LA DOWANS: Sitta afungwa mdomo; Ikulu yakanusha!

acheni wawalipe dowans, ili serikali ya ccm ijimalize, wanazani mpaka 2015 tutakuwa tumesahau kuwa 2011 waliwalipa dowans? Wale wazee wa afrika mashariki nao waanze kudai kwa nguvu haki yao
haaaaaaaah.. sasa mwaka 2015 mbona mbali saaaan.
mission yenu ya kuhakikisha jamaa anaondoka kabla ya 2015 mmeisahau????
mbona hamueleweki au mnazuga???
 
Tatizo ni haya mambo kufanywa kwa siri, Kuanzia wakati wa uendeshaji wa kesi mpaka hukumu inatolewa
Kwa kuwa serikali inataka kulipa kwa kutumia pesa za umma ingetuelewesha walipa kodi kwa nini tulishindwa kwenye hiyo kesi licha ya kwamba uvunjaji wa mkataba ulizingatia matakwa yote ya kisheria. Wanasheria wa Tanesco, AG, na Rex Attorney hawakuona hilo tatizo?
 
Narudia kusema, sasa hivi kwa lugha mbaya zaidi;

It goes on and on!

Meremeta, Richmond, EPA, Dowans.......tutaendelea kubakwa mpaka lini? Napata hasira sana tunaporudi pale pale!!

Mkuu umesahau TRL & RITES ya India (21bn)! Bado MADINI.
 
Waache wabaki huko huko,wawape shida wenzao hadi kieleweke,na tupate taarifa za vikao vya baraza la mawaziri.
Sitta na Mwakyembe si watu wa kufunga mdomo,hawakupinga uamuzi wa ICC na Ngeleja bila kujua consequence za matendo yao,they have guts to do what other ministers can not do.:frusty:

Pamoja na kuwa tungependa kupata taarifa za Cabinet, kimaadili na sheria hawaruhusiwi kutoa siri zake. Na hilo wamelitamka wazi katika viapo vyao.
 
Ushauri wangu kwa Sitta na mwakyembe:
Kupitia bunge lililopita na kauli zenu huvi karibuni kwenye vyombo vya habari mmeudhihirishia umma kwamba mna uchungu na nchi hii. Wananchi wanajivunia kuwa na watu wa aina yenu. Ili kulinda heshima yenu mbele ya jamii na kuandika historia katika nchi yetu, nawaomba mjiuzuru na kujitenga na serikali dharimu dhidi ya wapiga kura wake. Nawahakikishia mkifanya hivyo, yatafanyika maandamano nchi nzima kuwaunga mkono. Kazi kwenu.

Kweli kabisa ndugu yangu
 
Mkuu umesahau TRL & RITES ya India (21bn)! Bado MADINI.

Tatizo la kubakwa unasahau umebakwa mara ngapi na nani aliyekubaka! Afadhali umeongeza kamanda! Hii nchi imeshaibiwa mpaka basi! Imekuwa kama vile haina mwenyewe ila naamini kwamba kama viongozi tutasimamia haki itendeke. Hatuwezi kukaa pembeni na kuacha hii hali iendelee
 
tatizo alilonalo Sita ni kwamba anaona akijiuzulu uwaziri na ikiwa atafukuzwa CCM, atakosa mahali pa kukimbilia maana huko CHADEMA alikuwa anamponda Dr. Slaa na sera za CHEDEMA hadi kuitisha mdahalo akidai kuwa Dr. Slaa ni saizi yake. Halafu akiwa bungeni aliuzima mjadala wa Richmond na Dowans bila wabunge kuafiki. Maana yake siasa za Sita ni za ndumila kuwili. KWA HIYO HAWEZI KUJIUZULU.

Nasema hivi, wahalifu wote walioiibia nchi hii kuanzia awamu ya TATU hadi ya NNE dawa yao iko jikoni na watahukumiwa kwa kutumia Katiba Mpya ambayo italeta viongozi makini mwaka 2015 wenye kufuata utawala bora na wa kisheria. Sio lazima tuendelee kuwataka Sta na Mwakyembe kujiuzulu. Kwani wao ni watoto wadogo hadi waambiwe la kufanya?
 
