(f) Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na
kudumisha vyama vya ushirika;
(g) Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa
katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu;
(h) Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote,
wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;
(i) Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma,
vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;

(j) Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara
njia kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo
itarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu;
(k) Kuona kwamba Serikali inashirikiana na dola nyingine katika
Afrika katika kuleta Umoja wa Afrika.
(l) Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salama
ulimwenguni kwa njia ya Chama cha Umoja wa Mataifa.






SEHEMU YA PILI
SIASA YA UJAMAA

(a) Hakuna Unyonyaji:
Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina
ubepari wala ukabaila. Haina tabaka mbii za watu: tabaka ya
chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya
watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa
kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi
hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi
aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali
hayapitani mno.
Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi
kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao
ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao,
kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya
kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe.
Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini sin
chi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
ikapanuka na kuenea.

(b) Njia kuu za uchumi ni chini ya wakulima na wafanya
kazi:
Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha ujamaa ni
kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu
zinatawaliwa na kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi
wenyewe kwa kutumia vyombo vya Serikali yao na Vyama
vyao vya Ushirika. Pia ni lazima kuthibitisha kuwa Chama
kinachotawala ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.
Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini,
maji, mafuta na nguvu za umeme; njia za habari, njia za
usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na
biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari,
simenti, mboleo; nguo, na kiwanda cho chote kikubwa
ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika
kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine;
mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima
katika viwanda vikubwa.
Baadhi ya njia hizi na nyingine zisizotajwa hapa hivi sasa
zinamilikiwa au kutawaliwa na Serikali ya Wananchi.

(c) Kuna Demokrasi:
Nchi haiwi ni ya Ujamaa kwa sababu tu njia zake kuu au
zote za uchumi hutawaliwa na humilikiwa na Serikali. Sharti
Serikali iwe inachaguliwa na kuongozwa na Wakulima na
Wafanya kazi wenyewe. Serikali ya Makaburu wa Rhodesia au
Afrika ya Kusini ikitawala au kumiliki njia zote za uchumi, hiyo
itakuwa ni njia ya kukomaza Udhalimu siyo njia ya kuleta
Ujamaa. Hakuna Ujamaa wa kweli pasipo na Demokrasi ya
kweli.
(d) Ujamaa na Imani:
Lakini Ujamaa hauwezi kujijenga wenyewe. Kwani
Ujamaa ni imani. Hauna budi kujengwa na watu wanaoamini
na kufuata kanuni zake. Mwana-TANU wa kweli ni Mjamaa, na
Wajamaa wenzie, yaani waamini wenzie katika imani hii ya
kisiasa na uchumi ni wote wale wanaopigania haki za wakulima
na wafanyakazi katika Afrika na po pote duniani. Wajibu wa
kwanza wa mwana-TANU na hasa kiongozi wa TANU, ni kutii
kanuni hizi za ujamaa hasa katika maisha yake mwenyewe. Na
hasa mwana-TANU kiongozi hataishi kwa jasho la mtu
mwingine au kufanya jambo lo lote ambalo ni la kibepari au
kikabaila.

Utimizaji wa shabaha hizo na nyinginezo zinazofuatana na
siasa ya ujamaa unategemea sana viongozi kwa sababu ujamaa
ni imani na ni vigumu kwa viongozi kujenga siasa ya ujamaa
ikiwa hawaikubali imani hiyo.










SEHEMU YA TATU
SIASA YA KUJITEGEMEA
Tunapigana vita:
TANU ina vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na
kulitia katika hali ya nguvu; vita vya kuwafanya wananchi wa
Tanzania (na wananchi wa Afrika) watoke katika hali ya dhiki na
kuwa katika hali ya neema.
Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha,
na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya
tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi;
mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena.
Mnyonge hapigani kwa Fedha:
Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua
silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa
unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo
sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na
vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi
yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, “Fedha ndiyo msingi wa
maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo”!
10
Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni
kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,
mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa
wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT.,
Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi,
mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama
wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, “Tukipata fedha
tutaendelea, bila fedha hatutaendea”!
Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake
kwa kifupi ni shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yetu
tuliyotilia mkazo sana ni fedha. Ni kama tumesema, “Katika miaka
mitano ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na afya, na ili
kutimiza shabaha hizo tunatumia $ 250,000,000”. Kama tumetaja na
tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha hizo tunavitaja
kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika akili zetu, silaha
kubwa katika mawazo yetu, ni FEDHA.
Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu
yake wana shida ya maji, je Serikali ina mpango gani wa kuondoa
shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa
kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo – KWA FEDHA.
Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina
barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani?

Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao
mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga shule au
hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge Mheshimiwa
huyo - kwa FEDHA.
Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya
chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba
wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo
kusikia ni kuwa Serikali inao mpango maalum wa kuongeza
mishahara na kujenga majumba bora - KWA FEDHA.
Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana
ambazo hazipati msaada wa Serikali. Je Serikali ina mpango gani wa
kuzisaidia shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko
tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa -
wa FEDHA!
Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yo yote ya
mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za
mkulima – kwa FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili Taifa letu
wananchi tunawaza Fedha, Fedha, Fedha!
Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya
makadirio yake ya matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo
kwa kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na

Wizara moja tu hushughulikia pia kufanya makadirio ya mapato. Ni
Waziri wa Fedha. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya
maendeleo. Wizara zinapoleta makaidirio yao ya matumizi huwa
zinaamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Waziri wa Fedha na
Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara yake
awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna fedha.
Na kila mwaka Wizara zote huinung’unikia Wizara ya Fedha kwa
kupunguza Makadirio yao ya matumizi.
Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali
itimize mipango mbali mbali huwa nao wakiamini kwamba fedha zipo
ila mkorofi ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge
na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba
Serikali haina fedha.
Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini?
Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi
walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha
shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi.
Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha
tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha
zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya
kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi

zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi
bila kutaka Ng’ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri
kwamba tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka
Serikali iongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa
kuongeza kodi. Tunatambua kuwa ng’ombe hana maziwa zaidi;
kwamba hata ng’ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo
au yanywewe na ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa
yake; utashi huo hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa
zaidi.
Fedha kutoka nje ya Tanzania, Je?
Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri
kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za
kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-
(a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure
tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo.
Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au
Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya
maendeleo.
(b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata
kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo.
Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha

Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za
maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa,
kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.
(c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa
kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni
yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali
mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti
kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba
shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba
Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka
kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa
wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao.
Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya
nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili
la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na
viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia
za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata
ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na
viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa
neema imekuja au iko njiani inakuja. Tukipata msaada
hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda
kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda
kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au

shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara
hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo
hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza
mazungumzo ya neema!
TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO
Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza
kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka
nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.
Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo
zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani
ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga
viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.
Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote
zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa
msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata
katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili
zisaidie Serikali kuondoa dhiki.
Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza
kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo

maana japo tungewakamua vipi wnanachi na wakazi wa Tanzania,
matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza
mipango yetu ya maendeleo. Wala duniani hakuna Serikali ambayo
yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili
kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna
Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa
huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe.
Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.
MISAADA NA MIKOPO
VITAHATARISHA UHURU WETU
Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka
kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli
hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya
Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au
mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji
kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi
yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini
kwa Uhuru wetu na uzima wetu.
Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au
nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada

unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza
maswali.
Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya
“bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada
itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha
jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe
kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya
kukuwezesha kuulipa.
Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa.
Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama
tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu
maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni
kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa
walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.
Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka.
Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni
wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia
yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi
inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama
italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila
vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali
mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha. Lakini hata

kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni
hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji
katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli?
Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka
Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na
mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi
kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha
uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata
faida na kuipeleka katika nchi zao? Hata kama wasingedai
kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata
wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli
tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu? Huu
Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje?
Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa
misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha
uhuru wetu? Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji
ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na
Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila
kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu
wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.
Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu
ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu ya

maendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka
nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata
fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama
tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na
siasa nyingine za nchi yetu.
TUMEKAZANIA MNO VIWANDA
Kwa sababu ya kutilia mkazo fedha tumefanya kosa kubwa la
pili. Tumekazania mno viwanda. Kama vile tulivyosema “Bila Fedha
hakuna maendeleo,” ni kama twasema pia “Viwanda ndiyo
maendeleo. Bila viwanda hakuna maendeleo”. Hii ni kweli siku
tutakapokuwa na fedha nyingi, tutaweza kusema kwamba
tumeendelea. Tutaweza kusema, “tulipoanza mipango yetu tulikuwa
hatuna fedha za kutosha na upungufu huu wa fedha ulitupunguzia
nguvu za kuendesha maendeleo yetu haraka zaidi. Lakini leo
tumeendelea na tunazo fedha za kutosha”. Tumeendelea,kwa hiyo,
tunazo fedha za kutosha”. Yaani fedha zetu zitakuwa zimeletwa na
maendeleo.
Kadhalika siku tutakapokuwa na viwanda tuna haki ya kusema
kuwa tumeendelea. Maendeleo yatakuwa yametuwezesha kupata
viwanda. Kosa tunalofanya ni kudhani kwamba maendeleo yetu
yataanza kwa viwanda. Ni kosa maana hatuna uwezo wa kuanzisha
viwanda vingi vya kisasa katika nchi yetu. Hatuna fedha

zinazohitajiwa na hatuna ufundi unaohitajiwa. Haitoshi kusema kuwa
tutakopa fedha na kuazima mafundi kutoka nje kuja kuanzisha
viwanda hivyo. Kosa hili jibu lake ni lile lile kwamba hatuwezi kupata
fedha za kutosha na kuazima mafundi wa kutosha kutuanzishia
viwanda hivyo tunavyotaka. Na pia kwamba hata kama tungeweza
kupata msaada huo kuutegemea huko kunaweza kukapotosha siasa
yetu ya Ujamaa. Siasa ya kualika msululu wa mabepari kuja kuhozi
viwanda katika nchi yetu ingefanikiwa kutupatia viwanda vyote
tunavyotaka, basi ingefanikiwa pia kuzuia maendeleo ya Ujamaa. Ila
labda tuwe tunaamini kwamba bila kujenga ubepari kwanza hatuwezi
kujenga Ujamaa.
TUMJALI ZAIDI MKULIMA VIJIJINI
Vile vile mkazo wa fedha na wa viwanda unatufanya tukazanie
zaidi maendeleo ya mijini. Tunatambua kuwa hatuwezi kupata fedha
za kutosha kuleta maendeleo katika kila kijiji na ambayo yatamfaa
kila mwananchi. Tunajua pia kuwa hatuwezi kujenga kiwanda katika
kila kijiji ili kisaidie kuleta maendeleo ya fedha na viwanda katika kila
kijiji; jambo ambalo tunajua kuwa haliwezekani. Kwa ajili hiyo, basi,
fedha zetu huzitumia zaidi katika miji na viwanda vyetu pia hujengwa
katika miji.
Na zaidi ya fedha hizi huwa ni mikopo. Japo zijenge shule,
hospitali, majumba au viwanda ni fedha za mikopo. Hatimaye lazima
21
zilipwe. Lakini ni dhahiri kwamba haziwezi kulipwa kwa fedha
zinazotokana na maendeleo ya mijini au maendeleo ya viwanda.
Hazina budi zilipwe kwa fedha tunazopata kutokana na vitu
tunavyouza katika nchi za nje. Kutokana na viwanda vyetu hatuuzi
na kwa muda mrefu sana hatutauza vitu vingi katika nchi za nje.
Viwanda vyetu zaidi ni vya kutusaidia kupata vitu hapa hapa
ambavyo mpaka sasa tunaviagiza kutoka nchi za nje. Itapita miaka
mingi kabla ya kuweza kuuza katika nchi za nje vitu vinavyotokana na
viwanda vyetu.
Kwa hiyo ni dhahiri kwamba fedha tutakazotumia kulipa madeni
haya ya mikopo ya fedha kwa maendeleo na viwanda mijini
hazitatoka mijini na wala hazitatokana na viwanda. Zitatoka wapi,
basi? Zitatoka vijijini na zitatokana na KILIMO. Maana ya ukweli huu
ni nini? Ni kwamba wale wanaofaidi maendeleo yanayotokana na
fedha tunazokopa sio kwa kweli watakaozilipa. Fedha zitatumika
zaidi katika miji lakini walipaji watakuwa zaidi ni wakulima.
Jambo hili linafaa kukumbukwa sana, maana kuna njia nyingi
za kunyonyana. Tusisahau hata kidogo kwamba wakaaji wa mijini
wanaweza wakawa wanyonyaji wa jasho la wakulima wa vijijini.
Hospitali zetu kubwa zote ziko katika miji. Zinafaidia sehemu ndogo
sana ya wananchi wa Tanzania. Lakini kama tumezijenga kwa fedha
za mkopo walipaji wa mkopo huo ni wakulima, yaani wale ambao
hawafaidiwi sana na hospitali hizo. Mabarabara ya lami yako katika

