Kwanini Tanzania Hatuna Music Charts Zinazoeleweka Kama Billboard Hot 100? Tunakwama Wapi

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Kama unafuatilia muziki kwa umakini utabaini kwamba Bongo hamna music chart ya kueleweka, the likes of Billboard.

Hapa Bongo kila kituo kina charts zake. Clouds ina Clouds FM top 30, EA Radio ina za kwake na vituo vingine vingi.

Ubaya wa charts hizi ni kwamba hazina uhalisia. Zina upendeleo na binafsi nazionaga kama promotional prop tofauti na charts za Billboard.

Charts za Billboard zenyewe zinajumuisha streams from Spotify, Apple Music na DSPs ZOTE, Digital Sales from Itunes na Amazon, Radio Airplay na TV Airplay.

Kwa hiyo unakuta ngoma ikienda namba moja kwenye Billboard Hot 100, hiyo ngoma inastahili kweli na sio kwamba Adam Mchomvu na Mussa Saliboko wa Clouds ndo wameamua hiyo ngoma ikae namba moja.

Sasa swali langu ni, hivi ni kwanini Bongo hatuna such charts? Changamoto iko wapi? Ni technology, funding au hatuna interests?

Nawasilisha.
 
Hapa nchini zitakuwa za kitapeli tu, hongo na rushwa n.k. Hadi mabadikiko yawepo sehemu nyingi..

Bora zisiwepo..
 
Tatizo ni kuaminika, ni nani atakayefanya hivyo apate kuaminika kwamba hana nia ovu dhidi ya msanii fulani?
Muziki wetu umekumbwa na fitna nyingi, ndio maana kila kinachoanzishwa kinakosa support (kuaminika) hivyo hakuna mwendelezo.

Tuzo ngapi zimeanzishwa baada ya Kili Music kukosa kuaminika? Ziko wapi? Nazo zilikosa kuaminika kwa kuonekana ni ajenda ya watu fulani juu/dhidi ya msanii fulani.
Hadi tuondokane na mtazamo wa kuhujumiana ndipo hayo yanaweza kufanyika na kufanikiwa.
 
Tatizo ni mifumo ya kupata taarifa

Wenzetu wana mifumo mizuri sana ya kueleweka ya kupata taarifa

Nyimbo ikitoka ni rahisi kupata taarifa zake za mauzo, streams, radio&tv plays, charts nk

Kama upo interested unaweza kuanzisha ukatumia taarifa za streams za YouTube, Boomplay, zikii nk

Au wasiliana na Billboard myajenge wakiona inalipa uanzishe Tz Billboard kama ilivyo Uk, Canada nk
 
Kama unafuatilia muziki kwa umakini utabaini kwamba Bongo hamna music chart ya kueleweka, the likes of Billboard.

Hapa Bongo kila kituo kina charts zake. Clouds ina Clouds FM top 30, EA Radio ina za kwake na vituo vingine vingi.

Ubaya wa charts hizi ni kwamba hazina uhalisia. Zina upendeleo na binafsi nazionaga kama promotional prop tofauti na charts za Billboard.

Charts za Billboard zenyewe zinajumuisha streams from Spotify, Apple Music na DSPs ZOTE, Digital Sales from Itunes na Amazon, Radio Airplay na TV Airplay.

Kwa hiyo unakuta ngoma ikienda namba moja kwenye Billboard Hot 100, hiyo ngoma inastahili kweli na sio kwamba Adam Mchomvu na Mussa Saliboko wa Clouds ndo wameamua hiyo ngoma ikae namba moja.

Sasa swali langu ni, hivi ni kwanini Bongo hatuna such charts? Changamoto iko wapi? Ni technology, funding au hatuna interests?

Nawasilisha.
Taka za majumban znashindwa manajiwa mnataka mambo ya ziada.. bongo bana
 
Tatizo ni mifumo ya kupata taarifa

Wenzetu wana mifumo mizuri sana ya kueleweka ya kupata taarifa

Nyimbo ikitoka ni rahisi kupata taarifa zake za mauzo, streams, radio&tv plays, charts nk

Kama upo interested unaweza kuanzisha ukatumia taarifa za streams za YouTube, Boomplay, zikii nk

Au wasiliana na Billboard myajenge wakiona inalipa uanzishe Tz Billboard kama ilivyo Uk, Canada nk
Wazo zuri naamini ikitokea taasisi Makini italifanyia kazi hili wazo na walau tunaweza shuhudia tena muziki mzuri
 
Kwanini kila kilichopo USA tunataka kiwepo Tz?

Hata YouTube Wana trending chart Kwa kila nchi ikiwemo Tz...haitoshi?
 
Youtube is not a music streaming service, so Yes HAITOSHI.

Nenda kajielimishe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom