Kwanini wanafunzi wa shule ya Msingi na Sekondari siku hizi hawana vitambulisho?

Siempre Hechos

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
1,117
1,327
Nimekuwa nikijiuliza kwani kitambulisho maana yake ni nini? na kazi yake ni nini?, au vinatumika kwa baadhi tu ya watu na taasisi na sekta nyingine?. Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari siku hizi hawana vitambulisho ama ni mimi sifatilii mambo? Yawezekana kwao sio muhimu kwa sababu wanavaa sare za shule yao na ni rahisi kutambulika?.

Lakini je mbona kuna baadhi ya taasisi za serikali wanavaa sare za kazi na vitambulisho wanavyo? Wanafunzi hawa hawa kunasiku hawana sare za shule na wanaenda huku na huko katika shughuli za kijamii ama binafsi wakiwa peke yao na wanasafiri kutoka kituo A mpaka B, Je, tutawatambuaje pale watakapopatwa na tatizo na fahamu hawana ili wasaidike? au ndo tutawapiga picha na kurusha kwenye mitandao ya kijamii halafu problem solved?
 
Siku hizi unamaanisha kuanzia mwaka gani?
Binafsi kitambulisho nimekuja kukutana nacho nilivyokuja chuo
 
Back
Top Bottom