comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,939
- Thread starter
- #21
Mkuu, TBC wanaamini kwamba wao pekee ndiyo wenye uwezo na nguvu ya kufika maeneo ya vijijini na hivyo kukaa kwao kimya katika matukio kama haya kunawafanya wananchi waliopo vijijini au pembezoni wasipate
habari zenye kushitua kama hizi
na kuwafanya wawe na maswali au mashaka na utendaji na umakini wa serikali yao. Rejea mkasa wa meli kule Nungwi TBC walikuwa wanapiga taarabu huku habari ikisambaa
kama moto hadi vijijini. Binafsi tukio la kuuwawa kwa askari huko Mkuranga nimelisikia kwa mara ya kwanza kutoka kwa ndg yangu aliyeko Nanyumbu tena kijijini kabisa.
Hivyo wamepoteza sifa ya kuitwa televisheni ya Taifa wanashindwa hata na vituo binafsi kuonyesha matukio kadhaa kwanza hata wakionyesha picha zinakua mnato mara sauti inawahi kuliko msemaji wa tukio, wakati mwingine picha giza tupu