Kwenu watetezi wa ndoa

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,434
9,863
Mmekua na kasumba wa kutushambulia ambao hatutaki ndoa lakini insasikitisha sana mashambulizi yenu huwa hamlengi kwenye point mahususi. Utetezi wenu huwa unalenga zaidi kwenye dhiaka mfano kataa ndoa ni mashoga, hawana hela, wamelelewa na single parent, wana trauma n.k lakini kwenye point huwa hampagusi.

Naomba tuelewane, hatukatai mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanaume na mwanamke, hatukatai malezi mema ya watoto chini ya uangalizi wa baba na mama kwa maana hayo yote yanaweza kufanyika bila ndoa. Vile vile hatuungi mkono wanaume wanaotelekeza watoto wao. Tunachokataa ni ule mkataba wa kitapeli uliopewa jina la "ndoa"

Tunachokataa ni huu mkataba wa kitapeli ambao mwanamke kapewa uhalali wa kuchukua mkopo kwa jina la mumewe na mumewe ndio atawajibika kuulipa hata kama hajanufaika nao kwa lolote na wala hakushirikishwa.

Tunachokataa ni huu mkataba wa kitapeli ambao endapo mwanamke akikengeuka na mwanaume ukachoka visa ukaamua muachane basi ni mwanaume ndio utatakiwa kuondoka kwenye nyumba uliojenga na kumuacha mwanamke ambae hajachangia hata tofali moja.

Tunachokataa ni huu mkataba wa kitapeli ambao wanandoa mkiachana mwanamke anapewa mgao wa mali ambazo hana mchango wa kifedha wala kitaaluma.

Tunachokataa ni huu mkataba unaombebesha mwanaume jukumu la kumuhudumia mwanamke hata kama uyo mwanamke ana kazi au akili timamu na nguvu za kuweza kufanya kazi na kujihudumia mwenyewe.

Kwa kawaida sheria inatakiwa kuziba mianya ya mtu kufanya upigaji lakini sheria ya ndoa imempa mwanamke mwanya mkubwa sana wa kufanya utapeli. Suala la mwanamke kukupiga kupitia ndoa ni maamuzi yake tu na akiamua kukupiga analindwa na sheria, sheria haitakiwi kuwa ivyo.

Kuacha sheria hii iendelee kutumika kwa wanawake matapeli wa mapenzi wa kizazi hiki ni kumvalisha mwanaume bomu ambalo litamlipukia muda wowote.

Kuna masuala kama mmong'onyoko wa maadili, tamaa ya luxury life style, athari hasi za utandawazi na kupumbazwa na itikadi ya feminism pia yanachangia kualibu akili za wanawake ivyo kupelekea vijana wa kiume kusita kuingia kwenye ndoa lakini dawa ya haya ni kuachana tu mkeo ila hili suala la kugawana mali linaumiza sana sio kwa mwanaume tu hata ndugu wa mwanaume pia.

Sheria ya ndoa ilitungwa kipindi ambacho mwanamke alikua inferior sana kwenye jamii ndio maana ipo katika mlengo wa kumlinda mwanamke. Kwa sasa tupo kwenye zama za 50/50 kwaiyo mwanamke anatakiwa kuondolewa izo kinga alizowekea kipindi cha mfumo dume ili linapokuja suala la mgogoro wa kijinsia/mahusiano kila jinsia iwe na uwanja sawa wa kutendewa haki.
 
jifunze kufupisha
mambo ni mengi muda ni mchache
 
Naona kama umechanganya mambo hapo
1. Kukataa ndoa
2. Kuikataa sheria ya ndoa.
Ila nimeona unakataa ndoa lakini hukatai familia,hukatai watoto kulelewa na baba na mama.
Zaidi ungezungumzia hiyo sheria uliyosema ni kandamizi na ingekua bora ukatoa mapendekezo .
Mfano ungesema kama wanandoa waliochuma wote wakiacjana kama ninyumba wapewe watoto yatima na mashamba serikali za vijiji,miji na majiji vitwae ardhi yake( huo nimfano nisije nikashambuliwa?
 
Wazungu waliona waafrika tunafaidi ndoa zetu

Wakatuletea 50/50 ambayo hata wao inawaendesha sana

Mwanamke kumlinganisha na mwanaume ni kumpinga Mungu
 
Naona kama umechanganya mambo hapo
1. Kukataa ndoa
2. Kuikataa sheria ya ndoa.
Ila nimeona unakataa ndoa lakini hukatai familia,hukatai watoto kulelewa na baba na mama.
Zaidi ungezungumzia hiyo sheria uliyosema ni kandamizi na ingekua bora ukatoa mapendekezo .
Mfano ungesema kama wanandoa waliochuma wote wakiacjana kama ninyumba wapewe watoto yatima na mashamba serikali za vijiji,miji na majiji vitwae ardhi yake( huo nimfano nisije nikashambuliwa?
jamaa anacholalamikia ni kwa nini sheria inamtetea mwanamke peke yake?

Sheria ya ndoa haina usawa kama walileta usawa wa 50/50 basi na sheria itetee wote

Sheria inawatetea wanawake tu
 
Naona kama umechanganya mambo hapo
1. Kukataa ndoa
2. Kuikataa sheria ya ndoa.
Ila nimeona unakataa ndoa lakini hukatai familia,hukatai watoto kulelewa na baba na mama.
Zaidi ungezungumzia hiyo sheria uliyosema ni kandamizi na ingekua bora ukatoa mapendekezo .
Mfano ungesema kama wanandoa waliochuma wote wakiacjana kama ninyumba wapewe watoto yatima na mashamba serikali za vijiji,miji na majiji vitwae ardhi yake( huo nimfano nisije nikashambuliwa?
Ukishasema ndoa tayari iyo ni sheria mzee baba, ukitoa ule mkataba mnaosaini basi mapenzi yenu yanabaki kuwa mahusiano ya kawaida tu ya boyfriend na girlfriend. Kabla hatujaletewa hizi sheria wazee wetu walioa lakini hawakufunga ndoa. Hatukatai mahusiano ya kimapenzi tunakikataa ni ndoa.
 
Hivi hii topic haiwachoshi jamani. Kila mtu afanye lake..kama unaoa oa, kama unaolewa olewa. Kama unaacha acha. Kama unabak single baki...mambo ni mengi wazee...
izo ni indicator za kutokujiamini wew kama umeau kutoa oa kaa kimya shida watu wanatafta attention zisizo na Msingi kina John cena wameau kuto oa kabisa na hawipi pigi kelele
 
Hivi hii topic haiwachoshi jamani. Kila mtu afanye lake..kama unaoa oa, kama unaolewa olewa. Kama unaacha acha. Kama unabak single baki...mambo ni mengi wazee...
Nafikiri hili ni jukwaa huru kila mtu anaweza kupost anachotaka na uhuru wa kusoma anachotaka ilmradi havunji sheria za jf. Ukiona topic inakuchosha ni suala la ku-skip tu
 
Dada angu mbona kama umepaniki vile
Nimepaniki kusema ukweli????

Sasa bro umetafuta hela kwa jasho, umejipata umejenga una biashara.....linakuja tu janamke from no where unalioa na kutumia mali zako hii sio sawa.

Kataa ndoa, au???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom