Kwanini Wabunge hawakumlilia Kawambwa naye awajibike kuhusu matokeo mabaya ya elimu?

Kwa kweli wizara ya elimu inahitaji mtu anayeweza...huyu waziri wa sasa sijui anafanya nn kwa kweli anyways serikali inajitahidi kuwafanya wananchi wasiwe na elimu nzuri...ili wawatawale vizuri
 
HIvi inawezekana kuwa na mafanikio katika nyanja nyingine bila kuwa na mafanikio katika elimu?
Wanaotakiwa kuwa shule ili baadae wawe viongozi na watawala tayari wako shule na shule zao sio hizi anazosimamia Kawambwa na Nagu. Unaona wanasoma vizuri tu. Wanakuwa Wabunge halafu wanateuliwa kuwa manaibu au mawaziri kamili kutegemea na uzito wa mzazi wake.
Mfumo wa wanaotakiwa kwenda shule umekamilika. Watanzania wachache masikini watajipenyeza hapa na pale kutoka shule hizi za Kata, watapelekwa Bungeni pale kama vikatuni, ngoma itakuwa kwenye ajira tena.
 
Hakuna hasara kubwa kama taifa kuwa na wajinga wengi, Ajira wanazoweza ni kuokota makopo na chupa zamaji mitaani, kazi ambazo hazileti maendeleo binafsi wala kwa taifa.
 
Waheshimiwa woooote wanaweza kutimuliwa lakini kamwe sio huyo jamaa. Na kwa hakika wala huitaji miwani ya macho kuona alivyovurunda kote alikopita,lakini utashangaa jamaa bado yupo anadunda.Kimsingi ana uswahiba mkubwa na nyumba kubwa!
 
Hawa jamaa wanalia sana pale ambapo pesa imetumika vibaya na wao hawajapata mgawo; sorry for this lakini ndo ukweli. Hebu fikiria elimu na afya kufanyika biashara bunge liko kimya, huwezi ukapata wasomi wazuri wakati elimu inauzwa kama bidhaa nyingine yoyote; matokeo mabaya au mazuri ya wanafunzi sio kipaumbele cha bunge; Bunge halijui vipaumbele ambavyo vingesaidia taifa hata bila jasho, ELIMU KUFANYIKA BIASHARA JANGA KWA TAIFA. Wafidieni waliofungua shule kisha shule ziwe mali ya serikali, elimu na biashara TZ itaumbuka, tumeiga jambo baya sana na tutajuta.
 
Sikutaka kulileta hili lakini inaonekana sina ujanja. Katika kikao kilichopita wabunge wetu wengi walionekana kukerwa zaidi na ripoti za CAG na zile za kamati kuhusiana na mambo mbalimbali. Wizara kadhaa zilinyoshewa kidole na hatimaye mawaziri wake wakaondolewa. Hata hivyo, binafsi naamini hakuna kashfa yenye madhara ya moja kwa moja na ya kudumu kama iliyoko kwenye elimu.

KUanzia elimu ya msingi na sekondari kuna changamoto ambazo kwa kweli ni dhambi kwa watoto wetu. Cha kuudhi zaidi inaonekana wabunge wetu wamekubali hali ilivyo na sijasikia wengi wakitaka waziri wa elimu Bw. Shukuru Kawambwa awajibike pia kama walivyowajibishwa wale wa sekta ya afya. Ni kwanini? Ni kweli hawajaona uovu uliopo kwenye sekta hiyo? ni kweli wabunge wetu hawajaona hali ilivyo kwenye shula za kata na mamia ya shule za msingi vijijini na mijini?

Hivi, inakuwaje Ngeleja anawajibishwa lakini Kawambwa anaachwa? Ni kweli sekta ya nishati ina umuhimu mkubwa kuliko elimu? Ni kweli madhara ya kukosa umeme wa kudumu kwa asilimia 14 ya wananchi wetu ni makubwa zaidi kuliko kukosa elimu bora na mazingira bora kwa asilimia zaidi ya tisini ya watoto wetu? Ni kweli kwamba wabunge wetu hawajasoma ripoti mbalimbali za elimu ambazo zimetolewa na CAG taasisi nyingine.

Kwanini, hata upinzani hauonekani kukerwa na kushindwa kwa sera ya elimu ya serikali ya chama cha mapinduzi na badala yake na wao wako kimya kutaka watu wawajibike? Hivi ni mpaka walimu na wanafunzi nao wagome ndio tutajua kweli kuwa tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyodhania?

Kilichowafanya wabunge wawashupalie NGeleja, maige, mponnda na nundu si service felivery per se - wabunge waliona wivu jinsi wenzao wanavyopinga panga na kununua majumba ya kifahari, sikuona wabunge wakilalamikia human mortalities(afya), kukosa umeme(nishati), kukosa ndege na usfiri duni(usafirishaji), simba na wanyama wengine kuua watu na kuahribu mali(mali asiri). Wabunge walisukumwa zaidi na wivu na gere na si kutaka maendeleo.
 
Watoto gani?

