Kwenu bodi na viwanda ya Kahawa, chai,Cocoa

CORONAZ

Senior Member
Apr 26, 2020
181
337
Kama kuna zao lenye "ZERO" marketing strategy ni zao la kahawa. Huwezi hata kujua upo kwenye nchi au mkoa unaolima kahawa. Unywaji uko chini sana na bei ziko juu.

Hakuna msukumo wa kuitambulisha na kuongeza unwaji wa Kahawa hata kwenye maeneo ya utalii.
1. Hebu angalia miji yetu, kama hunywi pombe au soda basi ni maji yamebaki. Coffee shops ni za kutafuta. Kahawa chache iliyopo mahotelini ni ile ya hali ya chini kabisa.
2. Hakuna elimu jinsi ya kutengeneza kahawa bora. Hawa vijana wa "kigoma" wanaotembeza kahawa, hawaonekani kama fursa ya mafunzo ili watengeneze na kuuza kahawa bora?
3. Mashine ya kuandaa kahawa bora zinauzwa ghali na hazipatikani kiurahisi nchini. Wahusika wamelala fofofo.
4. Angalia mabasi, malori na magari madogo yanasafiri usiku sasa. Je njia zooote, wapi umeona coffee shop au hoteli inayotengeneza kahawa safi usiku? Hakuna.
5. Hizi taasisi zina maafisa masoko kweli? Wanatangaza wapi? Hakuna hata madhindano ya uandaaji wa kahawa bora? Au mafunzo kwa wanaotaka kuingia kwenye hii biashara?
6. Na ninyi TBS, Hizo tea bags ambazo zikichanika unashindwa kunywa hiyo chai kwa kuwa inachafuliwa na kilichomo ndani ya tea bag. Hamuoni tunavyofungashiwa na kuuziwa vumbi hilo?
Hiyo kahawa ya pakti na makopo ambayo ni chunguuu, hamuzijui? Mbona hakuna nchi nyingine yenye haya makapi?
7. Cocoa ndo kabisaaaa...na tunalima na tunauza...
Bodi za mazao sizielewi.....kabisaaa......
 
Back
Top Bottom