La Mgambo Kwa Vijana Wote wa BAVICHA na Mashabiki wao

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Enyi vijana wangu wa BAVICHA!

Poleni sana na hongereni kwa kazi nzuri mlofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mlidharauliwa sana na kubezwa kwa kuitwa kwamba nyie ni wanywa viroba msiojua mbele, nyuma au pembeni. Hasa hapa JF ikiletwa thread yenye kukosoa upande wa pili wachangiaji wanaokunywa maji ya kijani huchangia kwa kusema "mawazo ya kibavicha hayo" au "viroba vya bavicha hivyo"

Lakini hao wanywa maji ya kijani, kwa kupoteza ufahamu wao kama ilivyo kawaida yao hawakufahamu hata kidogo kwamba ninyi ni jeshi kubwa la wapiga kura lenye uwezo wa kubadili serikali ya nchi hii.Wao wamebaki kusema wanywa viroba hao.Lililotokea kwenye chaguzi za serikali za mitaa limewapa kizunguzungu kiasi hawalikumbuki neno 'viroba' tena.

Wanalolifahamu ni 'tutaangalia tulipojikwaa ili tujisahihishe' Hawajui kuwa walianza kujikwaa tangu hilo kundi lilipozaliwa 1977.

Sasa vijana wangu wapendwa nawaomba hivi:msisahau kujiandikisha kwenye uboreshaji wa daftari la wapiga kura katika sehemu unayoishi, ili mwakani 2015 uwe na kibali cha kuwachinjia mbali hii mijitu inayoita wenzao 'wanywa viroba'

Ni hayo tu kwa leo vijana wangu, sina mengi.
 
Ni kweli kabisa wenyeviti wa mitaa wanaowakilisha wawe mstari wa mbele kukagua mitaa yao na kuhakikisha wanawauliza bila ya kuwa na ganzi wakazi wao ,Je umejiandikisha ? Hili ni suali ambalo sasa linatakiwa lipewe kipau mbele ,mbali ya viongozi wakuu kuonekana wakiwahimiza wananchi katika majukwaa ya mikutano kuhusu kujiandikisha ,sasa iwe ni kazi ya kila raia nyumba kwa nyumba kushawishiana ili wwale wenye umri ya kujiandikisha wakajiandikishe na kuhakikisha kila kitu chao kipo uptodate hadi siku ya kupiga kura ,lengo ni moja tu kumuangusha Adui CCM.
 
Kamanda hii kazi yetu wrote kila mahali tulipo tuwaelimishe wakituelewa tuwambie wawaelimishe na wengine
 
Ni kweli kabisa wenyeviti wa mitaa wanaowakilisha wawe mstari wa mbele kukagua mitaa yao na kuhakikisha wanawauliza bila ya kuwa na ganzi wakazi wao ,Je umejiandikisha ? Hili ni suali ambalo sasa linatakiwa lipewe kipau mbele ,mbali ya viongozi wakuu kuonekana wakiwahimiza wananchi katika majukwaa ya mikutano kuhusu kujiandikisha ,sasa iwe ni kazi ya kila raia nyumba kwa nyumba kushawishiana ili wwale wenye umri ya kujiandikisha wakajiandikishe na kuhakikisha kila kitu chao kipo uptodate hadi siku ya kupiga kura ,lengo ni moja tu kumuangusha Adui CCM.
Yote kweli tupu kamanda wangu!
 
MSALANI na washirika wake walinipa hasira sana comments zao za kijinga jinga
_nikaingia mtaani na kwenye vijiwe vya kahawa kuhamasisha watu,kweli walinielewa na sasa ni muda wakuwapa shukrani
 
Last edited by a moderator:
Saizi vijana wetu sana lugha moja, magamva watakoma lazima wawe wapinzani, UKAWA ndo habari ya mjini,
 
Back
Top Bottom