Kweli serikali imejishindwa kabisa

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
522
240
Kuchukiwa kwa serikali hii kunatokana na kutowajibika hata katika masuala madogo sana. Hivi nyie watu mliopo serikalini hamjajua kwamba vitu vidogo mnavyoshindwa kusimamia kunawafanya mchukiwe na kila mtu?
Kwa mfano, hii michango wanayochangishwa wanafunzi wa shule za msingi eti iliwafanye mitihani ni sahihi? Kama ni sahihi mbona watoto hawapewi risiti ya hiyo michango? Hebu angalieni mambo kama hayo. Hilo si swala la kusubiri mzungu aje asaidie. Hebu angalieni shule za manispaa za Iringa muone kama hii michango uko kwenye utaratibu wa kiserikali. La sivyo muamini hakuna mchawi anawaloga mchukiwe ila ni ninyi wenyewe. Eti mtoto aende na fedha shule halafu mwalimu anamwandika kwenye karatasi bila risiti. Mtoto anarudishwa nyumba mkachukue fedha ya mtihani. Hivi matumizi ya hizo fedha nani anaratibu. Mtoto wa darasa la tano mtihani Tsh. 2000. Imekaaje hapo?
 
Back
Top Bottom