Hawa wanaovaa suruali za Pink mlegezo, viatu vya ulimi? na vi skin tight wanazunguza mitaani mida ya shule?

Nadhani wakuwajibishwa ni wazazi!

PENYE RED

100% Naunga mkono hoja. Waziri hashindi na watoto wetu. Wazazi ndio vinara wa kusaka mitihani kwa ajiri ya watoto wao. Waziri awajibishwe kwa makosa yake ya watumishi waliochini yake kukubali kuhongwa na wazazi na kuvujisha mitihani.
 
Kikwete ameondoa wabadhirifu wa pesa za umma, suala na nani mwenye uwezo wa kutawala nini haikuwa hoja kwake, ameangalia uaminifu(nadhani)
 
Sikutaka kulileta hili lakini inaonekana sina ujanja. Katika kikao kilichopita wabunge wetu wengi walionekana kukerwa zaidi na ripoti za CAG na zile za kamati kuhusiana na mambo mbalimbali. Wizara kadhaa zilinyoshewa kidole na hatimaye mawaziri wake wakaondolewa. Hata hivyo, binafsi naamini hakuna kashfa yenye madhara ya moja kwa moja na ya kudumu kama iliyoko kwenye elimu.

KUanzia elimu ya msingi na sekondari kuna changamoto ambazo kwa kweli ni dhambi kwa watoto wetu. Cha kuudhi zaidi inaonekana wabunge wetu wamekubali hali ilivyo na sijasikia wengi wakitaka waziri wa elimu Bw. Shukuru Kawambwa awajibike pia kama walivyowajibishwa wale wa sekta ya afya. Ni kwanini? Ni kweli hawajaona uovu uliopo kwenye sekta hiyo? ni kweli wabunge wetu hawajaona hali ilivyo kwenye shula za kata na mamia ya shule za msingi vijijini na mijini?

Hivi, inakuwaje Ngeleja anawajibishwa lakini Kawambwa anaachwa? Ni kweli sekta ya nishati ina umuhimu mkubwa kuliko elimu? Ni kweli madhara ya kukosa umeme wa kudumu kwa asilimia 14 ya wananchi wetu ni makubwa zaidi kuliko kukosa elimu bora na mazingira bora kwa asilimia zaidi ya tisini ya watoto wetu? Ni kweli kwamba wabunge wetu hawajasoma ripoti mbalimbali za elimu ambazo zimetolewa na CAG taasisi nyingine.

Kwanini, hata upinzani hauonekani kukerwa na kushindwa kwa sera ya elimu ya serikali ya chama cha mapinduzi na badala yake na wao wako kimya kutaka watu wawajibike? Hivi ni mpaka walimu na wanafunzi nao wagome ndio tutajua kweli kuwa tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyodhania?

Simple....wabunge wengi watoto wao wanasoma academia....hawana uchungu na elimu ya kata inayotolewa kwa watoto wa watanzania wa hali ya kawaida.
 
HIvi inawezekana kuwa na mafanikio katika nyanja nyingine bila kuwa na mafanikio katika elimu?
Mkuu, mimi kama mdau wa Elimu, naumizwa sana na ukurupukaji wa mipango ya sector ya elimu nchini, lakini pia na priority ndogo inayopewa sector ya elimu.

However, hili swala tukilizungumzia katika hali ya kisiasa........kwamaana ya kwanini Kawambwa asijiuzulu au why Ngeleja and not Kawambwa tutakuwa tunaikosesha ladha hii mada, kwasababu issue za report ya CAG zilikuwa ngumu kumeza kwenye wizara nyingine na sio Elimu. Kumbuka Wizara ya Elimu imevurugika sana kwa maana ya kwamba, sio kila kitu kuhusucho ELIMU kipo sehemu wizara ya Elimu.

Kama kuna mishahara hewa, itabidi TAMISEMI wahusike, kama kuna capitation grants haifiki mashuleni, itabidi Halmashauri za wilaya na manispaa zijibu tuhuma.

There is a lot here........!
 
Me naona wabunge wetu hawako makini na jambo la elimu,yaani elimu kwao haina umuhimu kabisaa na ndio maana wabunge wengi ni vilaza,hili swala la elimu linatakiwa lianze kupigiwa kelele na sisi wenyewe majimboni kwetu,kwa sababu bungeni wanalikwepa kana kwamba halina umuhimu.

Na ukipata takwimu za matokeo mwaka huu form 6 utazimia
 
Sikutaka kulileta hili lakini inaonekana sina ujanja. Katika kikao kilichopita wabunge wetu wengi walionekana kukerwa zaidi na ripoti za CAG na zile za kamati kuhusiana na mambo mbalimbali. Wizara kadhaa zilinyoshewa kidole na hatimaye mawaziri wake wakaondolewa. Hata hivyo, binafsi naamini hakuna kashfa yenye madhara ya moja kwa moja na ya kudumu kama iliyoko kwenye elimu.