Sitta na/au Mwakyembe (w)akikubali kufungwa mdomo na Kiiwete ni kwa sababu kwa ridhaa yao wameamua kukubali na sio kuwa wamelazimishwa. Mtu unatakiwa na msimamo na maadili. Tena ukiwa kiongozi wa umma unatakiwa pamoja na hayo uwe na ufhamu, ujasiri na hekima. Wakikubali kufungwa midomo au kudhalilishwa na hilo genge la wahuni chini ya Kikwete, nasema ni wao wenyewe wa kulaumiwa.

Kisheria au kikanuni lazima wajiondoe toka gengeni kama wanataka kubaki na heshima na moral obligations juu ya malipo ya Dowans na ufisadi. They have a decision to make, and urgently.
 
6 na mwakyembe huo ni usanii, kwanini msijiuzuru kama mnaona ukweli? CCM mnatuzika watanzania
 
"Jaji Werema amekaririwa akimweleza Waziri Sitta kwamba iwapo kweli alikuwa ana uchungu na suala la Dowans, basi wakati kesi ikiendelea alipaswa kuisaidia serikali katika kuwasilisha utetezi dhidi ya malalamiko 17 yaliyokuwa yamewasilishwa na kampuni hiyo.

Habari zinaeleza kwamba hatua ya Sitta ambaye alikuwa akitambua fika namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendelea kutochangia jambo lolote wakati shauri hilo likiwa ICC na badala yake kusubiri hadi serikali ishindwe ndipo aanze kutoa matamshi katika vyombo vya habari ilikuwa ni ya kuchochea hasira za wananchi dhidi ya viongozi pasipo sababu zozote"

LAKINI PIA NI SITA HUYO HUYO AKIWA KAMA SPIKA ALIISHAURI SERIKALI KUVUNJA MKATABA NA DOWANS ZIKIWA ZIMEBAKIA SIKU 90 KABLA YA MKATABA KUISHA HUKU AKIJUA MKATABA HUO NI WA KIMATAIFA NA KULIKUWA NA UWEZEKANO WA UPANDE WA PILI KUISHITAKI SERIKALI. HIVYO SITA KAMA MWANASHERIA NA MWENYE UZOEFU SERIKALINI ALIPASWA SI TU KUSHIRIKI KATIKA KUINUSURU SERIKALI KULIPA GHARAMA KUBWA WAKATI WA KESI BALI KUTOA ANGALIZO KABLA YA MKATABA KUVUNJWA.

HUYO NDIYE MH. SANA _SIX.
 
tatizo alilonalo Sita ni kwamba anaona akijiuzulu uwaziri na ikiwa atafukuzwa CCM, atakosa mahali pa kukimbilia maana huko CHADEMA alikuwa anamponda Dr. Slaa na sera za CHEDEMA hadi kuitisha mdahalo akidai kuwa Dr. Slaa ni saizi yake.

wewe Dr. Slaa si kitu ndani ya CDM, ni kama kondom tu inayotumiwa na wenye chama( akina mzee Mtei) wakimaliza kumtumia watamtupa tu kama wanavyofanya kwa Zitto leo(ila dogo kiburi hawamuwezi)
 
thubut wanafiki tu hao, eti wajiuzulu?

Njaa, na vyeo wamwachie nani?

Nasubiri kwa hamu tujaze nafasi hizo wako wengi kwenye list yetu wanasubiri kupewa ok/
 
wewe Dr. Slaa si kitu ndani ya CDM, ni kama kondom tu inayotumiwa na wenye chama( akina mzee Mtei) wakimaliza kumtumia watamtupa tu kama wanavyofanya kwa Zitto leo(ila dogo kiburi hawamuwezi)

Hujisikii vibaya ukisoma michango mingine kuhusu kinachozungumzwa? Huoni umuhimu wa wewe kuchangia angalau kusaidia suluhu ipatikane? Kama CDM ni ya Mtei na Dr Slaa sio kitu at least Tanzania ni yetu wote basi tuijenge na kuitetea!
 
