Kwanini wanawake wengi hawapendi kufundishwa kuendesha gari na waume zao?

Looh...n'nachokumbuka ni kununiana karibu wiki nzima.
Nilichojifunza ni kuwa sio kila mtu ni mwalimu.
 
Ndivyo nilivyokufundisha kukanyaga clutch? hebu kanyaka hadi mwisho ala!, nimekwambia kanyaga mafuta taratibu, unaangalia wapi? hebu tazama barabara na sio watu pumba*v zako wewe... mara ghafla kofi pwaaaaaa!
Usipokua mkali utapeleka gari garage kila siku
 
Nilifundishwa na mdogo wang it reached a stage machozi yananitoka maana ananikaripia balaa so he (husband) had to be soft kunipa ile courage ila hawafai katika kufundisha haswa pale unapochanganya desa in reverse badala ya kulia uende kushoto na kushoto uende kulia
 
Yaani ni Majanga haswaaa kufundishwa na mume,matusi yatakuwa yako,maneno yenye kuudhi na vibao ukubaliane navyo,kumbe ni janga la kitaifa mi nilifikiri ni kwangu tu.
 
Kumbe wewe ndo umenipa jibu my wife pamoja na kwenda driving school hataki kuendesha ananiambia mpaka ninunue automatic kumbe anadhani nitamdhabua lol! ngoja nikamilishe visenti vyangu ninunue nione kama atatoa sababu nyingine.
 
Basi na nyie nunueni ya kwenu muwafundishe waume zenu ili muwapige vibao! natania jamano msiniuo fatadhali.
 
Ha ha ha haaaaa, naja Nyerere Day ujue.
Safari hii simtaki tena yule babu mwenzio kawa bahili ka nini, nampotezea, tukutane pale facebook

Mzee Mtambuzi asisome hapa

Nakusubiri kwa hamu......

Ngoja nijifue kabisa.
 
Dada yangu kanilalamikia kwamba mumewe akimfundisha kuendesha gari huwa anamlabua makofi kila akikosea na anakuwa na lugha kali sana wakati akitoa maelekezo, lakini pia nimewahi kuwasikia baadhi ya wanawake wakisema ni heri kwenda driving school kuliko kufundishwa kuendesha gari na waume zao kutokana na kukaripiwa wakati wakifundishwa pale wanapokosea na kulabuliwa makofi.

Je, wanaume tuhuma hizi zina ukweli?
Sasa kama mko barabarani na kuna lori mbele, halafu anakanyagia accelarator badala ya breki nimpige busu? Hapo ni konzi tu atakula!
 
mie huwa sielewi mwanamke unapigwa bado upo tu! mie wangu alianza mazoea ya kunikaripia nikamwambia ndugu kwa heri....mtu mwenyewe sura ka kitunguu halafu akae ananikaripia mtoto wa mwenzio hell NO!
 
mie huwa sielewi mwanamke unapigwa bado upo tu! mie wangu alianza mazoea ya kunikaripia nikamwambia ndugu kwa heri....mtu mwenyewe sura ka kitunguu halafu akae ananikaripia mtoto wa mwenzio hell NO!

Acha kuwapotosha wenzako wewe huna Mume waache walioolewa na ndoa zao.
 
Sasa si kwa manufaa yako mwenyew ili uwe serious kujiepusha na ajali nà damage.mie nkiona unakosea kizembe hadi mateke juu nani anataka kuwa widower??
 
Hili ni kweli mara nyingi huishia ugomvi lakini hili la kuzabuliwa vibao limepitiliza viwango, hutokea hata kwa mababa na mabinti zao. Tatizo la baadhi ya wanaume wanadhani makosa yanayofanywa na wanafunzi wao hayastahili kufanywa hivyo huanza kutumia lugha ya ukali na mwisho huzaa varangati. Mdada mmoja ugomvi na mumewe akasusa akaamua kwenda kulipa driving school.

Back
Top Bottom