Kwanini Serikali haiajiri Madaktari (MD) wakati kuna upungufu mkubwa, inaajiri CO (Clinical Officers) na manesi?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Ni ajabu sana kuona Daktari aliyesoma miaka 5 na kukaa hospitali mwaka mmoja yupo mtaani kwa kukosa ajira, juzi nimekutana na daktari aliyemaliza mwaka 2020 Udom, ni dereva bodaboda.

Nimeambiwa sasa hivi katika ajira tamisemi 95% wanaajiri clinical officers (diploma) na nurses na wizara ya afya haijaajiri kabisa toka 2015 kama imeajiri hawafiki hata madaktari 100.

Kila mwaka kuna madaktari MDs around 2000 wanaopata leseni, je hawa wote watafanya kazi wapi.

Kwa sasa kwa Tanzania medicine siyo kozi ya kusoma ni bora mtu asome nursing au CO kuliko kusota miaka 6 na uishie kufungua duka la vyombo au kuendesha boda.

Wakati ajira za MDs zinasuasua hivi, kwenye hospitali nyingi za serikali kuna upungufu mkubwa sana wa MDs.

Serikali itafakari sana juu ya hili, mtaani kuna MDs zaidi ya 3000 pengine ambao hawana sehemu za kufanya kazi.

Ushauri wizara ya elimu na wizara ya afya zishirikiane kuweka mkakati haraka wa kuounguza idadi ya wanafunzi wanao soma MDs.

Au iweke utaratibu ili kusoma medicine ni lazima uwe usome kwanza CO na ufanye kazi walau mwaka mmoja, na ifute watu kusoma direct kozi za medicine wakitokea high school.

Tutakuja kuwa taifa la vilaza hadi kwenye issue serious za matibabu. Daktari anakaa mtaani miaka 3 ndio anaajiriwa, huyo si atakua amesahau kila kitu?

Waziri wa afya na waziri wa elimu pamoja na waziri wa tamisemi mna la kujibu kuhusiana na jambo hili.

Ni matumizi mabaya ya resource, Daktari kuendesha bodaboda wakati kuna watanzania wanakufa kwa kukosa wahudumu wenye uelewa mzuri wa mwili wa binadamu.
 
Ningejua kwamba serikalini ni njaa kiasi hiki nisingethubutu kuja serikalini ningebakia kwenye shirika(MDH)
 
Doctor hafi njaa go outside our country unapata kazi nje nje ukisema cha nn wenzio wanasema nitakipata wapi,Malawi Mozambique hata Kwa museven hapo they need you guys hapa anaejua siasa ndio anakula hela sio kwenye taaluma
 
Back
Top Bottom