miji, kwa faida ya wakaaji wa mijini na hasa wenye magari. Kama
mabarabaraba hayo tumeyajenga kwa fedha za mikopo walipaji ni
wakulima; na fedha zilizonunua magari yenyewe zilitokana na mazao
ya wakulima. Taa za umeme, maji ya mabomba, mahoteli na
maendeleo mengine yote ya kisasa yako zaidi katika miji. Karibu
yote yametokana na fedha za mikopo na karibu yote hayana faida
kubwa kwa mkulima, lakini yatalipwa kwa fedha zitakazotokana na
jasho la mkulima. Tusisahau jambo hili.
Japo tunapotaja unyonyaji hufikiria mabepari, tusisahau kuwa
bahari ina samaki wengi. Nao hutafunana. Mkubwa hutafuna mdogo
na mdogo naye humtafuna mdogo zaidi. Katika nchi yetu twaweza
kugawa wananchi kwa njia mbili. Mabepari na Makabaila upande
mmoja; na wafanya kazi na wakulima upande mwingine. Pia
twaweza tukagawa wakaaji wa mijini upande mmoja na wakulima wa
vijijini upande mwingine. Tusipoangalia tutakuja kugundua kuwa
wakaaji wa mijini nao ni wanyonyaji wa wakulima.
WANANCHI NA KILIMO
Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha.
Fedha ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji
vitu vine: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora.
Nchi yetu ina zaidi ya watu milioni kumi na eneo la eka 362,000.

MAENDELEO YATALETWA NA KILIMO
Sehemu kubwa ya eneo hili ni yenye rutuba na mvua ya
kutosha. Nchi yetu inaweza kutoa mazao ya aina mbali mbali
ambayo tunayahitaji kwa chakula na kwa fedha.
Mazao ya chakula (na fedha kama tukiyatoa kwa wingi) ni
kama vile mahindi, mchele, ngano, maharage, karanga n.k. Mazao
ya fedha ni kama vile mkonge, pamba, kahawa, tumbaku, pareto,
chai n.k.
Pia nchi yetu ni nzuri sana kwa ufugaji wa ng’ombe, mbuzi,
kondoo, kuku n.k. Pia twaweza kuvua samaki katika maziwa, bahari
na mito.
Wakulima wetu wako katika sehemu ambazo zaweza kutoa
mazao haya, kama si yote walau mawili matatu au hata zaidi. Kila
mkulima wetu aweza akaongeza mazao haya ili ajipatie chakula kingi
zaidi au fedha nyingi zaidi. Na kwa sababu nia kubwa ya
maendeleo ni kupata chakula zaidi na fedha zaidi kwa ajili ya
kujipatia mahitaji yetu mengine, ndiyo kusema kuwa jitihada ya
kuongeza mazao ni jitihada, na kwa kweli ndiyo jitihada peke yake,
ambayo italeta maendeleo, yaani chakula zaidi na fedha zaidi kwa
kila mwananchi.

