Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,205
- 5,333
Nimewiwa kulizungumzia hili, kwa kuwa jamii inaendelea kupoteza kabisa ule mguso wa kimazingira na umuhimu wake katika maisha yao.
Katika ngazi ya familia waathiriwa zaidi ni watoto wetu, Mtoto aambiwi wala kufundishwa kwa vitendo kupanda miti na kuitunza, kupenda wanyama na kuwahudumia wala kutunza nyumba na mazingira yake ikiwemo kupalilia na kufanya usafi.
Inasikitisha kuwa na kizazi ambacho mtoto kila aonapo mti mdogo wenye afya njema uwaza kuuharibu tu kwa kuuchuma kama fimbo kwa kuwa ndicho kitu pekee anachoelewa ni matumizi sahihi ya mti huo iwe ni shuleni au nyumbani daima uagizwa akalete fimbo ili aadhibiwe.
Chakusikitisha ni kuwa watoto hawa wanakuwa wakiwa na ile mentality ya uharibifu wa mazingira ndani yao, kwani mitaani kwao wanakoishi kila siku wanachoshuhudia ni utupaji taka ovyo na uchimbaji mchanga barabarani, matumizi yaliyokithiri ya mkaa, ukataji miti kiholela kupisha maendeleo ya vitu kwani miti na uoto kama nyasi uonekana kama kikwazo cha upitishaji wa huduma za kijamii kama maji na umeme, na pia uoto pekee ni matumizi mabaya ya eneo la ardhi.
Leo hii tunalea kizazi ambacho ukipanda miche yako lazima uwe mwenyewe ndiye mlinzi dhidi ya watoto kwa maana badala ya kuwaofia wanyama, watoto wetu ndiyo janga kuu.
Ukijisahau kidogo tu utakuta mtoto wa watu ashang'oa au kuvunjavunja mashina ya miti yako yuko comfortable kabisa hana wasiwasi anaichezea hapo hapo alipoichumia.
Na chakumfanya huna kwa kuwa watoto hao katika fahamu zao hawatambui hata kama kutenda hivyo ni kosa na wala hata jamii yenyewe haioni ikiwa suala kama hilo lina uzito wowote ule.
Anakuja mtu mzima kukuomba umruhusu achume dawa katika mti mmoja hapo nyumbani kwako, pasipo kusita unamruhusu nenda kachume huku ukiwa hauna shaka yeyote ile unaingia zako ndani, punde anarudi kukushukuru kishamaliza haja zake yeye anaondoka.
Unapotoka kwenda kushuhudia alichokifanya unabaki kutikisa kichwa na kufyonza tu, kwa maana ni uharibifu tu utakuta mtu badala ya kuchuma majani katika tawi kaamua kuondoka na tawi kabisa.
Mwingine yeye ni kudonoa-donoa tu viini vya shina la miti akitafuta majani malaini na amalize haja zake haraka aondoke, wengine atachimba mizizi yote anaacha kisha anakata ule mzizi mkuu ili achukue kipande kidogo tu
na kama haitoshi hata kufukia pia ni mtihani atapaacha jinsi alivyopafukuwa pasipo kujalisha mwendelezo wa uhai wa huo mti utakuaje na kwa bahati mbaya anakuwa pengine kaambatana na mwanaye ambaye anashuhudia namna miti inavyopaswa kutendewa hasa isipokuwa yakwako.
Vijijini hali ni mbaya zaidi, mtoto tokea kukuwa kwake anachoshuhudia jamii yake ikipambana nacho kama adui mkubwa huwa ni miti, vichaka na majani.
Muda wote maadui hao watatu (miti, vichaka na majani) popote pale wanapoonekana huwa wanapaswa kuondoshwa kwa sababu yeyote ile iwe kwa kufyekwa, kukatwa au kuchomwa moto kwa kisingizio cha kujipatia kipato, kuandaa eneo la mashamba, kusafisha mji, kuepuka mbu, wanyama nakadhalika.
Unategemea mtoto wa mchoma mkaa ambaye hajawahi kushuhudia hata mara moja baba yake akipanda mti zaidi ya kuikata na kuichomea mikaa na matofali kesho na kesho kutwa aje kuwa balozi mwema wa mazingira yake.
Tunasahau kuwa vitu vidogo vidogo vinavyoonekana kutokuwa na madhara ndiyo baadae upelekea ufa mkubwa usiozibika.
Kama jamii ni wakati wa kubadilika na kuanza kuyajali mazingira yetu kwa vitendo kwa kuwaelekeza watoto wetu juu ya usahihi wa kutenda kwa kujali miti,vyanzo vya maji na uoto wa asili, kulinda na kutunza mazingira yao ili tuepuke kizazi kijacho kisichokuwa na huruma na mazingira, na mazingira nayo hayatokuwa na huruma nao.