Kweli Tanzania ni nchi ya ajabu... Hata ukikacha mdahalo bado unaweza kuukwaa Urais!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Mpaka leo bado ninajiuliza kwa nini kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 Kikwete alikacha mdahalo, kwanini CCM iliwazuia wagombea wake kushiriki midahalo na kwa vipi hali hii iliweza kukubalika ndani ya jamii iliyostaarabika.

Tume ye Uchaguzi ikiongozwa na Jaji Mstaafu ilikaa kimya, Ofisi ya Msajili wa vyama ikisimamiwa na Jaji mstaafu ilikaa kimya na taasisi mbali mbali zinazotetea utawala wa kidemokrasia nchini zilikaa kimya.

Lakini kubwa zaidi ni vipi mtu ambaye hakukubali kuhojiwa na waajiri wake (wananchi) kujua kama ana sifa, sababu na uwezo aliweza kupata hiyo ajira. Wana jamvi, naomba hili swali tulijadili bila jazba, kwa nini midahalo inayowapa wananchi fursa ya kuwasikiliza wagombea na kuwauliza maswali, hasa katika hadhi kama ya Uraisi, haikufanyika mwaka 2010?

Kwanini chama tawala kilihakikisha midahalo haifanyiki?
 
walizui baada ya kuona wanazidiwa hoja na wapinzani! Tanzania ukiwa na Pesa nirahisi kushinda hata usipofanya hivyo! WATU WANASHINDA KWA RUSHWA! katika uhalisia ukisema washindane kwa hoja! MABWEPANDE watashindwa vibaya!
 
Najaribu kufikiria hali itakavyokuwa kwa mfano nchini Marekani kama mgombea mojawapo anakacha mdahalo, nadhani ni jambo lisilo hata kufikirika kwani itakuwa ni sawa na kujiondoa kwenye kinyang'anyiro. Wapiga kura wanataka wawasikie wagombea wote wakijieleza na kujibu maswali ili waweze kuamua ni yupi anafaa...hapo ukikosea stepu tu umeanguka.
 
mkuu usilinganishe siasa za USA na za hapa BONGO! hapa ukiwanapesa yakuhonga wapiga kula huko vijijini unashinda! labda kama CHADEMA watafanikiwa kwa 90% kufikisha elimu ya uraia na haki zao! watashinda la sivyo hakuna kitu! kwanza ishu ya watuhumiwa wa UFISADI kuruhusiwa kuwa viongozi wa juu wa CCM kwa siasa za kama USA ilikuwa kashifa yakufanya chama kishindwe vibaya! lakini hapa kwetu hao ndio watakuwa viongozi wetu 2015/2020!
 
Mchakato majimboni ulimuudhi sana mkuu wa kaya maana ulikuwa unamuumbua yeye na chama chake ndiyo maana baada ya "ushindi"wake alimtupilia mbali Tido wa Mhando.Kwa kifupi hawakuwa na jipya na hawana jipya,ila walijiamini kuwa watashinda hata kama wasingeshiriki mdahalo maana Tume ya uchaguzi iko mikononi mwao hivyo kuweza kupika matokeo.Halafu nadhani vilevile suala la mdahalo katika nchi yetu, bado watu wengi wanaona siyo sehemu ya kutathimini mwajiriwa wetu(Rais), ila bado wengi wanaamini kuwa kuzunguka nchi nzima na kufanya kampeni ndiyo sehemu ya kufanya tathimini.
 
Mkuu Mag3 hili la mdahalo ni lazima liwekwe kwenye katiba mpya, vinginevyo magamba wataingia tena mitini 2015 kwa sababu wanajua hawana hoja kutokana na madudu mbali mbali yaliyofanyika katika awamu 6 zilizopita na hawakuweza kufanya lolote lile kuyasafisha madudu hayo yaliyofanywa na Serikali za magamba.

Najaribu kufikiria hali itakavyokuwa kwa mfano nchini Marekani kama mgombea mojawapo anakacha mdahalo, nadhani ni jambo lisilo hata kufikirika kwani itakuwa ni sawa na kujiondoa kwenye kinyang'anyiro. Wapiga kura wanataka wawasikie wagombea wote wakijieleza na kujibu maswali ili waweze kuamua ni yupi anafaa...hapo ukikosea stepu tu umeanguka.
 
Last edited by a moderator:
Its obvious hawakuwa na cha kujadili! Ahadi zinafika mahali zinaisha. Na ukumbuke kwenye mdahalo n maswali na majibu, period. Hakuna taarab. Ni suala kwa hoja. The big point is, sio lazima washinde kwa hoja wala kuchaguliwa na wananchi ili kuwepo madarakani.
 
Pale kichwani hamna kitu!Angewezaje kujibu hoja wakati anajijua mweupe???Hata darasani wanafunzi vilaza huogopa maswali sasa kile kiazi si kinge umbuka tu pale kwa kuzomewa!
 
Hakuna kiongozi wa ccm mwenye uwezo wa kukubali maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wananchi. Wamezoea kuandaliwa maswali na majibu yake. NATOA CHANGAMOTO, KAMA KWELI KUNA KIONGOZI WA CCM MWENYE UWEZO WA KUHUDHURIA MDAHALO LIVE NA WANANCHI, AJITOKEZE. Sababu ni kwamba hiki chama kimejaa DHAMBI kuliko mema, ndio maana viongozi wake wameamua kuwa wababe tuu. Watanzania tukiongeza uelewa wetu wa mambo, ccm hawana pa kupitia.
 
wangeshindwa vibaya sana kama wange kubali midahalo hiyo..

tume zote zinaongozwa na wastaafu. Unategemea kibarua chao kikisitishwa watakula nini? Mpaka tutakapobadili huu utaratibu wa kuwapa watu walioishiwa sera kuongoza idara zetu ndo tutafanikiwa. Hawa watu lazima wakae benchi na kuwa mawakili wa kujitegemea ili damu changa zifanye kazi wao wakishuhudia nchi inavyoendelea.
 
CCM hawakuwa na option nyingine zaidi ya kukwepa mdahalo ili kukwepa aibu ya wazi kwa candidate wao, na watu kama jaji mkuu,msajili wa vyama na kadhalika wasingeweza kuchukua hatua yoyote kwa bosi wao.
 
Hana huwezo wa kujenga hoja kabisa ndio maana alikimbia na kipengele cha mdahalo kingekuwa cha lazima, hakika angejiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Woga ni kitu kibaya asikwambie mtu.

Ukiona kiongozi wa ccmweli kakubali maswali ya papo kwa papo ujue lazima atoe machozi.
*****************************
Wanao sema ccm itakufa watakufa wao-jk
 
Jamaa ni mweupe, ndo maana walimfukuza Tido Mhando. Najua uchaguzi ujao TBCCM hawatakuwa na kipindi kama mchakato majimboni ili tukose fursa ya kuona, sasa nashauri TV binafsi zijiandae na kitu kinachofanana na hicho ili kutupa fursa wanachi kuona uwezo wa uelewa wa watu wetu.
 
Back
Top Bottom