Kwanini Serikali imeweka Mawakili wake kuwatetea akina Mdee? AG akichafuka wakubwa zake watabaki wasafi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Tumetoka kuondoa kesi mahakamani dhidi ya Mbowe serikali ikiwa imechafuka, utaratibu wa kuondoa kesi hiyo ukiwa na maswali mengi KUHUSU uhusika wa viongozi wakubwa. Tumejisafisha lakini Bado atujatakata.

Hali ikiwa Tete tumeingia Tena kwenye mgogoro wa ajabu usiohutaji kujadiliwa. Usiotoa political mailage badala yake unafifisha juhudi na kuwapa mailage akina kibatala bila Hata sababu ya maana.

Serikali imeanza kuvuliwa nguo Kupitia uandaaji wa affidavit kitu ambacho watu makini walipaswa kukiona; tumeanza kuonekana Mawakili wa Jamhuri awaelewi .

Tutaendelea na kesi hizi tukidhani tunaikomoa Chadema lakini tukumbuke wapo Wana CCM wanalalamika chama kuendelea kuikumbatia wageni Kwa kuwapa Ubunge, udiwani ukuu wa wilaya na mkoa Hadi uwaziri huku Wana CCM wakisota bench. Wapo Wana CCM wanajua 2025 akina Halima watapitishwa kwa upendeleo na hivyo wao wataendelea kusota. Wapo Wana ccm wanaelewa mchezo wa wapinzani kujipitisha wanunuliwe wajijenge kiuchumi wakijiandaa kuivuruga CCM

Najiuliza washauri wa serikali wanaona CCM inanufaika vipi na migogoro hii? Kwanini tusishtuke kwamba wapo wanasayansi wa siasa wanamvuruga mwenyekiti Ili Hali 2025 iwe Tete wapige fedha Kupitia dola wakimwaminisha akubaliki?

Kupanga ni kuchagua
 
Hakuna wakili wa serikali anatetea mtu binafsi.

Sheria inataka serikali ikishitakiwa AG awe part ya kesi.

NEC imeshitakiwa hivyo mawakili wa serikali lazima wawepo.
sasa kwenye hilo suala la kina mdee kuitaka mahakama kuangalia kama taratibu za katiba ya chadema imefuatwa .sasa hapo serikali (NEC) imeshtakiwa kivipi .
Hilo ni suala binafsi la hao kovid 19 na chama chao
 
Yaani hapo ndio unaona mchongo wao ulivyp bugi. AG ameshindwa kuishauri vyema serikali amebaki kupelekeshwa na CCM wasio jitambua.
Kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wao badala ya kudili na Chadema wana kimbilia kuihusisha na NEC sijui hao wanahusikaje na uanachama wa wanaofukuzwa.
 
Tumetoka kuondoa kesi mahakamani dhidi ya Mbowe serikali ikiwa imechafuka, utaratibu wa kuondoa kesi hiyo ukiwa na maswali mengi KUHUSU uhusika wa viongozi wakubwa. Tumejisafisha lakini Bado atujatakata.

Hali ikiwa Tete tumeingia Tena kwenye mgogoro wa ajabu usiohutaji kujadiliwa. Usiotoa political mailage badala yake unafifisha juhudi na kuwapa mailage akina kibatala bila Hata sababu ya maana.

Serikali imeanza kuvuliwa nguo Kupitia uandaaji wa affidavit kitu ambacho watu makini walipaswa kukiona; tumeanza kuonekana Mawakili wa Jamhuri awaelewi .

Tutaendelea na kesi hizi tukidhani tunaikomoa Chadema lakini tukumbuke wapo Wana CCM wanalalamika chama kuendelea kuikumbatia wageni Kwa kuwapa Ubunge, udiwani ukuu wa wilaya na mkoa Hadi uwaziri huku Wana CCM wakisota bench. Wapo Wana CCM wanajua 2025 akina Halima watapitishwa kwa upendeleo na hivyo wao wataendelea kusota. Wapo Wana ccm wanaelewa mchezo wa wapinzani kujipitisha wanunuliwe wajijenge kiuchumi wakijiandaa kuivuruga CCM

Najiuliza washauri wa serikali wanaona CCM inanufaika vipi na migogoro hii? Kwanini tusishtuke kwamba wapo wanasayansi wa siasa wanamvuruga mwenyekiti Ili Hali 2025 iwe Tete wapige fedha Kupitia dola wakimwaminisha akubaliki?

Kupanga ni kuchagua
Ndo ujue:-
Halima na genge lake, spika, serikali, ccm.. lao moja
 
Tofautisha AG na DPP
Taahi.ra hilo lisikupotezee muda, hii mijitu hujitia kujua kila kitu wakati kuchwani empty kabisa, mfano huyu mleta mada hajui hata kama AG pia kashtakiwa kwenye hiyo kesi na ndo sababu ya kupeleka mawakili wa serikali.
 
Tusidanganyane, serikali ina mkono kwenye issue ya wakina Mdee, tena kuanzia bungeni kwa Spika Tulia.

Hao mawakili wa serikali walitumwa kuke kuwaongezea nguvu mawakili wa kina Mdee for special purpose, ili kuwalinda vibaraka wao wanaowatumia kule bungeni kwa maslahi yao.

Jaji nae akaungana na mawazo ya Spika kuhakikisha kina Mdee wanaendelea kukaa bungeni, tena hii ni baada ya ile mbinu yao ya kwanza ya kutaka kusikiliza kesi upande mmoja bila kuwa summon Chadema kushindwa.

Kujaribu kuutetea huu ujinga kwa sababu yoyote ni uzezeta tu, kama Samia alidhani kukaa na Mbowe ikulu pekee ndio kipimo cha maridhiano amefeli, kwa mtindo huu ni bora awaite wakina Zitto akakae nao milele.
 
Kwahiyo AG ndio akawatuma mawakili wa serikali wakawasimamie wakina Mdee kuiomba mahakama isiwaondolee ubunge wao?

Yani unaemshtaki atume watu wake ili waje kukutetea?

Mjue tu ujinga wenu sio wa wote.
Kwa hiyo unamaanisha akina Kibatala pia walienda kuiomba mahakama isiwaondolee ubunge wao? vichwani mmejaa ug.oro tupu.
 
Back
Top Bottom