WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Nimekuwa nikijiuliza kila mara, kwenye nchi za wenzetu ni kawaida sana kukutana na wahudumu ( waiters/waitresses) ambao ni wanafunzi hasa wa vyuo vikuu wakifanya kazi kwenye mahoteli au migahawa kama namna ya kuongeza kipato kwa njia ya halali. Siyo huko tu, hata kwenye maktaba, maduka ya nguo, vyakula, nk. Hii ni kwa uchache tu.Tanzania sijabahatika kuona hili... hapo hapo unaona wanafunzi waki struggle sana kupata pesa au kulalamika kuwa pesa wanayoipata haiwatoshi. Siyo ajabu kusikia wanafunzi hasa wa kike wakisemwa kuwa wanafanya vitendo visivyo sawa kujipatia pesa.
Ni kwanini watanzania hatujaona hizi fursa za kupata pesa ya halali na hapohapo kujitengenezea CV ili pale mtu utakapotafuta kazi " experience" isiwe ni tatizo tena maana moja ya sababu zinazowakosesha kazi vijana wengi ni kukosa uzoefu.
Naweza nikawa nakosea , labda tayari wapo wenye kufanya hizi part time, lakini nadhani wengi bado wanasubiri kuja kuanza kazi wamalizapo vyuo au kufanya "tempo" wawapo likizo...
Hebu tubadilishane uzoefu kama namna ya kusaidiana kutatua matatizo ya kijamii..