Kweli serikali imeishiwa!

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
Malipo ya fedha ya kujikimu mwanzo ilikuwa per diem jumla ya siku 7 ikapanda kuwa siku 14 na sasa imeshushwa mpaka siku 7.kama kweli hatujaishiwa kwa nini imepunguzwa?
 
Nchi inaliwa na wahuni watz tumebaki macho kodoooo.............
 
Nasikia hata fedha ya mizigo imefutiliwa mbali.kazi ipo bado kupunguziwa mshahara.
 
Enzi za mzee wa ruksa serikali haikuwa na pesa lakini wananchi walikuwa na pesa mpaka wakawa hawafanyi kazi tena

Enzi za uwazi na ukweli wananchi hawakuwa na pesa lakini serikali ilikuwa na hela mpaka ikaweza kujenga miradi kibao,mfano,Uwanja wa mpira,barabara,chuo cha UDOM,madaraja ya Mkapa na Umoja na kuvuta maji ya viktoria-Shy n.k

Tofauti ya hizo mbili hapo juu,Mzee wa mapoooda yeye serikali haina pesa na wananchi ndo kabisaaa wamekuwa maskini wa kutupwa,hapa kila kitu kinatoka 10 na kinarudi 0,from HERO TO ZERO

rushwa ni balaa,elimu hovyo,matokeo hovyo mpaka yanavunja rekodi tokea Uhuru,polisi wanazidi kuua,mabomu yanazidi kulipuka,shilingi imekufa kupita maelezo,migomo kila mtaa,umalaya na ulevi mpaka mawaziri wanaongoza,visasi mpaka kwa rais,wizi mpaka benki kuu n.k
 
bora kuishiwa mfukoni kuliko kuishiwa akili. kwa serikali yetu, imeishiwa vyote
 
Ama kweli kumbe yaliyowakuta ndugu zetu Zimbabwe yaweza hata sisi kutukuta...jamani najua hawa wanao tuhumiwa kujichotea pesa zetu wanapita humu JF kama sio wao basi vibaraka wao, umasikini wa Nchi sii wa bahati mbaya, huu ni wakutengenezwa. Siku inakuja ambapo hayo mliyoyachota yatarudishwa kama kwa Mubarak na mwenzake wa Tunisia. Zaidi hata zile mlizozipeleka nje mkidhani itakuwa salama bado vitarudisha...someni alama za nyakati.
 
Back
Top Bottom