Kwanini waliozaliwa katika familia maskini wana nafasi kubwa na wao kuwa maskini kuliko waliozaliwa katika familia tajiri?

Wazazi maskini ushauri wao kwa watoto ni kuhusu umaskini tu, mfano utawasikia Wakinga wanaroga ndomaana wanafanikiwa au Wachaga wezi ndomaana wanafanikiwa.
Mzazi anawaambia watoto mambo ya kufikirika.
Mimi ni Mkinga najua maskini wengi hawajitumi na sio wabunifu wao wanafikiri waliofanikiwa ni Freemason au wametoa kafara. Bahati mbaya wazazi maskini huwakaririsha ujinga huu watoto wao.
 
Ni swali fikirishi kidogo ukiangalia wengi wanaotokea familia maskini wengi huishia kuwa masikini ni wachache sana ambao hutoboa kimaisha. Au ndo tuseme umasikini mtu anaweza kuurithi?
mfano: mawazo ya kimasikini kutoka kwa baba yanaweza kuhamia kwa mtoto
kama baba hakuwa na vitega uchumi hawezi kukushauri kuhusu kuwa na vitega uchumi, kama alikuwa muoga katika kuwekeza itaweza kukufanya na wewe kuwa muoga.
Kwa kifupi falsafa ya baba ni rahisi sana kuhamia kwa mtoto mpaka ujipambanue sana ndo unaweza kuondokana nazo.
Tunatokaje katika hili? hebu tupeane mawazo zaidi

karibuni kwa mawazo wakuu
Umasikin mbegu
 
Utajiri wa kweli ni ule unaorithishwa kizazi hadi kizazi.
 
umezaliwa uswahilini, shule ukasoma uswahilini, ukaendelea kukaa uswahilini, Vijiwe vyako ni vilabuni, vijiwe vya bao na solo au drafti, mpira unaangalizia vibanda umiza, utakuwa tajiri saa ngapi na hao matajiri utawaona wapi?

Sasa mwenzio kkazaliwa uzunguni, kakulia uzunguni, kasoma IST, huko kakutana na
"wenye dunia" sasa kwanini asije kuwa tajiri?

Mazingira yana nafasi kubwa sana ya kumfanya mtu kuwa tajiri au kuendelea kuwa masikini.
Mazingira yanaweza kuwa shida sana.Tatizo waafrika wengi hatuamini tena katika uendelevu wa familia na mali.Tuna amini sana katika ku survive (Ajira) badala ya kuchukua hatua endelevu za kuondokana na umasikini wa familia na ukoo.
 
Ni swali fikirishi kidogo ukiangalia wengi wanaotokea familia maskini wengi huishia kuwa masikini ni wachache sana ambao hutoboa kimaisha. Au ndo tuseme umasikini mtu anaweza kuurithi?
mfano: mawazo ya kimasikini kutoka kwa baba yanaweza kuhamia kwa mtoto
kama baba hakuwa na vitega uchumi hawezi kukushauri kuhusu kuwa na vitega uchumi, kama alikuwa muoga katika kuwekeza itaweza kukufanya na wewe kuwa muoga.
Kwa kifupi falsafa ya baba ni rahisi sana kuhamia kwa mtoto mpaka ujipambanue sana ndo unaweza kuondokana nazo.
Tunatokaje katika hili? hebu tupeane mawazo zaidi

karibuni kwa mawazo wakuu
Like a father, like a son. Viscous circle of poverty.
 
1. Maskini hana urithi wa mali

2. Maskini hana wazazi wenye connections kwasababu watu wengi wanaojuana huwa katika level moja ya uchumi, mara nyingi matajiri circle zao ni za matajiri na wazazi wake wakiwa maskini, basi circle zao zimejaa maskini wenzao

Suluhisho.

1. Atengeneze connections zake kwa jasho lake yeye mwenyewe

2. apambane kwa bidii awe juu sana kwenye kitu anachofanya, kama ni shuleni basi afaulu mpaka vyuo vinambakiza awe lecturer, kama ni biashara inabidi ajibane kweli kweli ili mtaji uongezeke, n.k

3. atumie kipaji chake, hapa wenye vipaji wengi (sio wote) wanatokeaga maisha magumu kuanzia kina pele, maradona, messi, ronaldonho, michael jackson, n.k. tumia ulichojaaliwa kikunufaishe.

Vitu ambavyo havina msaada:

Tamaa - hapa atageuka kuwa kibaka anaweza kuishia kuchomwa moto, anaweza kuwa malaya akaishia kufubazwa kwa magonjwa na kujishusha utu.