MASHARTI YA MAENDELEO
(a) Juhudi:
Kila mwananchi anataka maendeleo, lakini si kila mwananchi
anaelewa na kukubali masharti ya maendeleo. Sharti moja
kubwa ni JUHUDI. Twendeni vijijini tuzungumze na wananchi
kuona kama inawezekana au haiwezekani wananchi kuongeza juhudi.
Kwa mfano, katika miji, mfanyakazi wa mshahara hufanya kazi
kwa saa saba na nusu au nane kutwa kwa muda wa siku sita au sita
na nusu kwa juma. Tuseme saa 45 kwa juma, kuondoa majuma
mawili au matatu ya livu, katika mwaka mzima. Ndiyo kusema
mfanya kazi wa mjini hufanya kazi ya saa 45 kwa juma kwa majuma
48 au 50 kwa mwaka.
Katika nchi kama yetu muda huu ni mdogo kwa kweli. Nchi nyingi
hata zilizoendelea kutuzidi – hufanya kazi kwa muda mrefu zaidi
kuliko saa 45 kwa juma. Si jambo la kawaida nchi changa kuanza na
muda mfupi kama huo. Jambo la kawaida ni kuanza na muda mrefu
zaidi na kuupunguza kila nchi inavyozidi kuendelea. Sisi kwa kuanza
na muda mfupi huu na tunapodai muda mfupi zaidi kwa kweli tunaiga
nchi zilizoendelea. Na kuiga huku kunaweza kukaleta majuto. Lakini
hata hivyo wafanya kazi wa mishahara hufanya kazi ya saa 45 kwa
juma; livu yao kwa mwaka haizidi majuma manne.

Yafaa kujiuliza wananchi wakulima hasa wanaume, hufanya kazi kwa
saa ngapi kwa juma na miezi mingapi kwa mwaka. Ni wengi mno
ambao hawatimizi hata nusu ya wastani wa mfanyakazi wa
mshahara.
Ukweli wenyewe ni kwamba vijijini kina mama hufanya sana kazi.
Pengine hutimiza saa 12 au 14 kutwa. Hawana Jumapili, na hawana
livu. Kina mama wa vijijini hufanya kazi zaidi kuliko mtu mwingine ye
yote katika Tanzania. Lakini kina baba wa vijijini (na baadhi ya kina
mama wa mijini) nusu ya maisha yao ni livu. Nguvu hizi za mamilioni
ya kina baba vijijini na maelfu ya kina mama wa mijini ambazo hivi
sasa hazifanyi kazi yo yote ila kupiga soga, kucheza ngoma na
kunywa pombe, ni hazina kubwa yenye manufaa zaidi kwa maendeeo
ya nchi yetu kuliko hazina za mataifa matajiri.
Tutafanya jambo la faida kubwa kwa nchi yetu kama tukienda vijijini
na kuwaambia wananchi kwamba wanayo hazina hii na kwamba ni
wajibu wao kuitumia kwa faida yao wenyewe na faida ya Taifa letu.
(b) Maarifa:
Sharti la pili la maendeleo ni MAARIFA. Juhudi bila maarifa haiwezi
kutoa matunda bora kama juhudi na maarifa. Kutumia jembe kubwa
badala ya jembe dogo, kutumia jembe la kuvutwa na ng’ombe badala

