Kwanini Ziwa Nyasa na Tanganyika ni Mali ya Watanzania

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Kwanza kabisa lazima niseme kuwa bwawa na ziwa havina tofauti sana ni kwamba Moja ni la asili jingine ni la kutengenezwa na binadamu.

Bwawa la Nyerere au ziwa Nyerere likikamilika ndo litakuwa ziwa la tatu Kwa ukubwa Africa mashariki baada ya Victoria na Tanganyika Kwa mfatano wa Drainage basin Area. Hii ni kwamba uhai wa ziwa unategemea mito mikuu inayopeleka maji katika ziwa husika.

Diktator Jiwe Chuma Joseph Stalin miaka ya 1940-50 alizuia mto Mkuu unaopeleka maji katika ziwa Moja Kwa ajili ya mashamba makubwa yaliyoleta Mapinduzi ya kiuchumi huko usovieti lakini madhara yake ilikuwa ni kupotea na kukauka Kwa ziwa Hilo, hivo hivo uhai wa ziwa Tanganyika na nyasa unategemea mito mikuu inayolowesha(Konde gang) ziwa Hilo. Sasa kwanini nasema hivo, mto Mkuu unaolowesha ziwa nyasa(inflow) ni Mto Ruhuhu na ndo roho ya ziwa hili mto huu unaanzia huko Kwa kina vunja bei Kipengere mountain range Njombe , Sasa Tukiamua kuzuia mto huu ziwa nyasa litakauka baada ya miaka kadhaa

Vivo hivyo ziwa Tanganyika mloweshaji Mkuu(inflow) ni Mto malagarasi , hata hivyo tiki uchepusha mto huu baada ya miaka kadhaa ziwa litakauka.

Sasa Stiglers au bwawa la Nyerere Lina mto unaitwa Rufiji ambao ndo mto mkubwa na wenye maji mengi kuliko mto wowote unaoujua nchi hii, Sasa mto huu na vijito vingine ndo utakuwa unalowesha ziwa Nyerere na kulifanya kuwa ziwa la tatu Kwa ukubwa nchi hii. Mito inayolowesha ziwa Nyerere mingi inaanzia huko Tukuyu, mbeya vijijini na makete Njombe Yaani nyanda za Juu Kusini mangaribi ambako ndo breas basket ya nchi hoi
 
Kwanza kabisa lazima niseme kuwa bwawa na ziwa havina tofauti sana ni kwamba Moja ni la asili jingine ni la kutengenezwa na binadamu.
Hapa umeuliza swali au umejijibu swali lako?

Mbona kichwa cha habari na habari yenyewe havilingani?

Hebu oga kwanza, kunywa chai afu ndo uandike habari yako.
 
Kwanza kabisa lazima niseme kuwa bwawa na ziwa havina tofauti sana ni kwamba Moja ni la asili jingine ni la kutengenezwa na binadamu.
Ziwa tanganyika linalounganisha nchi yetu na Burundi, Congo na Zambia ulilinganishe na bwawa lako la Rufiji!!!!???

Kuna watu wanapotea ziwa Tanganyika wanazunguka na boti wiki nzima bila kuona ardhi (kutokana na ukubwa wa ziwa lenyewe)
 
Elewa mada
Ziwa tanganyika linalounganisha nchi yetu na Burundi, Congo na Zambia ulilinganishe na bwawa lako la Rufiji!!!!??? Punguza bangi wewe, kuna watu wanapotea ziwa Tanganyika wanazunguka na boti wiki nzima bila kuona ardhi (kutokana na ukubwa wa ziwa lenyewe)
 
Bro nati zako zitakua zimelegea kama hujui kutofautisha ziwa na bwawa bas ww ni KILAZA
Umemkosoa Bure tu ndg, mleta maada Yuko sahihi. Kitaalam (kihandisi) bwawa ni lile tuta linalojengwa kukinga/kuzuia kiasi flani cha maji yabaki upande wa juu(upstream).

Yale maji yanayozuiliwa upande wa juu ya moto husambaa eneo la ukubwa flani kutengeza ziwa.
 
Kwanza kabisa lazima niseme kuwa bwawa na ziwa havina tofauti sana ni kwamba Moja ni la asili jingine ni la kutengenezwa na binadamu.

Bwawa la Nyerere au ziwa Nyerere likikamilika ndo litakuwa ziwa la tatu Kwa ukubwa Africa mashariki baada ya Victoria na Tanganyika Kwa mfatano wa Drainage basin Area. Hii ni kwamba uhai wa ziwa unategemea mito mikuu inayopeleka maji katika ziwa husika.
Mkuu unataka kusema nini?
 
Kwanza kabisa lazima niseme kuwa bwawa na ziwa havina tofauti sana ni kwamba Moja ni la asili jingine ni la kutengenezwa na binadamu...
Acha kabisa mkuu mto rusizi unaujua lakini au Burundi umefika maana nikuambie tu Burundi ndio inawezeka inalishia maji mengi kuliko sisi tz maana hata hio malagarasi yenyewe inaanzia Burundi pia
 
Ziwa tanganyika linalounganisha nchi yetu na Burundi, Congo na Zambia ulilinganishe na bwawa lako la Rufiji!!!!??? Punguza bangi wewe, kuna watu wanapotea ziwa Tanganyika wanazunguka na boti wiki nzima bila kuona ardhi (kutokana na ukubwa wa ziwa lenyewe)
uchambuzi wa wa soka la kibongo ndio anataka kuuleta kwenye mambo ya kisayansi!!hahaaaa,
 
Back
Top Bottom