Kulalamika kuzaliwa maskini - kuzaliwa maskini si uamuzi wako lakini kufa maskini kwa kiasi kikubwa ni uamuzi wako, kama nguvu unazo, akili unazo, n.k pambana mpaka kieleweke, hapa nikianza kuweka listi ya matajiri waliokuwa maskini tutakesha maana hata Mengi (r.i.p) alizaliwa familia ya kimaskini.

kuendekeza kauli za kimaskini - tumevikuta na tutaviacha, kulikuwa na matajiri flani ila leo wako wapi, cha muhimu kupumua, n.k achana na taka taka hizi aisee, umevukuta na utaviacha lakini hakikisha na wewe vikupitie hata kwa mbali, ukiendekeza hizi kauli za kijinga utateseka sana.

Kutafuta connection kwa kujishusha utu wako - tafuta connections bila kuondoa utu wako, kuwa chawa inapobidi kwa mbali lakini usiwe kupe ambae hata unapoona kabisa watu wanakuvumilia uwepo wako wewe unang'ang'ania, yani unalazimisha sana ukaribu lakini watu unaona kabisa wanakuvumilia tu kinafki wanatamani uondoke na hawana muda na wewe, mfano mzuri hapa nahisi pana Steve Nyerere, yani huyu hata kwa mwaka huu kuna semina ilikuwa ya viongozi wa kike pale Dodoma, jamaa alienda aisee, Pia huko kwa viongozi wengine analazimisha sana connection anabaki kituko tu maana washamkariri yupo kwa maslahi yake tu, matokeo yake hata michongo ama teuzi hapati kwa tabia hizi.

Wivu na chuki kwa wenye navyo - Wivu hautakusaidia chochote zaidi ya kukuumiza tu na mwishowe kuwa mshirikina tu na ushirikina haunaga maendeleo, wivu wako na chuki kwa waliofanikiwa utakuumiza sana hii dunia, kutwa nzima utawaombea mabaya wenzako na utazidi kuumia wanavyozidi kutoboa.

kuwekeza muda mwingi kwenye anasa - Sio tatizo ukiwa na ratiba maalum lakini ni tatizo ukizidisha,,,,iwe ni pombe, ngono, sigara, bangi, n.k hivi vitu vitakufanya usahau kabisa malengo yako huku afya yako ikizidi kuzorota.
.. kutwa nzima unawaombea mabaya.....sentesi hii unaweza iita executive summary ya andiko lako. Muda mwingi badala ya kupanga mambo yako, unautumia kulalamika na kuwaombea watu wengine mabaya.
 
hakika ndugu! .yaani tunatumia muda mwingi kulalamika kuliko kuchukua hatua
Na hata viongozi pamoja na ukwasi walio nao, akili ni za kimaskini. Wanatumiwa muda mwingi kuelezwa matatizo badala ya njia za kutatua.
 
Utajiri ulithishwa vizazi na vizazi. Wale wanaotokea kwenye familia zilizo na mali huwa na kazi ndogo ya kuendeleza. Vivyo hivyo umasikini nao urithishwa vizazi na vizazi maana watoto hukosa pa kuanzia. Kule kwetu kuna msemo wa kihenga kuwa mwenye kuwa na mali huanzia kwa baba yake.

Taikuni wa fasihi alileta uzi humu juu ya umuhimu wa kurithisha vizazi vyetu mali Ila kuna watu walimpuuza Ila ni ukweli japo ni mchungu. Agano la kale tunasmbiwa Isaka alivifukua upya visima vya baba yake vilivyofukiwa na maadui zake. Hatuambiwi alichimba. Hiyo ni one step ahead dhidi ya yule ambaye baba hakuacha hata shimo. Ni wachache sana wanaokuwa matajiri wakitokea from the scratch nao ni kwa mateso makubwa sana.
 
Wazazi maskini ushauri wao kwa watoto ni kuhusu umaskini tu, mfano utawasikia Wakinga wanaroga ndomaana wanafanikiwa au Wachaga wezi ndomaana wanafanikiwa.
Mzazi anawaambia watoto mambo ya kufikirika.
Mimi ni Mkinga najua maskini wengi hawajitumi na sio wabunifu wao wanafikiri waliofanikiwa ni Freemason au wametoa kafara. Bahati mbaya wazazi maskini huwakaririsha ujinga huu watoto wao.
Nakubaliana na wewe kabisa. Mimi nina ndugu yangu yaani yeye muda wote analalamikia maisha awe na familia au mtu baki. Mfano ukimpigia simu ukamuuliza tu umeamkaje leo, weee ataanzia hapo, unadhani kuna kulala basi, yaani maskini anatoa wapi usingizi, ohh ukiwa maskini unajikuta tu ni asubuhi, ohh matajiri ndio wanalala sisi wengine tulala mbinguni ohhh hiki mara kile yaani mi mama maskini hivi au vile duh yaani utajuta kusalimia😂 yaani shida tupu. Wakati na wewe una pambana mbio mbio ye kulalamika na kuukumbatia umasikini wake.

Anaamini kwenye ushirikina haswaa, au mara yule mwanamke ana mikosi ndio maana maisha yangu hayaeleweki (mke) ohh mara nilikuwa na mwanamke huyu kidogo nilishika hata elfu 10,
(mchepuko) 😂😂😂😂 mara anapata kazi anafanya hela haoni hapo ujue anaona kalogwa😭 au mara anapata kazi sehemu wanakubaliana kimtindo tu siku akija anakuta mtu mwingine anafanya malalamiko kama kawaida yaani ni shida.

Akikitumia msg hata 10 zote analalamikia umasikini tu wake etc. yaani tunasaidiana hivyo hivyo maisha yanakwenda maana hata umshauri wala haelewi kitu. Yaani analalamikia shida zake kuliko kutafuta solution. Sasa mtu wa hivi unamsaidiaje wakuu?
 
Ni swali fikirishi kidogo ukiangalia wengi wanaotokea familia maskini wengi huishia kuwa masikini ni wachache sana ambao hutoboa kimaisha. Au ndo tuseme umasikini mtu anaweza kuurithi?
mfano: mawazo ya kimasikini kutoka kwa baba yanaweza kuhamia kwa mtoto
kama baba hakuwa na vitega uchumi hawezi kukushauri kuhusu kuwa na vitega uchumi, kama alikuwa muoga katika kuwekeza itaweza kukufanya na wewe kuwa muoga.
Kwa kifupi falsafa ya baba ni rahisi sana kuhamia kwa mtoto mpaka ujipambanue sana ndo unaweza kuondokana nazo.
Tunatokaje katika hili? hebu tupeane mawazo zaidi

karibuni kwa mawazo wakuu
Investing behaviour ndo zinatutofautisha huko mbele,what to invest in and how much to risk.
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Mimi nina ndugu yangu yaani yeye muda wote analalamikia maisha awe na familia au mtu baki. Mfano ukimpigia simu ukamuuliza tu umeamkaje leo, weee ataanzia hapo, unadhani kuna kulala basi, yaani maskini anatoa wapi usingizi, ohh ukiwa maskini unajikuta tu ni asubuhi, ohh matajiri ndio wanalala sisi wengine tulala mbinguni ohhh hiki mara kile yaani mi mama maskini hivi au vile duh yaani utajuta kusalimia😂 yaani shida tupu. Wakati na wewe una pambana mbio mbio ye kulalamika na kuukumbatia umasikini wake.

Anaamini kwenye ushirikina haswaa, au mara yule mwanamke ana mikosi ndio maana maisha yangu hayaeleweki (mke) ohh mara nilikuwa na mwanamke huyu kidogo nilishika hata elfu 10,
(mchepuko) 😂😂😂😂 mara anapata kazi anafanya hela haoni hapo ujue anaona kalogwa😭 au mara anapata kazi sehemu wanakubaliana kimtindo tu siku akija anakuta mtu mwingine anafanya malalamiko kama kawaida yaani ni shida.

Akikitumia msg hata 10 zote analalamikia umasikini tu wake etc. yaani tunasaidiana hivyo hivyo maisha yanakwenda maana hata umshauri wala haelewi kitu. Yaani analalamikia shida zake kuliko kutafuta solution. Sasa mtu wa hivi unamsaidiaje wakuu?
Hahaha aisee yaani bado tuna safari ndefu sana. Watu wa hivyo mara zote tunawaacha tu maana ataanza kukusimulia hapo atakwambia nilifuga kuku wakafa wote (wananiloga) nilifanya biashara fulani nayo ikafa . Hana muda wa kutafakari kwanini biashara ilikufa huenda ilikufa kwa uzembe wake tu. Mtu wa hivyo anakwambia mi nimejaribu kila kitu lakini bado masikini.
 
Back
Top Bottom