ya jembe la mkono, kutumia mbolea badala ya ardhi tupu,
kunyunyizia dawa ili kuuwa wadudu, kujua ni zao gani lifaalo
kupandwa na zao gain lisilofaa, kuchagua mbegu vizuri kabla ya
kuzipanda, kujua wakati mzuri wa kupanda, wakati wa kupalilia n.k.,
ni maarifa yanayowezesha juhudi kutoa mazao mengi zaidi.
Fedha na wakati tunaotumia kuwapa wakulima maarifa haya ni fedha
na wakati uletao faida kubwa zaidi kwa nchi yetu kuliko fedha na
wakati mwingi tunaotumia katika mambo mengi tunayoyaita
maendeleo.
Jambo hili kwa kweli tunalifahamu. Katika mpango wetu wa miaka
mitano, mipango inayoendelea vizuri na hata kuzidi makisio ni ile
inayotegemea juhudi ya wananchi wenyewe. Pamba, kahawa,
korosho, tumbaku, pareto ni mazao yaliyoongezeka kwa haraka sana
katika muda wa miaka mitatu iliyopita. Lakini ni mazao ambayo
yameongezeka kwa sababu ya juhudi na uongozi wa wananchi, siyo
kwa sababu ya fedha.
Kadhalika wananchi kwa juhudi zao wenyewe na maelekezo au
msaada kidogo wametimiza mipango mingi sana ya maendeleo huko
vijijini. Wamejenga shule, dispensary, majumba ya maendeleo,
wamechimba visima, mifereji ya maji, mabwawa, mabarabara,
wamejenga mabirika ya kukoshea mifugo na kujiletea wenyewe

maendeleo ya aina mbali mbali. Kama wangengoja fedha
wasingeyapata maendeleo hayo.
JUHUDI NI SHINA LA MAENDELEO
Mipango inayotegemea fedha inakwenda vizuri lakini kuna mingi
ambayo imesimama na yumkini mingine haitatimizwa kwa sababu ya
upungufu wa fedha. Lakini kelele zetu bado ni kelele za fedha.
Juhudi yetu ya kutafuta fedha inazidi kuongezeka! Sio kwamba
tuipunguze, bali, badala ya safari nyingi ndefu na zenye gharama
kubwa za kwenda kutafuta fedha za maendeleo yetu, itafaa kufunga
safari kwenda vijijini kuwafahamisha na kuwaongoza wananchi katika
kujiletea maendeleo kwa juhudi yao wenyewe. Ndiyo njia ya kweli ya
kuleta maendeleo kwa kila mtu.
Hii maana yake si kwamba tangu sasa hatutajali fedha, wala
hatutajenga viwanda au kufanya mipango yo yote ya maendeleo
inayohitaji fedha. Wala siyo kusema kuwa tangu sasa hatutapokea
wala kutafuta fedha kutoka nchi za nje kwa ajili ya maendeleo yetu.
LA, SIVYO. Tutaendelea kutumia fedha; na mwaka hata mwaka
tutatumia fedha nyingi zaidi kwa maendeleo yetu ya aina mbali mbali
kuzidi mwaka uliopita. Kwani hiyo itakuwa ni dalili moja ya
maendeleo yetu.

Lakini hii ni kusema kwamba tangu sasa tutajua nini ni shina na nini
ni tunda la maendeleo yetu. Katika vitu viwili hivyo FEDHA na WATU,
ni dhahiri kwamba watu na JUHUDI yao ndiyo shina la maendeleo,
fedha ni moja ya matunda ya juhudi hiyo.
Tangu sasa tutasimama wima na kutembea kwa miguu yetu badala
ya kupinduka na kuwa miguu juu vichwa chini. Viwanda vitakuja, na
fedha zitakuja, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI yao na
hasa katika KILIMO. Hii ndiyo maana ya kujitegemea. Kwa hiyo
basi, mkazo wetu na uwe:-
(a) Ardhi na Kilimo.
(b) Wananchi.
(c) Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, na
(d) Uongozi bora.
(a) Ardhi:
Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea na utaendelea
kutegemea kilimo na mifugo, Watanzania wanaweza kuyaendesha
maisha yao barabara bila ya kutegemea misaada kutoka nje kwa
matumizi bora ya ardhi hiyo. Ardhi ni ufunguo wa maisha ya
binadamu kwa hiyo Watanzania wote waitumie ardhi kama ni
raslimali yao kwa maendeleo ya baadaye. Kwa kuwa Ardhi ni mali ya
Taifa, Serikali ni lazima iangalie kuwa ardhi inatumiwa kwa faida ya

Taifa zima na wala isitumiwe kwa faida ya mtu binafsi au kwa watu
wachache tu.
Ni wajibu wa TANU kuona kuwa nchi yetu inalima chakula cha
kutosha na kutoa mazao ambayo yataleta fedha nchini kwa kuuzwa
katika nchi za ng’ambo. Ni wajibu wa Serikali na Vyama vya Ushirika
kuona kuwa wananchi wanapatiwa vyombo, mafunzo ya uongozi
unaohitajika katika kilimo na ufugaji wa kisasa.
(b) Watu:
Kuiwezesha siasa ya kujitegemea itekelezwe vizuri, wananchi ni budi
wajengwe moyo na shauku ya kujitegemea. Wajitegemee katika
kuwa na chakula cha kutosha, mavazi ya kufaa na mahali pazuri pa
malazi.
Katika nchi yetu kazi iwe ni kitu cha kujivunia. Bali uvivu, ulevi na
uzururaji uwe ni jambo la aibu kwa kila mwananchi. Katika upande
wa ulinzi wa Taifa, wananchi wawe macho na vibaraka waliomo
nchini ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nje wenye nia
mbaya ya kuliangamiza Taifa hili na wawe tayari kulilinda Taifa
inapolazimika kufanya hivyo.
30
(c) Siasa Safi:
Msingi wa siasa ya kujitegemea lazima uambatane na siasa ya
Ujamaa ya TANU. Ili kuzuia unyonyaji ni lazima kila mtu afanye kazi
na aishi kwa jasho lake yeye mwenyewe. Na ili kuleta usawa wa
kugawana mapato ya nchi ni lazima kila mtu atimize wajibu wake
kwa kufanya kazi kwa bidii zake zote. Asiweko mtu wa kwenda kwa
ndugu yake na kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi kwa sababu
atakuwa anamnyonya yule ndugu yake. Vile vile mtu ye yote
asiruhusiwe kuzurura zurura hovyo mijini au vijijini bila kufanya kazi
ya kumwezesha kujitegemea mwenyewe bila kuwanyonya ndugu
zake.
TANU inaamini kuwa kila anayelipenda Taifa lake ni budi aweze
kulitumikia kwa kujitolea nafsi yake na kushirikiana na wananchi
wenzake kwa kuijenga nchi kwa manufaa ya watu wote. Ili
kudumisha Uhuru wa nchi yetu na raia zake barabara ni budi
kujitegemea kwa kila hali bila kwenda kuomba misaada nchi zingine.
Kujitegemea kwa mtu mmoja ni kujitegemea kwa nyumba kumi.
Kujitegemea kwa nyumba zote kumi za balozi ni kujitegemea kwa
tawi zima. Kujitegemea kwa matawi ni kujitegemea kwa Wilaya
ambayo ni kujitegemea kwa Mkoa. Kujitegemea kwa Mikoa yote ni
kujitegemea kwa Taifa lote ambalo ndilo lengo letu.

(d) Uongozi Bora:
TANU inatambua umuhimu wa kuwa na Uongozi Bora. Tatizo lililopo
ni ukosefu wa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi na kwa
hiyo Ofisi Kuu ya TANU ni budi itengeneze utaratibu maalum kuhusu
mafundisho ya Viongozi tangu wa Taifa zima hadi Mabalozi ili
waielewe siasa yetu na mipango ya uchumi. Viongozi ni lazima wawe
mfano mzuri kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia.

SEHEMU YA NNE
UANACHAMA
Tangu Chama kilipoanzishwa, tumethamini sana kuwa na
wanachama wengi iwezekanavyo. Hii ilifaa wakati wa kupigania vita
vya kumng’oa mkoloni. Hivyo ndivyo ilivyobidi TANU kufanya kwa
wakati huo. Lakini sasa Halmashauri Kuu inaona kuwa wakati
umefika wa kutilia mkazo kwenye imani ya Chama chetu na siasa
yake ya Ujamaa.
Kifungu cha Katiba ya TANU kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye
Chama kinachohusu uingizaji wa mtu kwenye Chama kifuatwe na
ikiwa inaonekana kuwa mtu haelekei kuwa anakubali imani,
madhumuni na sheria na amri za Chama, basi asikubaliwe kuingia.
Na hasa isisahauliwe kuwa TANU ni Chama cha wakulima na
wafanyakazi.

SEHEMU YA TANO
AZIMIO LA ARUSHA
Kwa hiyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana katika
Community Centre ya Arusha kuanzia tarehe 26/1/67 mpaka
29/1/67, inaazimia ifuatavyo:-
A. VIONGOZI
1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au
mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au
kikabaila.
2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.
4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi
5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
6. Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama
vilivyoshirikishwa na TANU, Wakuu wa Mashirika ya
34
Kiserikali. Viongozi kutokana na kifungu cho chote cha
Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye
vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki
kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).
B. SERIKALI NA VYOMBO VINGINE
1. Inaipongeza Serikali kwa hatua zote ilizokwisha chukua
mpaka hivi sasa katika kutimiza siasa ya Ujamaa.
2. Inaihimiza Serikali, bila kungojea Tume ya Ujamaa, ichukue
hatua zaidi za kutimiza siasa yetu ya Ujamaa kama
ilivyoelezwa katika Tamko la TANU juu ya Ujamaa.
3. Inahimiza Serikali kutengeneza mipango yake kwa
kutegemea uwezo wa nchi hii kuiendesha mipango hiyo na
wala isitegemee mno mikopo na misaada ya nchi za
ng’ambo kama ilivyofanya katika mpango wa maendeleo ya
miaka mitano. Halmashauri Kuu ya Taifa inaazimia mpango
huo urekebishwe ili ulingane na siasa ya kujitegemea.
4. Serikali ione kuwa mapato ya wafanyakazi nje ya Serikali
hayapitani mno na yale ya wafanya kazi Serikalini.
5. Serikali itilie mkazo sana njia za kuinua maisha ya wakulima.

6. Inahimiza NUTA, Vyama vya Ushirika, TAPA, UWT, TYL.,
mashirika yote ya Serikali, kuchukua hatua ili kutekeleza
siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
C. UANACHAMA
Wanachama wafundishwe kwa ukamilifu imani ya TANU ili
waielewe, na wakumbushwe wakati wote umuhimu wa kuishika
imani hiyo.
 
Azimio la Arusha liliweka misingi imara sana katika Taifa.Lilileta usawa,lilipiga vita kila aina ya ufisadi,lilisisitiza UZALENDO na uwajibikaji miongoni mwa Watanzania.Kwa nchi changa na masikini kama yetu lingetufaa sana na kwa kweli lingeisogeza mbele nchi.Lakini MAFISI yenye uchu binafsi yaliona kama linahatarisha SHIBE yao!Yakaamua kutumia hila yakalizika kimyakimya pale Zanzibar.Laana yake haitawaacha milele.
 
Back
Top Bottom