Kwanini wafanyakazi wengi wa Serikali wanapenda kutengeneza mazingira ya kupewa hela katika huduma wanazotoa?

Smith Rowe

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
3,311
5,417
Mzuka,

Hivi ni Serikali haiwalipi watumishi wake au shida ni nini?

Yaani unaenda kufata huduma ofisi za Serikali lakini mtoa huduma muda wote anatengeneza mazingira ya kupewa hela (rushwa).

Ofisi imeandikwa kabisa huduma hiyo ni bure lakini yeye anataka umpe hela akusaidie wakati hilo ndo jukumu lililomuweka pale, mfano nilifata TIN number ya kampuni ukiingia tuu kwenye ofisi zao unaona kabisa kumeandikwa TIN number ni bure lakini lenyewe lilivyo-lijinga linataka kitu kidogo RUBBISH.

Halmashauri na TRA zimejaa rushwa.

Kuna ofisi nyingine tena huko kanda ya ziwa ya TRA nilienda kufanyiwa makadirio ya kampuni mpya badala ya kunieleza jinsi ya kufanya linataka nilipe laki tano linifanyie makadirio ambayo ni kitu cha bure, yaani wakiona mtu mzee mzee umekaa ki-mbugila mbugila wanaamini huelewi kitu wanataka uwape hela wakupe huduma.

Hili jambo limenikasirisha sana itabidi nipambane familia yangu isihangaike na ajira ambazo ni kama wizi.

Swali
Serikali hamuwathamini wafanyakazi wenu hadi wamekuwa wanatamani fedha za wananchi kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom