Kweli Marehemu Dennis Michael (R.I.P) ni mhanga wa Demokrasia?

MsandoAlberto;1493110]Kamaradi, ushabiki wa siasa unao wewe. Hiyo unayoita turufu ni nini?
Je ulitaka CHADEMA waiachie familia ya Dennis mzigo wa kumzika bila kupaza sauti ili umma ujue nini kilichotokea? Haya, tuwe waungwana, kama CHADEMA ingekaa pembeni na kuachia familia izike kimya kimya kwa kuogopa watu kama wewe kusema mnayoyasema ni michango kiasi gani ingetolewa kuwasaidia watoto wawili, Angel na mwenzake, wa marehemu? Watu kama wakina Sabodo wangeguswa vipi kuchangia sh. Milioni Tano kwa kila familia kusaidia angalau kidogo? Serikali kama inajua kwamba Dennis hakuwepo kwenye maandamano kwanini hawajatoa hata sanda ya kumzikia??? Kwanini hakutoa msaada wowote badala wakawaachia CHADEMA kufanya hicho unachoita siasa??
Kama ni hivyo, kwa waungwana wangetoa mchango tu tena bila ya kujitangazia na kuwaacha ndugu kuamua na kutekeleza shughuli za maziko bila kuwaingilia. Lakini ninyi sio tu mkatumia kuwashurutisha na hata kuwatisha ndugu hao lakini mkahakikisha kuwa mnaonekana dunia nzima mmebeba mwili wake huo kwenda kuzika. Ni wazi kilichowashurutisha sio roho ya kuwasaidia bali nia ya kujifaidisha kisiasa. Mnasahu kuwa Munu anaona yaliyo moyoni. Subiri malipo yakianza hapahapa duniani.

Labda hujui, Polisi walienda nyumbani kwa marehemu wote wakawa wanawashawishi wasipeleke miili uwanjani kuagwa. Familia ya Ismail ilisumbuliwa sana mpaka asubuhi tarehe 12-01-2011 bado walikuwa wanasumbuliwa. CHADEMA wakaamua kusema wanaheshimu uamuzi wa familia na mwili wa Ismail hautapelekwa uwanjani lakini baada ya muda familia ikawafuata vingozi wa CHADEMA na kusema wako tayari marehemu aagwe uwanjani. Hiyo ilikuwa saa tano asubuhi!!!! Ikabidi ratiba iangaliwe upya, utaratibu ufanyike ndipo Ismail akaletwa uwanjani!! Na ndiyo sababu ratiba ilichelewa kuanza!
Hili maelezo yake yameshatolewa na mzazi wa marehemu na ni wazi vitisho na ushawishi ulikuwa ukitoka katika pande zote mbili. Lakini zaidi mkatumia vijana wa Arusha kuwatisha ndugu zake hao kukubali kupeleka maiti ya Ismail katika uwanja mlikuwa mkifanya usanii wenu.

Unayoyasema ni kutoka kichwani kwako na siyo hali halisi iliyopo. Ni vyema ukauliza badala ya kuwa mwepesi kuconclude jambo.

Ndugu wa Dennis (baba yake mkubwa) wakati wa mazishi alisema "sitanyama mpaka niambiwe ni mahakama gani iliamuru Dennis ahukumiwe kifo. Sitanyamaza mpaka haki na ukweli vipatikane". Kwa hasira kubwa alifikia mahali akasema "yeyote anayesema viongozi wa dini wavue majoho waache kukemea dhambi ni malaya" (Mod hayo si maneno yangu nimenukuu kuonyesha ukweli.) Huo ndio msimamo wa familia au ndugu zake Dennis. Sasa kama ukweli utakuwa ni CHADEMA ndio wamesababisha basi watajua!!
Hivi ulitegemea Mzee ama watu wa Rombo kufanya tofauti na kile ambacho Chadema wanataka?

Mazishi yaliyoratibiwa na CHADEMA yalikuwa na malengo yafuatayo;

1. Kuonyesha kusikitishwa kwake na vitendo vya polisi kutumia nguvu kupitiliza na kuua raia wasio na hatia.

2. Kutimiza wajibu wake kama chama cha siasa kinachojali uhai wa mtu na kuguswa na maisha ya kila mtu.

3. Kuuonyesha umma kwamba vitendo vya polisi havina nafasi katika jamii yetu.

4. Kuwapa wanananchi fursa ya kushiriki mazishi ya binadamu wenzao ambao wameuwawa kikatili na polisi.

Ndio sababu hukuona CHADEMA wakitumia magari kueleka watu uwanjani. Ndio maana hukuona CHADEMA wakipita mitaani na miili ya marehemu kuwaonyesha wananchi. Ndio maana wananchi wote walijaa uwanjani walienda pale wenyewe kwa mapenzi yao. Usilaumu CHADEMA kwa sifa wanazopata kutokana na kufanikisha hilo.
Samahani, hujadiliani na mtoto wa mtaani hapa.

Kuhusu suala la 'imani' kwamba waislamu hawaweki marehemu hadharani lazima ujue yafuatayo;

1. imani ya kiislamu hairuhusu polisi kuua raia wasio na hatia.

2. imani ya kiislamu hairuhusu unyanyasaji wa raia.

3. imani ya kiislamu haizuii ukweli kusemwa na haki kupiganiwa.

4. Na mbona hukuhoji Dkt Omar Ali Juma alivyofariki? Au Ismail ndio imeleta shida??

Si kwamba naifahamu imani ya kiislamu au nina uelewa bali nadhani kwa kiasi kikubwa kulikuwa na msukumo kutoka kwa baadhi ya watu kuzuia mwili wa Ismail usiletwe NMC ili kueonyesha kwamba CHADEMA ni chama cha wakristo na hawakumjali muislamu. Pili kuongeza nguvu kwenye hoja kwamba Masheikh Arusha wamemtambua Meya. Sasa hii kwako inaweza kuwa sio siasa ila ni vyema ukaipatia jina!!
Ni kweli kama hujui imani ya dini ya mtu ni vizur kutjaribu kuiongelea. Mazishi ya Dr Omar hayakuwa kama hayo mliyomfanyia Ismail. Dr Omar alizizkwa siku ya pili tu na wala hakusubiri siku nne kuzikwa ili kukamilisha mipango ya wanadunia. Dr Omar alisaliwa tu na sio kuagwa. Lakini pia yaliyofanyika kwa Dr Omar hayakulenga kufaidika kisiasa kwa kikuendi chotechote. Na hili la kujenga picha kuwa Chadema ni chama cha wakristo mnajenga wenyewe na ni wazi ndio maana mlitumia nguvu zote kuhakikisha mnapata wasaa wa kuonekana mkiwa na maiti yake mkasahau hata kuafuta kiongozi mmoja muislamu kubeba mwili wake wakati mkipozi kwa picha ile. Sura ya Ukristo mnaijenga wenyewe kutokana na kushindwa kuwa wavumilivu na kutumia busara zaidi ya ujanjujanja wa kuwa tayari kufaidika na lolote lile hata kama litajenga nyufa za utaifa.

Siku ambayo tutaacha kuwa mashabiki na wakurupakaji badala yake tukatoa hoja objectively then tutakuwa tumewatendea haki watanzania wote wasio na nafasi kama ya kwetu. Endapo tutaendelea kutoa mawazo kwa ushabiki basi nchi itaendelea kuzama kwenye tope na sisi tutabaki kupiga story humu JF!!
Ushabiki unakuwa dhambi pale unapokuwa unakosoa ujanja wenu lakini halali pale unapowafaidisha.
 
Unaweza kufafanua hili "hamuoni tatizo na kutumia kifo chake kufaidika kisiasa. Na hapa ndio ninahoji uungwana na uaminifu kwa watanzania ambao mnadai mnafanya yote haya ili kuwakomboa".

CHADEMA imenufaikaje na kifo cha Dennis? Au CHADEMA imetumiaje kifo cha Dennis kunufaika kisiasa?

Na kwa maoni yako CHADEMA walipaswa kufanya nini mara baada ya kifo cha Dennis na wakati wa mazishi yake?

Kuhusu kuhonga madiwani wa TLP si sahihi. Kama una ushahidi uutoe. Ila sioni sababu ya wewe kuingiza hoja ya Halmashauri ya Moshi katika hili. Sina taarifa kwamba mwenye nyumba aliyefukuza polisi ni mchaga na mfuasi wa CDM. Kama ni taarifa za kweli nakushukuru.

Na suala la kutokuwa objective inawezekana. Na hilo ni kutokana na hisia zangu kwa polisi kwa sababu zaidi ya kuwa wakili na mwana-CDM nilishuhudia kwa macho yangu polisi wakiwapiga wananchi waliokamatwa, wakiwadhalilisha wananchi wanyonge, wakiwaonea wananchi wasio na hatia na mengineyo mengi. Polisi walikuwa wanatekeleza maagizo. Hawakuwa na haki ya kuwafanyia wananchi yale waliyoyafanya! Kama wananchi walikuwa wanaenda kuteka kituo saa kumi na moja jioni, saa tano Mke wa Dr Slaa alipopigwa na kitako cha bunduki alikuwa anaenda kuteka kituo? Mh. Lucy Owenya alivyoshushwa kwenye gari na kupigwa na askari zaidi ya watano na kuibiwa simu na polisi ambaye amehamishia fedha kwenye simu ya polisi mwingine pia ni sawa??? Dennis amepigiwa risasi Kaloleni akiwa anaenda kuchukua gari kama ulivyosema. Picha iliyopigwa mara tu baada ya kupigwa kwake risasi inaonyesha mambo mengi. Utaniambia kwamba polisi walikuwa sahihi?? Siwezi kuwaona walifanya jambo jema hivyo hisia zangu zinaponisukuma kuwaita 'mbuzi' na kufurahia 'taabu' zao lazima uelewe. Natambua umuhimu wa kuwa objective na sio kwamba nitashindwa kutambua hilo simply kwa sababu na mimi huwa naghafilika naishia kuruhusu hisia zangu zinitawale kwa kipindi kifupi. Lazima tuwe objective kama kweli tunataka kuisaidia hii nchi!!
 
Moderator acha ushabiki. Ni haki yangu kutumia kichwa cha habari nilichochagua na kama hakina madhara ya kijamii si jukumu lako kubadilisha na kuweka kichwa cha habari kinachokufurahisha ama kukidhi maslahi yako.....Kichwa cha habari (Title) niliyotumia ni Ninahoji UHANGA wa Marehemu Dennis Michael (R.I.P) na sio Kweli Marehemu Dennis Michael (R.I.P) ni mhanga wa Demokrasia?

Husiwe mkali, Kubali kufundishwa kuna mambo huyajui kuna mambo unajua; sasa Moderator kama amekusaidia siyo Ushabiki ni kazi yake, kuwa Mpole unyolewe sasa kaka.
 
Hakuma mhanga wa demokrasia hata mmoja katika hao waliofariki Arusha na watakaoendelea kufariki iwapo Chadema itaendeleza azima yake ya fujo.

Mwenyekiti wa Chadema hana maadili kwa kuweka danguro katilati ya jiji na kuwatoa muhanga mpaka watoto wa chini ya umri, na ili kufanikisha azma ya kuendeleza ushetani wake, huweka mpaka disko toto pale kwake. Huyo ndio anafaa kusikilizwa kweli?

Upande mwingine, katibu Mkuu wa Chadema kakubuhu kwa uvunjaji sheria mpaka wa kanisa lake, alifukuzwa upadiri kwa zinaa, akaonba hiyo haitoshi sasa kapira mke wa mtu. Jee, waTanzania wenye maadili na wenye kufikiri japo kidogo mnategemea nini kwa watu kama hawa?

Mtegemee kila namna ya upotoshaji wa maadili katika jamii, mpaka wanafikia kudanganya watu waandamane kwa uchu wao wa madaraka.

Halfu watu wanasema ni wahanga wa demokrasia? Ajabu kubwa sana kwa watu wenye akili zao kutaka kuburuzwa na hawa watu wasio na maadili hata kwa dini zao.
 
Ni kweli hakuwa kwenye maandamano ila alipofika eneo la kaloleni na kukuta polisi wanapiga mabomu aliungana na vijana wenzake ambapo alichukua dumu la maji kwenye kibanda cha mama ntilie akawa anawamiminia wananawa uso kupunguza athari za mabomu hata kijana aliekuwa ameongozana naye alipomshauri waondoke alikataa huku akimsisitizia mpk kieleweke
hivyo hakushiriki maaandamano ila alikuwa mpigania haki
 
Back
Top Bottom