Jamani wanajamvi naoma tusaidiane, huyu Tesha aliyekubali kuitwa Katuni wa Mwigulu anatumia muda mwingi kuzungushwa majukwaani badala ya kutafuta/tiwa tiba. Namuomba huyu Mwigulu Mchemba aache kabisa ukiukwaji wa haki za binadamu na amtafutie Tesha madaktari wa ngozi ili wamfanyie upasuaji na apone. Si vyema kabisa kumtembeza mtu hivyo, nawashangaa hata hao Polisi walioruhusu Mwigulu kumtumia hivyo wakati jana tu Kiwia kaenda na watoto wake kudai aonyeshwe mumewe alipo wanasema anavunja sheria. Haya ni maajabu ambayo yapo TZ tu.