Hujisikii vibaya ukisoma michango mingine kuhusu kinachozungumzwa? Huoni umuhimu wa wewe kuchangia angalau kusaidia suluhu ipatikane? Kama CDM ni ya Mtei na Dr Slaa sio kitu at least Tanzania ni yetu wote basi tuijenge na kuitetea!

na wewe nakuheshimu usinitibue, huoni nilikuwa na respond jamaa aliposema kinachomzuia sitta kwenda CDM ni Slaa au unataka tu kunitafutia ban mapema hii? hivi kwa akili zako tunaweza kujenga CDM kwa michango ya hapa JF? humu ni ushabiki tu, hata kwenye uozo wewe sifia tu halafu nenda kafanye shughuli zako au kama mtaani kwako lipo tawi la CDM nenda hapo kajenge chama chako hapa si mahala muafaka.
 
narudia kusema, sasa hivi kwa lugha mbaya zaidi;

mtu unabakwa unakaa kimya, ubaki kutoa machozi. Unaogopa kupiga kelele eti watu watajua umebakwa utakosa mume au hutachangiwa harusi!! Unatelekeza utu wako kwa sababu ya woga.

Mbaya zaidi unavyozidi kubakwa (kwa sababu mbakaji ameshaja huwezi kupiga kelele wala kuzuia kubakwa) unaanza kumpa ushirikiano. Unachezesha kiuno kidogo mara unakumbuka unabakwa unaanza kulia kwa sauti ya chini halafu unanyamaza! Hali hiyo inaendelea, inakuwa kawaida! Ipo siku utajikuta mjamzito. Mbakaji atakimbia maana hana muda wa kulelea mtoto! Unabaki na uchungu zaidi, umepoteza utu, umeachiwa mtoto ambaye hukumtaka, huna uwezo wa kumlea! Unajiuza zaidi! Sasa unaamua acha iwe mbaya, nitafanya biashara!! It goes on and on!

Meremeta, richmond, epa, dowans.......tutaendelea kubakwa mpaka lini? Napata hasira sana tunaporudi pale pale!!

Sitta na mwakyembe ni wafanyakazi wa ndani wa anayetubaka, wanatuhurumia lakini wao ndio wanatumwa ky jelly. Wao ndio wanafunga madirisha na kufungua radio kwa sauti ya juu zaidi. Tukishabakwa wanatusomea neno na kutupa pole. Wanatupa panadol kesho tena zoezi linaendelea. Sisi tunawaona mashujaa. Wanatufariji, wanatupa panadol!! Tunafurahi na kuwapenda kwa sababu wanatumwa ky inatupunguzia maumivu lakini inatusaidia kubakwa kwa urahisi zaidi!!

Nimechoka na mifano inayoonekana na adabu na heshima. Labda lugha hii itaelezea ukubwa wa tatizo letu!
kwa mara ya kwanza leo naona somo la unafiki wa akina sitta linaelekea kukubalika humu ndani mifano yako ni bomba ,wala hakuna lugha mbaya ,kuna siku niliandika kwa nn tunawashangilia sana sitta na mwakyembe ilhali ni waoga nilikepewa majina ya kejeli ila kuna siku ukweli uatajulikana na ataonekana nani ni great thinker .!jana niliandika kuwa sita toka humo ndani ya shimo lenye maji ya kinyesi,tutaamin vipi usafi wako,kwa kupiga kelel kuwa hayo maji yana kinyesi ili hali uwezo wa kutoka unao ,historia itakuhukumu baba,mbona wanyamwezi tu wajasiri wewe ni mfipa nn!/
 
Utawala wa jakaya kikwete umepimwa na kuonekana umepungua na sasa utaondolewa kwa nguvu za ummma!!!
Kama kikwete amefikia kumwambia sitta na mwakyembe wasiongelee dowans nje ya bunge katika kikao cha bunge , namushauli ajihoji ni kwa nini kikao hicho kimefanyika kwa siri ikulu , lakini bado siri hizo zimevuja???

Bila shaka , wapo mawaziri wengi hawamtaki , na wapo wabunge wengi hawamtaki na tena wapo uvccm wengi hawamtaki na kwa hili analo moja tu kuhakikisha anatubu haraka na kuomba mungu amusamehe !!!!

Siku zaja ambazo watu waoga watapata ujasiri wa kutenga sawasawa na haki ili kuokoa taifa hili na wizi , ufisadi, na kiburi!!!
 
Kikao cha baraza la mawaziri ni siri na kimefanyika ikulu, kwa ulinzi mkali lakini siri za kikao chote zipo kweye gazeti la tanzania daima!!!!

Kutokana na makala ya absoloni kibanda , ya leo ,kikwete anatakiwa kuwafukuza kazi mawaziri wote waliovujisha siri za kikao hicho!!!
 
Back
Top Bottom