KUanzia elimu ya msingi na sekondari kuna changamoto ambazo kwa kweli ni dhambi kwa watoto wetu. Cha kuudhi zaidi inaonekana wabunge wetu wamekubali hali ilivyo na sijasikia wengi wakitaka waziri wa elimu Bw. Shukuru Kawambwa awajibike pia kama walivyowajibishwa wale wa sekta ya afya. Ni kwanini? Ni kweli hawajaona uovu uliopo kwenye sekta hiyo? ni kweli wabunge wetu hawajaona hali ilivyo kwenye shula za kata na mamia ya shule za msingi vijijini na mijini?

Hivi, inakuwaje Ngeleja anawajibishwa lakini Kawambwa anaachwa? Ni kweli sekta ya nishati ina umuhimu mkubwa kuliko elimu? Ni kweli madhara ya kukosa umeme wa kudumu kwa asilimia 14 ya wananchi wetu ni makubwa zaidi kuliko kukosa elimu bora na mazingira bora kwa asilimia zaidi ya tisini ya watoto wetu? Ni kweli kwamba wabunge wetu hawajasoma ripoti mbalimbali za elimu ambazo zimetolewa na CAG taasisi nyingine.

Kwanini, hata upinzani hauonekani kukerwa na kushindwa kwa sera ya elimu ya serikali ya chama cha mapinduzi na badala yake na wao wako kimya kutaika watu wawajibike? Hivi ni mpaka walimu na wanafunzi nao wagome ndio tutajua kweli kuwa tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyodhania?
oWOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOTE
wanapozungumzia sera ya elimu ya Tanzania hawaelewi wala kufeli kwa wanafunzi siyo kawambwa issue iko wazi serikali inawalipa waalimu mshara mdogo hivyo waalimu wanatumia muda mdogo mashuleni,yaani waalimu wa tanzania walishagoma miaka mingi iliyo pita hata utenge sera gani hali ni hivi hivi,marupu rupu kama taasisi nyingine
 
Hivi, inakuwaje Ngeleja anawajibishwa lakini Kawambwa anaachwa? Ni kweli sekta ya nishati ina umuhimu mkubwa kuliko elimu? Ni kweli madhara ya kukosa umeme wa kudumu kwa asilimia 14 ya wananchi wetu ni makubwa zaidi kuliko kukosa elimu bora na mazingira bora kwa asilimia zaidi ya tisini ya watoto wetu? Ni kweli kwamba wabunge wetu hawajasoma ripoti mbalimbali za elimu ambazo zimetolewa na CAG taasisi nyingine.
...Ukiwa kama mwananchi wa kawaida, utaudhika kwenye lipi, umeme ukikatika kila siku masaa 12 kwa miezi miwili, au mtoto mmoja mtaani asipoenda shule kwa utoro na au kumaliza darasa la saba akiwa hajui kusoma wala kuandika, tena jina lake?.

...The whole incident was reactionary, and so, the measures taken. Bado tunajifunza, kutokana na makosa. Hatimae tutafika.
Kwanini, hata upinzani hauonekani kukerwa na kushindwa kwa sera ya elimu ya serikali ya chama cha mapinduzi na badala yake na wao wako kimya kutaka watu wawajibike? Hivi ni mpaka walimu na wanafunzi nao wagome ndio tutajua kweli kuwa tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyodhania?
...Sera haijashindwa. Uchambuzi na vigezo vilivyotumika kuonyesha sera imeshindwa vi wapi?. Watu ndio wameshindwa!

...Huduma za afya zinapokuwa mbaya, huwezi sema madawa yameshindwa kutibu -wakati yanamwagwa yenye thamani ya mabilioni ya pesa- bila kuangalia mchango wa watu -wataalamu wa afya, watendaji, madaktari, n.k- ambao ni muhimu katika kufanya madawa yatimize malengo yaliyokusudiwa.
 
wanapozungumzia sera ya elimu ya Tanzania hawaelewi wala kufeli kwa wanafunzi siyo kawambwa issue iko wazi serikali inawalipa waalimu mshara mdogo hivyo waalimu wanatumia muda mdogo mashuleni,yaani waalimu wa tanzania walishagoma miaka mingi iliyo pita hata utenge sera gani hali ni hivi hivi,marupu rupu kama taasisi nyingine
...Observation sahihi kabisa. Na nadhani tunaisahau hii mara kwa mara tunapojadili vitu kama hivi.

...Sera ya elimu inaongelea mengi, ikiwa ni pamoja na kuboresha shule, mitaala, maslahi ya walimu, n.k. Tatizo, haitekelezwi kwa vitendo. Mathalan, unaposema utaboresha shule, halafu hauzipi maabara wala maktaba, uboreshaji uko wapi? Je, sera ni mbaya au wewe unayetakiwa kutekeleza sera ndiye mbaya? Kumbuka, sera imeainisha nani atafanya nini kwa kushirikiana na nani

...Tukumbuke, anayetakiwa kuboresha maslahi ya walimu si Mh. Kawambwa pekee, bali ni pamoja na Waziri Mkuu, Tamisemi, Utumishi, Fedha, Chama cha Walimu na hata Wazazi. Jukumu hili linahusisha wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom