Kweli wabongo majiniazi!!!!!!!

Bundewe

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
400
141

Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi? Fikiri, matumizi nyumbani: chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni.

Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu. Matibabu hospitalini, pesa ya walinzi kwa mwezi, sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya; Zaka ya kanisani na misikitini, Kupanda Mbegu/ Sadaka, Shukurani ya Neno, Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzitupa hapo hapo), Madalali wa nyumba/viwanja, Pango la nyumba, Fremu ya biashara/ofisi, Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers];

Mafuta ya gari Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa); Tozo za kuegesha magari, Makato ya Mikopo, Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf. Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu, Harusi ya ndugu yako waa ukoo na zawadi, Sendoff ya mtoto wa mdogo wake rafiki yako na zawadi, Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi,

Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara; Michango ya besdei party na zawadi; Ndugu wa kule kijijini, Mshahara wa Hausigeli na hausiboi; Bodaboda, teksi na bajaj; Duka la dawa, Tuisheni ya mtoto, Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko. Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa, Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu.

Chakula cha mbwa, Mchango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa, Kuchangia Uinjilisti Masasi, outing ya kitimoto, Ujenzi wa Nyumba Mabwepande, Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa).

Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi. Maji ya Traffik, Chai ya Nesi na Daktari, Kahawa ya Hakimu, Karani na PP. Vishoka waunganisha maji na umeme; Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa. Hivi hali inakuwaje? Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba, kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni.

umeme uliopanda bei, gesi iliyopanda bei, maji yaliyoadimika, bado contingency mana huu usafiri unaotembelea ball joint, bush, feni belt havijafa - hapo bado service.

Bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana na bei za restaurants, bado mchango wa kitchen pati na sare, baby shower.

Na hapo bado hujatoa watoto outing jumapili , upatu, mchango wa wawata, saluni, ukiangalia hapo hujanunua nguo wala kiatu kipya...kina sie mara dada aseme pampers zimeisha.n.k
Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%. Ndipo unapoimba "Mwokozi nitoe roho niepuke na hili balaaa"

Ukifikiria kwa makini unajiuliza watanzania wana-survive vipi kwa style hii???


Kweli wabongo ni majiniazi!!!!!
 
Dah, hata mi nashangaa kumbe nalipaga vitu vingi hivi? Kiukweli kuna kitu huwa nafanya, haiwezekani kwa mshahara huu.
 
Dah Ndio maana ikifika mwisho wa mwezi nakuwa sina kitu, kuweka akiba ya maana inakuwa ishuuuuu
 
Back
Top Bottom